Nadhani katika kusaini hukumu ile Mwl Nyerere alikuwa katika capacities mbili: Ya kwanza kama Rais wa nchi ambaye sheria inasema ndiye atakayeridhia utekelezwaji wa hukumu ya kifo inapotamkwa na mahakama, lakini ya pili ni capacity ya kibinadamu ya kutaka kumlipia rafikiye kisasi, ambayo hii inaelekea ilimzidi. Imagine katika miaka 23 ya uongozi wake, ni watu wengi sana walihukumiwa adhabu za kifo, lakini aliridhia 3 tu, mojawapo ikiwa hii ya Mwamwindi. Labda zingeletwa na hizo hukumu nyingine alizosamehe tukaona hazikumgusa binafsi naweza kufuta maneno yangu, lakini nahisi kutekelezwa kwa hukumu hii haraka haraka kulichangiwa pia na ukweli kwamba kosa lililotendwa lilimuumiza Nyerere binafsi. Hivi kwa mfano ukipigana na mtu mtaani ukamuumiza halafu ukakamatwa ukashitakiwa mahakamani, na huko ukakuta hakimu ni baba mzazi wa mlalamikaji, unatarajia nini? Sisemi ilikuwa sawa Nyerere kuendeshwa na hisia binafsi, lakini tunapaswa kuangalia pia namna ya kudhibiti hali kama hii. Katika mahakama zetu kuna utaratibu (sijui kama umeandikwa au la) kuwa hakimu akiona kesi husika ana maslahi nayo, huwa anajitoa na kuomba ipangiwe hakimu mwingine. Kwa rais wa nchi hali ikoje? Hivi mtu akihukumiwa kunyongwa kutokana na kutenda jambo ambalo liligusa maslahi binafsi ya rais (rafiki yake, familia yake nk), rais anaweza kusema kuwa 'anajitoa' katika suala la kuridhia utekelezwaji wa hukumu hiyo?