Dkt. Wilbert Kleruu - Utata wa kifo chake, historia na maisha yake

Dkt. Wilbert Kleruu - Utata wa kifo chake, historia na maisha yake

Miaka ya zamani kulikuwa na mashujaa hasa kwa sasa hivi mtu anampiga mke wake vingumi viwili akizimia anakwenda kujiua na kutuachia barua ambazo wanazichukua police
 
WhatsApp Image 2019-01-15 at 23.12.58.jpeg

Siku ya Krismasi 255/12/2020, ni miaka 49 imepita toka Mnyalukolo, SAID ABDALLAH SIULANGA MWAMWINDI, ammimimie risasi na kumuua aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Iringa, marehemu Dr. WILBERT KLERUU. Mauaji hayo yaliyokea tarehe 25/12/1971 kijijini Mkungugu, Isimani, Iringa.

Dr. WILBERT KLERUU alikuwa ni mzaliwa wa Mwika, Kilimanjaro ambaye alikuwa ni mmoja wa Watanzania wachache wakati huo waliokuwa na shahada ya uzamivu(PHD) ya uchumi wa kijamaa.

Dr. KLERUU alikuwa ni kipenzi cha Baba wa Taifa, Mwalimu JK NYERERE, kutokana na weledi na utendaji wake usio na mfano. Mwanazuoni mwa mwaka 1971, DR.

.KLERUU alikuwaamehamishiwa mkoani Iringa kutokea Mtwara.

Dr. KLERUU alikuwa ni kiongozi machachari sana na ilikuwa kawaida kwake na alikuwa hana hiana kuwafokea hadharani watumishi wa umma wazembe. Kwa hakika, Dr. KLERUU alikuwa mbabe sana. Akiwa Iringa, kuna wakati gari yake ilipigwa "overtake" na gari hilo lililompiga"-overtake" likamziba kwa mbele. Kufumba na kufumbua, Dr. KLERUU alishuka kama komandoo na kwenda kumuwasha vibao dreva wa gari hilo! Dr. KLERUU, mara kwa mara, alipenda kuwafokea watu kwa kuwaambia "Hamnijui Mimi? Kawaulizeni watu wa Mtwara" na yeye hakuwa mtu wa kukaa ofisini kama viongozi wengi wa wakati huo, bali alijumuika na wananchi na kufanya nao shughuli za maendeleo bega kwa bega ambapo ilikuwa ni kawaida kwake kushika jembe kwa masaa kadhaa bila kula!.

Kipindi hicho kulikuwa na kampeni kubwa ya kuwafanya wananchi walime mashamba ya pamoja na hivyo wakulima waliokuwa na mashamba makubwa walinyang'anywa, kitendo ambacho hakikuwapendeza Wanyalukolo waliokuwa matajiri wenye mashamba makubwa ya mahindi.

Dr. KLERUU alihamishiwa Iringa ili akatekeleze mpango huo wa serikali na alipofika tu akatangaza kwamba mashamba yote binafsi yanapaswa kuwa ya ujamaa kufikia Novemba 1971.

Bw. MWAMWINDI alihamia eneo la Mkungugu, Isimani mwaka 1954 akitokea Iringa mjini alikokuwa dreva. Alianza kilimo kidogo kidogo hatimaye akawa na mashamba makubwa ya mahindi ya hekari takriban 160. Akawa analima mashamba yake kwa trekta katika eneo hilo ambalo awali lilikuwa ni pori. Kipindi hicho, hakukuwa na sehemu Tanzania iliyokuwa ikizalisha mahindi mengi kama Isimani.

Jumamosi ya tarehe 24/12/1971, Dr. KLERUU alitembelea mashamba mbalimbali maeneo ya Tarafani, Igulu na Ndolela kuhamasisha kilimo cha pamoja. Kesho yake, Jumapili ya tarehe 25/12/1971, Dr. KLERUU( ambaye hakuwa na Jumapili wala skukuu) aliendelea na shughuli hizo za kutembelea mashamba ya wakulima.

