Dkt. Wilbert Kleruu - Utata wa kifo chake, historia na maisha yake

SITASHANGAA UTAWALA HUU KUTOA MATUKIO KAMA HAYA MAANA TUNAPOELEKEA KWA UBABE NA KUWAPIGA RAIA KUNA WENGINE HAWATAKUBALI

Mfano mzuri wale wakuu wa wilaya na mikoa wanaochapa watu
 
SITASHANGAA UTAWALA HUU KUTOA MATUKIO KAMA HAYA MAANA TUNAPOELEKEA KWA UBABE NA KUWAPIGA RAIA KUNA WENGINE HAWATAKUBALI

Mfano mzuri wale wakuu wa wilaya na mikoa wanaochapa watu
Umeona eennhh???!!!,Wanasaikolojia wanasema Kuna mwisho wa Binadamu kuvumilia,akishavuka viwango hivyo binadamu anaweza kufanya chochote bila kuogopa chochote,hiyo wanaita'The point of no return", Hapo unasikia harufu ya damu ya binadamu tu.
 
Mwamwindi alionewa na Mahakama kwa kuhukumiwa kifo kwa mauaji ya 'kukukusudia'

Mtu kakufuata Shamba, anatoa maneno ya kashfa na kejeli

Umeamua kumkwepa unaondoka na kurudi Nyumbani bado anakufuata kwa nyuma anatoa maneno ya kejeli, mfano anapokejeli Makaburi ya Wazee wako uliowazika na kuwaita 'mirija' wenzio… hii ni provaction ya wazi kabisa sema ndo hivyo tena 'Mlalamilaji,ndio Mwendesha mashtaka, ndie Jaji, ndio mtoa hukumu na ndie anaesaini hati ya kifo'

Ujasiri wa Mwamwindi ulileta nidhamu sana kwa Ma RC na DC Nchi nzima


Said Mwamindi alikuwa mchapakazi sana aliekuwa anapambana na jamii ya watu wavivu

'Kwanini mje mpore mashamba yetu na kugeuza ya kijiji wakati kuna Mapori mengi tu…'

Miaka 20 baada tu ya kadhia hiyo Ujamaa unapelekwa Mortuary na tunaanza tena kudalalia Ubepari


Kwangu Mzee Said ndio Shujaa wa muda wote, wangekuwepo akina Mwamindi zama hizi ufala fala wa kufokeana na kudhalilishana hadharan ungeshapatiwa 'Alkasuus'
 
Mnara wa Kreluu kwa nyuma nyumbani kwetu Mkungugu.. home sweet home.
 
Hakika hata mimi namkubali Sana huyu baharia, Siku hizi unakuta kimjamaa kimepata kacheo basi full dharau.
 
Samahani chief kwa elimu tu, hukumu zingine 2 zilizosainiwa na Nyerere ni zipi?

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
 
Alikuwa daktari wa nini huyu Kleruu? Alikuwa kabila gani?
Inasemekana alikuwa na shahada ya uzamivu akiwa na umri mdogo tu wa miaka 29 aliyoipata kule Marekani. Aliporudi nchini alikataa kazi ya kufundisha pale UDSM akachagua kufanya kazi pale Lumumba kama Afisa wa TANU. Alikuwa ni mtu aliyeamini sana siasa za ujamaa. Ndipo Mwalimu alipompa kazi ya ukuu wa mkoa. Jamaa alikuwa ni mtu mmoja katili, jeuri, mwenye dharau na nyodo za hali ya juu. Alikuwa hapendwi hata na maofisa wenzie wa serikali kutokana na tabia zake mbaya.
 
Alhaji Mwamwindi huyu ndio shujaa wa kweli hakukubali siasa mbovu za Nyerere za kunyanganya watu mali zao. Mungu amlaze pahali mema Shujaa wa Tanganyika Alhaji Mwamwindi
Endelea kuvutia mibange yako chooni afande selle.
 
Dr. Kleruu ni Sabaya wa zama zetu. Alistahili kupata alichopata
 
Wewe ni mtizamo na msimamo wako kuhusu yafuatayo:
1.Hukumu iliyotolewa kuhusu Mwamwindi kumuua Kleruu,je ni sahihi?
2.Je,Mwamwindi kumuua Kleruu,ilikuwa kosa au sahihi?
3.Ingekuwa wewe ndiye Mwamwindi,je,ungefanya nini?
 
Yanaweza yakawa siyo matatizo ya akili as such bali uzalendo wao kwa nchi ndiyo uliosababisha wakawa kama wana matatizo ya akili, kwa sababu kwenye vita ya mwaka 1978, inasemekana baadhi yao (watoto wa mwalimu) walikuwa kwenye kikosi cha mizinga. Kwa teknolijia ya kipindi hicho, askari waliokuwa wnafanya kazi kwenye kikosi hicho baadhi walikuwa wanaonyesha dalili kama zimefyatuka kidogo
 
Samahani chief kwa elimu tu, hukumu zingine 2 zilizosainiwa na Nyerere ni zipi?

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
Sina uhakika sana ila kuna mtu mwingine aliwahi kumuua mtu nadhani mke wake kwa kumchoma akiwa ndani ya gari pale mlima wa Kironga na hatimaye kulisukuma gari hilo likaporomoka chini kwenye korongo refu nia ikiwa alipwe hlea ya BIMA. Huyu yeye alitengeneza ajali ya makusudi kwa kuchoma mtu ndani ya gari ili aweze kulipwa hela za bima. Niliwahi kusoma humu na pengine details nilizotoa hapa zinaweza zikawa haziko sahihi sana, nilishapoteza kumbukumbu
 
Makaburi yana maana kubwa hata ki-Biblia.
Waisrael walipokuwa wanatoka utumwani Misri kwenda kwenye nchi ya ahadi Kaanani, walihama wakiwa na mifupa ya Yusufu kwa maana kuwa walihama na kaburri la Yusufu kwa sababu alikuwa ameagiza hivyo
 
Huyo mtu alikuwa muasia ambaye alimsukumiza mkewe aliyekuwa na Bima kubwa ya maisha kwa kampuni moja ya huko UK.
Na ni milima ya Lukumburu kuelekea Songea sio kitonga. Milima hiyo kabla ya barabara kuwa ya lami ilikuwa ya hatari sana.
Upelelezi wa hapa ndani uliona ile ilikuwa ajali hadi ndugu wa mwanamke marehemu walipo hire wa pelelezi binafsi toka Scotland yard ndio waligundua kila kitu.
Jamaa alinyongwa, signed by mchonga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…