Benjamini Netanyahu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2014
- 102,675
- 126,930
Huyu ajuza angekuwa anajua kama kuna MUNGU asingekuwa mshirikina
Kina roho mbaya kama sura akeAnaelewa maana ya haki??
Hovyo kabisa pale hakuna Spika ni debe tupunani aombee ujinga spika wa ajabu ajabu tangu Tanganyika ipate uhuru
Wamefikia hatua ya kumdhihaki Mungu hawa. Ni kama jambazi anaenda nyumba ya ibada kutaka aombewe ili azidi kuiba.Huo uchaguzi wanashindana nani na nani kugombea nini?Atulie na kujisikiliza aliyoongea na apime kwenye nafsi yake kuna ukweli kiasi gani!
Wanataka ubatili wao uombewe.Wamefikia hatua ya kumdhihaki Mungu hawa. Ni kama jambazi anaenda nyumba ya ibada kutaka aombewe ili azidi kuiba.
Huu mshumaa una mambo ya kijinga sana.Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson ametumia mazishi ya aliyekuwa Askofu Mkuu wa kwanza wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Askofu Immanuel Lazaro kuwataka Watanzania kuliombea Taifa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ili viongozi wapatikane kwa haki.
Kauli hiyo ameitoa Mei 27, 2025 wakati akitoa salamu za Serikali katika ibada ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa la TAG-Jerusalemu Mudio, lilipo katika kata ya Masama, Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro.
"Kwa sababu huko mbele tunao uchaguzi niwaombe sana, pamoja na kwamba huwa mnatuombea sana sisi viongozi lakini pia mnaliombea Taifa letu, niwaombe mwaka huu tuliombee zaidi Taifa letu, mwaka huu tuwaombee viongozi watakaopatikana kupitia uchaguzi wa haki,"
Amesema, "lakini hao watakaopatikana kwa haki Biblia imetuagiza kuheshimu wenye mamlaka, ni vizuri sana sisi tumjuao Kristo kupanga nini cha kusema, cha kufanya, kujua namna ya kuenenda mbele ya viongozi wetu, wewe umjuaye Kristo usiwe sehemu ya kulikosea neno."
Akiendelea na salamu za Serikali Dk Tulia, amewataka pia Watanzania kuwaombea viongozi watakaopatikana kwa haki katika uchunguzi huo wa Rais, wabunge na madiwani.
"Wakati mwingine Mungu atatupa neema, hata wale wafalme wa zamani, sasa hivi ni viongozi wa nchi zetu kwa hiyo unavyowasoma wale na yale mamlaka yao na nguvu yao amini kwamba neno linaposema umuheshimu mwenye mamlaka ni kwa sababu hakuna mamlaka isipokuwa itokayo kwa Mungu,"amesema Dk Tulia.
Askofu Lazaro ambaye alizaliwa Oktoba 4, 1937, alifariki Mei 17, 2025 katika Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Kaskazini KCMC, siku na mwezi sawa na aliyofariki mke wake, Evagrace mwaka 2017.
Askofu Lazaro ambaye amezikwa Mei 27,2025 katika eneo la Kanisa la TAG -Jerusalemu Modio Masama, alianza huduma za kiroho mwaka 1959, na mpaka anastaafu huduma hiyo mwaka 2019 alikuwa amefikisha miaka 60 ya utumishi wake.
Hatuombei chochote maana wewe mwenyewe umenukuliwa ukisema kwa kipindi hiki cha uchaguzi hapo tayari kwenda mbinguni. Ulimaanisha kwamba mtaiba kura na kufanya chochote haramu alimradi mshinde uchaguzi! Watu aina yenu hatuwahitaji kabisa! Na kwa dhihaka yako kwa Mungu impendeze akusogeze mbele ya Baraza la haki mbinguni ukachukue tiketi yako tayari kwa safari ya kwenda kwenye moto wa milele.Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson ametumia mazishi ya aliyekuwa Askofu Mkuu wa kwanza wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Askofu Immanuel Lazaro kuwataka Watanzania kuliombea Taifa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ili viongozi wapatikane kwa haki.