WhatsApp Image 2019-01-15 at 23.12.58(1).jpeg

Muda wa saa 11 jioni, Dr. KLERUU alifika kwenye shamba la MWAMWINDI na kumkuta akilima kwa trekta lake. Pamoja nae kulikuwa na mtoto wake(Mohamed) na watu wawili aliowaajiri( Yadi Chaula na Charles Mwamalata), Bw. Joseph Kusava ambaye ni mkwe wake pamoja na wake zake waliokuwa wakishirikiana nae kulima siku hiyo. Dr. KLERUU alifika shambani hapo akiendesha gari lake binafsi aina ya Peugeot 404 rangi ya bluu na ubavuni ikiwa imeandikwa RC-Iringa.

Baada ya kushuka alimfuata moja kwa moja MWAMWINDI na kuanza kumuhoji maswali mengi kwanini hataki mashamba yake yawe ya ujamaa. Akamwambia "Unafanya nini hapo?"Shuka shenzi we". MWAMWINDI akamuuliza "kwanini unanitukana?" Dr. KLERUU akamjibu "Funga mdomo wako, n'ge n'ge n'ge nini? Kwanini nawaambia hamsikii? Blood fool".

Katika eneo hilo walikuwa wao wawili tu kwani watu wengine walikuwa mbali kidogo. Dr. KLERUU aliyekuwa na kawaida ya kutembea na kifimbo kidogo akakitumia kumchomachoma nacho MWAMWINDI.

MWAMWINDI akafura sana hivyo akaanza kwenda ndani kupitia eneo la makaburi ya baba yake na ndugu wengine huku Dr. KLERUU akimfuata na alipoyaona makaburi akasema "Tazama unaendelea kujenga nyumba za kudumu". MWAMWINDI akamjibu "Hizi sio nyumba, ni mahali ninapozika ndugu zangu". Dr. KLERUU akajibu "Ni mahali unapozikia mirija wenzio, mbwa we!".

Mnyalukolo MWAMWINDI akawaamehamaki sana. Akasema "Swela", akaingia ndani akachukua gobore akatoka nalo nje na kumfyatulia risasi Dr. KLERUU ambaye alianguka na kufariki hapohapo!!! MWAMWINDI aliuchukua mwili wake akauweka kwenye buti ya gari ya Mkuu huyo wa Mkoa, akachukua na kofia ya Pama ya Mkuu wa Mkoa akaivaa yeye na kuanza safari ya kilometa 40 kwenda Iringa mjini.

Mjini Iringa, watu walishangaa kuona gari ya Mkuu wa mkoa inapita upande wa kulia kwa vile mtaa wa Jamatini ulikuwa ni "One way" lakini wakahisi huenda Mkuu wa mkoa ana dharura. Saa 1 jioni, MWAMWINDI akafika kituo kikuu cha polisi akaenda moja kwa moja kaunta akamkuta PC MBETA KASONDA na kukwambia "Ebu nenda kwenye buti ukaitoe mbwa yenu nimeishaiua" na kumkabidhi bunduki pamoja na funguo za gari. PC KASONDA hakuamini macho yake alipouona mwili wa Dr. KLERUU ukiwa umetapakaa damu. Dr. KLERUU alikuwa amevaa ovaroli nyeusi na miwani.

Hivyo, mara moja PC KASONDA akamuweka MWAMWINDI chini ya ulinzi. Mtu mwingine aliyekuwepo kituoni hapo ni mzee DAVID BUTITINI(ambaye alikuwa askari polisi na baadaye kada wa CCM Iringa). Tarumbeta likapulizwa na askari wakakusanyika na kupewa rasmi taarifa ya kifo hicho cha Mkuu wao wa mkoa na gari lake likahifadhiwa nyuma ya kituo cha polisi.

Askari wanne wakaenda kuleta kitanda cha magurudumu toka hospitali na hatimaye mwili wa Dr. KLERUU ukapelekwa "mortuary". Kesho yake, siku ya jumatatu, mji mzima wa Iringa uligubikwa na simanzi kubwa.

