Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,564
Kumbe vichaa walikuwa tangu zamani?Hivi nani anaweza kutoa maelezo sahihi "Ni kwa nini Mwalimu alitia saini kifo cha Mwamwindi, wakati ripoti ya Madaktari wakiongozwa na Dr.Pendaeli waliithibitishia Mahakama kwamba Mtuhumiwa alikuwa na Ugonjwa wa Akili?".
Alhaj Mwamwindi aliua Desemba/1971 na mapema June/1972 kesi ilikuwa imekwishamalizika...Ni vipi kesi hii ya mauaji iliyohitaji uchunguzi wa muda mrefu iliendeshwa kihara haraka namna hiyo?Ni kweli kwamba Mwalimu alitia saini adhabu ya kifo kwa sababu tu kifo kilimuhusu rafiki yake?Mbona alikawia na hatimaye kumuacha huru Mama Liundi ambaye aliuawa watoto wake wawili kwa kuwatilia sumu kwenye chakula?(wakati hukumu ya mahakama ilikuwa ni adhabu ya kifo?)..
Kama mtakumbuka Mwalimu alikataa kuonana na watu kutoka England ambao walifuatilia kesi ya Mwamwindi....Mwl aliwaambia anafikiri waondoke tu...kwa sababu walikuja mwezi April/1972 siku ambayo karume nae alipigwa risasi Zanzibar....mara baada ya mazishi ya Karume Mwalimu alirudi Butiama kwa siku 7 na kusema wazi kwa kiingereza kwamba inabidi afanye "re-evaluation ya behaviour yake".Ni kwa nini alisema maneno hayo? unafikiri hiyo iliharakisha kusaini kifo cha Mwamwindi? au aliona yaliyomtokea Karume yanaweza kutokea kwake pia?Wakulu mnaolifahamu hili tunaliombea maelezo...