Kuna kundi la watu ambao walikuwa wakimchukia sana Dr. KLERUU kutokana na aina ya uongozi wake hivyo lilipopata tu taarifa za kifo chake wakanunua makreti ya bia usiku huohuo na kuanza kunywa kwa kushangilia hadharani! Msako ulipoanza usiku huohuo, jamaa hao walikuwa wa kwanza kukamatwa!.

Mzee BUTININI ambaye pia alikuwa Mtwara wakati DR. KLERUU alipokuwa Mkuu wa Mkoa, anakiri kuwa ni kweli DR. KLERUU alikuwa mtu wa shoka- "Ni kweli hata kule Mtwara alionekana mtemi sana mwenye kuhimiza mambo kwa nguvu. Lakini lazma muelewe maeneo ya Mtwara yalikuwa ya vita na tulikuwa tukiwasaidia ndugu zetu wa Frelimo hivyo kule kulihitaji mtu kama DR. KLERUU. Mtwara DR. KLERUU hakukumbana na upinzani ila Iringa hali ilikuwa tofauti. Kwa mawazo yangu, Dr. KLERUU alipaswa kwanza kujifunza juu ya mila na desturi za watu wa Iringa. Maana watu wa Iringa ni watu wa Iringa tu."

Mauaji hayo ya Dr. KLERUU yalimsikitisha sana Mwalimu NYERERE, wakuu wa mikoa na wananchi mbalimbambali. Lilikuwa ni tukio lililoongelewa nchi nzima. Majirani na wazee wengi waliokuwa wakilima pamoja na MWAMWINDI walisombwa na vyombo cha usalama na kumwekea ndani kuisaidia polisi ambapo walikuwa wakikamatwa na kusafirishwa usiku kwa ndege za jeshi.

Takribani watu 30 walikamatwa wakiwemo wazee maarufu kama IBRAHIM KHALILI, PESAMBIL, MURSALI na wengineo na kupelekwa sehemu mbalimbali za nchi mf Shinyanga, Mwanza na Zanzibar. Cha kusikitisha ni kwamba ndugu zao hawakujua wamepelekwa wapi! Aidha, nyumbani kwa MWAMWINDI huko Mkungugu kukawa kunalindwa na askari wa FFU muda wote.

Kitendo cha kukamatwa majirani na marafiki wa MWAMWINDI kilileta uhasama mkubwa baina ya ndugu wa majirani hao na familia ya MWAMWINDI.

Ikabidi mwanae (AMANI MWAMWINDI)(21) alazimike kutafuta kibali cha DC Iringa kwenda gereza la Dodoma alikokuwa anashikiliwa MWAMWINDI. Alipoganikiwa kukipata alikwenda na akamueleza hali hiyo ambayo ilimsukitisha sana Mzee MWAMWINDI. AMANI akamshauri baba yake aandike barua kwa Rais NYERERE, nae akafanya hivyo siku hiyohiyo. Katika barua hiyo, MWAMWINDI alimueleza Mwalimu kwamba yeye ndiye aliyemuua Dr. KLERUU hivyo wengine hawahusiki hivyo waachiwe. Baada ya kupita siku kadhaa, wazee hao majirani wakaachiwa na kurejea kijijini hapo, Isimani. Hata hivyo, tafrani hiyo iliyokuwaimewakumba ikafanya wengi wahame eneo hilo kwani waliishaona "togwa limeingia nzi"!.

Upelelezi wa mauaji hayo ulienda haraka na MWAMWINDI akafunguliwa kesi ya mauaji ya kukusudia Mahakama kuu. Kesi ilipoanza kusikilizwa, ilivuta hisia za watu wengi na umati wa watu uliokuwa ukitamalaki kila siku mahakamani ulikuwa "si wa nchi hii!.

Tarehe 2/10/1972, baada ya mashahidi wa pande zote kutoa ushahidi wao akiwemo RPC wa Iringa (Abubakar Hassan) aliyetoa ushahidi upande wa MWAMWINDI kwamba hakuwa na taarifa kwamba Mkuu huyo wa Mkoa angetembelea eneo hilo ndio maana hakumpa "Police escort", Jaji GABRIEL CHIKE ONYIUKE toka Nigeria(aliyehudumu Tanzania toka 1970-1973) alimtia MWAMWINDI hatiani na kumuhukumu kunyongwa hadi afe.

Hii ilikuwa ni baada ya kuukataa utetezi wake kwamba alitenda kosa hilo baada ya kurukwa na akili na pia alikasirishwa "provoked" na marehemu, Mh. Jaji aliona kwamba ingawa ni kweli MNYALUKOLO wa kawaida huwa si mtu wa mchezo-mchezo anapodhihakiwa hasa mbele za wake zake lakini kitendo cha MWAMWINDI cha kwenda ndani kufuata bunduki kilionesha, pasina shaka, kwamba aliua kwa kudhamiria.

Adhabu hiyo ya kifo ilitekelezwa mara moja kwani Mwalimu NYERERE alisaini hati ya kifo cha MWAMWINDI

. Hayo hiyo, ilikuwa ni moja ya hati tatu za vifo zilizosainiwa na Mwalimu NYERERE kuidhinisha kunyongwa kwa binadamu katika uongozi wake wa miaka 24 katika taifa hili.

Kesi hii ilikuwa ya aina yake na haikuchukua hata mwaka mmoja toka tukio kutokea na adhabu kutolewa tofauti na kesi nyingine za mauaji ambazo, kwa kawaida, huchukua miaka mingi kabla ya hukumu kutolewa. Kesi hii ilichukua miezi kumi tu.

Baada ya msiba, familia ya DR. KLERUU ilirudi Kilimanjaro. Hata hivyo, Mwalimu NYERERE na KARUME na baadae ABDU JUMBE walikuwa karibu sana na mjane wa DR. KLERUU na wakawasomesha wanawe nchini Urusi na Bulgaria. Aidha, viongozi wengine waliwatia moyo na kuwafariji sana mf. Marehemu Mzee RASHID KAWAWA na mama GETRUDE MONGELA. Dr. KLERUU aliacha watoto wanne ambao ni Eva, Andrew, Carmen na Edwin.

Mwezi Machi 2014, familia ya DR. KLERUU na ya MWAMWINDI zilikutana kwa furaha ili kusameheana kwa tukio hilo. Bi. EVA KLERUU(60) ambaye ni mtoto mkubwa wa Dr. KLERUU na Bw. AMAN MWAMWINDI(67) (aliyekuwa Meya wa mji wa Iringa) walifanya jambo hilo la kihistoria na hivyo kuyaishi kivitendo maandiko ya vitabu vitakatifu yatutakayo wanadamu kusameheana. Picha hii chini inawaonesha wawili hao wakiwa na bashasha baada ya tendo hilo la kihistoria na lisilo la kawaida.

Mnara wa DR. KLERUU umejengwa kwenye "mji" wa MWAMWINDI mahali ambapo alipigwa risasi . Nyumba ya Mkuu wa Mkoa DR. KLERUU bado ipo. Picha hizi hapa chini zinamuonesha Mnyalukolo MWAMWINDI baada ya kujisalimisha polisi pamoja na nyumba ya DR. KLERUU.

REST IN PEACE:

1. Dr. W. KLERUU

2. S. A. MWAMWINDI
 
KUTOKA MAKTABA[emoji116]

SAID MWAMWINDI MKULIMA ALIYEMUUA MKUU WA MKOA
[emoji117]Ilikua ni mnamo mwaka 1971 siku ya Krismasi ni miaka 48 imepita toka Mnyalukolo SAID ABDALLAH SIULANGA MWAMWINDI ammimimie risasi na kumuua aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Iringa marehemu Dr. WILBERT KLERUU.
Mauaji hayo yaliyokea tarehe 25/12/1971 kijijini Mkungugu Isimani Mkoani Iringa.

[emoji117]Dr. WILBERT KLERUU alikuwa ni mzaliwa wa Mwika Kilimanjaro ambaye alikuwa ni mmoja wa Watanzania wachache wakati huo waliokuwa na shahada ya uzamivu(PHD) ya uchumi wa kijamaa.
Dr. KLERUU alikuwa ni kipenzi cha Baba wa Taifa Mwalimu JK NYERERE kutokana na weledi na utendaji wake usio na mfano. Mwanzoni mwa mwaka 1971 DR.KLERUU alikuwaamehamishiwa mkoani Iringa kutokea Mtwara.

[emoji117]Dr. KLERUU alikuwa ni kiongozi machachari sana na ilikuwa kawaida kwake na alikuwa hana hiana kuwafokea hadharani watumishi wa umma wazembe.
Kwa hakika Dr. KLERUU alikuwa mbabe sana. Akiwa Iringa kuna wakati gari yake ilipigwa "overtake" na gari hilo lililompiga"-overtake" likamziba kwa mbele. Kufumba na kufumbua Dr. KLERUU alishuka kama komandoo na kwenda kumuwasha vibao dreva wa gari hilo Dr. KLERUU mara kwa mara alipenda kuwafokea watu kwa kuwaambia "Hamnijui Mimi? Kawaulizeni watu wa Mtwara" na yeye hakuwa mtu wa kukaa ofisini kama viongozi wengi wa wakati huo bali alijumuika na wananchi na kufanya nao shughuli za maendeleo bega kwa bega ambapo ilikuwa ni kawaida kwake kushika jembe kwa masaa kadhaa bila kula.

[emoji117]Kipindi hicho kulikuwa na kampeni kubwa ya kuwafanya wananchi walime mashamba ya pamoja na hivyo wakulima waliokuwa na mashamba makubwa walinyang'anywa kitendo ambacho hakikuwapendeza Wanyalukolo waliokuwa matajiri wenye mashamba makubwa ya mahindi.
Dr. KLERUU alihamishiwa Iringa ili akatekeleze mpango huo wa serikali na alipofika tu akatangaza kwamba mashamba yote binafsi yanapaswa kuwa ya ujamaa kufikia Novemba 1971.

[emoji117]Bw. MWAMWINDI alihamia eneo la Mkungugu Isimani mwaka 1954 akitokea Iringa mjini alikokuwa dreva. Alianza kilimo kidogo kidogo hatimaye akawa na mashamba makubwa ya mahindi ya hekari takriban 160. Akawa analima mashamba yake kwa trekta katika eneo hilo ambalo awali lilikuwa ni pori. Kipindi hicho hakukuwa na sehemu Tanzania iliyokuwa ikizalisha mahindi mengi kama Isimani.

[emoji117]Jumamosi ya tarehe 24/12/1971
DR.KLERUU alitembelea mashamba mbalimbali maeneo ya Tarafani Igulu na Ndolela kuhamasisha kilimo cha pamoja. Kesho yake Jumapili ya tarehe 25/12/1971 Dr. KLERUU( ambaye hakuwa na Jumapili wala skukuu) aliendelea na shughuli hizo za kutembelea mashamba ya wakulima.

[emoji117]Muda wa saa 11 jioni Dr. KLERUU alifika kwenye shamba la MWAMWINDI na kumkuta akilima kwa trekta lake.
Pamoja nae kulikuwa na mtoto wake na watu wawili aliowaajiri
Bw. Joseph Kusava ambaye ni mkwe wake pamoja na wake zake waliokuwa wakishirikiana nae kulima siku hiyo.

Moja ya wake wake alisema[emoji116]
Dr. KLERUU alifika shambani hapo akiendesha gari lake binafsi aina ya rangi ya bluu na ubavuni ikiwa imeandikwa RC-Iringa.
Baada ya kushuka alimfuata moja kwa moja MWAMWINDI na kuanza kumuhoji maswali mengi kwanini hataki mashamba yake yawe ya ujamaa. Akamwambia "Unafanya nini hapo?"Shuka shenzi we". MWAMWINDI akamuuliza "kwanini unanitukana?" Dr. KLERUU akamjibu "Funga mdomo wako, n'ge n'ge n'ge nini? Kwanini nawaambia hamsikii? Blood fool" Dr. KLERUU aliyekuwa na kawaida ya kutembea na kifimbo kidogo akakitumia kumchomachoma nacho MWAMWINDI.

[emoji117]MWAMWINDI akafura sana hivyo akaanza kwenda ndani kupitia eneo la makaburi ya baba yake na ndugu wengine huku Dr. KLERUU akimfuata na alipoyaona makaburi akasema "Tazama unaendelea kujenga nyumba za kudumu" MWAMWINDI akamjibu "Hizi sio nyumba ni mahali ninapozika ndugu zangu". Dr. KLERUU akajibu "Ni mahali unapozikia mirija wenzio mbwa we!".

Mnyalukolo MWAMWINDI akawaamehamaki sana. Akasema akaingia ndani akachukua gobore akatoka nalo nje na kumfyatulia risasi Dr. KLERUU ambaye alianguka na kufariki hapohapo MWAMWINDI aliuchukua mwili wake akauweka kwenye buti ya gari ya Mkuu huyo wa Mkoa akachukua na kofia ya Pama ya Mkuu wa Mkoa akaivaa yeye na kuanza safari ya kilometa 40 kwenda Iringa mjini.

[emoji117]Mjini Iringa watu walishangaa kuona gari ya Mkuu wa mkoa inapita upande wa kulia kwa vile mtaa wa Jamatini ulikuwa ni "One way" lakini wakahisi huenda Mkuu wa mkoa ana dharura. Saa 1 jioni MWAMWINDI akafika kituo kikuu cha polisi akaenda moja kwa moja kaunta akamkuta PC MBETA KASONDA na kukwambia "Ebu nenda kwenye buti ukaitoe mbwa yenu nimeishaiua" na kumkabidhi bunduki pamoja na funguo za gari. PC KASONDA hakuamini macho yake alipouona mwili wa Dr. KLERUU ukiwa umetapakaa damu. Dr. KLERUU alikuwa amevaa ovaroli nyeusi na miwani. Hivyo mara moja PC KASONDA akamuweka MWAMWINDI chini ya ulinzi. Mtu mwingine aliyekuwepo kituoni hapo ni mzee DAVID BUTITINI(ambaye alikuwa askari polisi na baadaye kada wa CCM Iringa). Tarumbeta likapulizwa na askari wakakusanyika na kupewa rasmi taarifa ya kifo hicho cha Mkuu wao wa mkoa na gari lake likahifadhiwa nyuma ya kituo cha polisi. Askari wanne wakaenda kuleta kitanda cha magurudumu toka hospitali na hatimaye mwili wa Dr. KLERUU ukapelekwa "mortuary" Kesho yake siku ya jumatatu mji mzima wa Iringa uligubikwa na simanzi kubwa.

[emoji117]Kuna kundi la watu ambao walikuwa wakimchukia sana Dr. KLERUU kutokana na aina ya uongozi wake hivyo lilipopata tu taarifa za kifo chake wakanunua makreti ya bia usiku huohuo na kuanza kunywa kwa kushangilia hadharani Msako ulipoanza usiku huohuo jamaa hao walikuwa wa kwanza kukamatwa[emoji16]

[emoji117]Mzee BUTININI ambaye pia alikuwa Mtwara wakati DR. KLERUU alipokuwa Mkuu wa Mkoa anakiri kuwa ni kweli DR. KLERUU alikuwa mtu wa shoka
"Ni kweli hata kule Mtwara alionekana mtemi sana mwenye kuhimiza mambo kwa nguvu. Lakini lazma muelewe maeneo ya Mtwara yalikuwa ya vita na tulikuwa tukiwasaidia ndugu zetu wa Frelimo hivyo kule kulihitaji mtu kama DR. KLERUU Mtwara DR. KLERUU hakukumbana na upinzani ila Iringa hali ilikuwa tofauti Kwa mawazo yangu Dr. KLERUU alipaswa kwanza kujifunza juu ya mila na desturi za watu wa Iringa Maana watu wa Iringa ni watu wa Iringa tu."

[emoji117]Mauaji hayo ya Dr. KLERUU yalimsikitisha sana Mwalimu NYERERE wakuu wa mikoa na wananchi mbalimbambali Lilikuwa ni tukio lililoongelewa nchi nzima Majirani na wazee wengi waliokuwa wakilima pamoja na MWAMWINDI walisombwa na vyombo cha usalama na kumwekea ndani kuisaidia polisi ambapo walikuwa wakikamatwa na kusafirishwa usiku kwa ndege za jeshi. Takribani watu 30 walikamatwa wakiwemo wazee maarufu kama IBRAHIM KHALILI, PESAMBIL MURSALI na wengineo na kupelekwa sehemu mbalimbali za nchi mfano Shinyanga, Mwanza na Zanzibar. Cha kusikitisha ni kwamba ndugu zao hawakujua wamepelekwa wapi Aidha nyumbani kwa MWAMWINDI huko Mkungugu kukawa kunalindwa na askari wa FFU muda wote.

[emoji117]Kitendo cha kukamatwa majirani na marafiki wa MWAMWINDI kilileta uhasama mkubwa baina ya ndugu wa majirani hao na familia ya MWAMWINDI.
Ikabidi mwanae AMANI MWAMWINDI (21) alazimike kutafuta kibali cha DC Iringa kwenda gereza la Dodoma alikokuwa anashikiliwa MWAMWINDI. Alipoganikiwa kukipata alikwenda na akamueleza hali hiyo ambayo ilimsikitisha sana Mzee MWAMWINDI.
AMANI akamshauri baba yake aandike barua kwa Rais NYERERE nae akafanya hivyo siku hiyohiyo. Katika barua hiyo MWAMWINDI alimueleza Mwalimu kwamba yeye ndiye aliyemuua Dr. KLERUU hivyo wengine hawahusiki hivyo waachiwe Baada ya kupita siku kadhaa wazee hao majirani wakaachiwa na kurejea kijijini hapo Isimani. Hata hivyo tafrani hiyo iliyokuwa imewakumba ikafanya wengi wahame eneo hilo kwani waliishaona "togwa limeingia nzi"[emoji16]
Upelelezi wa mauaji hayo ulienda haraka na MWAMWINDI akafunguliwa kesi ya mauaji ya kukusudia Mahakama kuu.

[emoji117]Kesi ilipoanza kusikilizwa ilivuta hisia za watu wengi na umati wa watu uliokuwa ukitamalaki kila siku mahakamani ulikuwa si wa nchi hii
Tarehe 2/10/1972 baada ya mashahidi wa pande zote kutoa ushahidi wao akiwemo RPC wa Iringa (Abubakar Hassan) aliyetoa ushahidi upande wa MWAMWINDI kwamba hakuwa na taarifa kwamba Mkuu huyo wa Mkoa angetembelea eneo hilo ndio maana hakumpa "Police escort"

[emoji117]Jaji GABRIEL CHIKE ONYIUKE toka Nigeria alimtia MWAMWINDI hatiani na kumuhukumu kunyongwa hadi afe. Hii ilikuwa ni baada ya kuukataa utetezi wake kwamba alitenda kosa hilo baada ya kurukwa na akili na pia alikasirishwa na marehemu Mh. Jaji aliona kwamba ingawa ni kweli MNYALUKOLO wa kawaida huwa si mtu wa mchezo[emoji16] mchezo anapodhihakiwa hasa mbele za wake zake lakini kitendo cha MWAMWINDI cha kwenda ndani kufuata bunduki kilionesha pasina shaka kwamba aliua kwa kudhamiria.

[emoji117]Adhabu hiyo ya kifo ilitekelezwa mara moja kwani Mwalimu NYERERE alisaini hati ya kifo cha MWAMWINDI
hiyo ilikuwa ni moja ya hati tatu za vifo zilizosainiwa na Mwalimu NYERERE kuidhinisha kunyongwa kwa binadamu katika uongozi wake wa miaka 24 katika taifa hili.
Kesi hii ilikuwa ya aina yake na haikuchukua hata mwaka mmoja toka tukio kutokea na adhabu kutolewa tofauti na kesi nyingine za mauaji ambazo kwa kawaida huchukua miaka mingi kabla ya hukumu kutolewa Kesi hii ilichukua miezi kumi tu[emoji848]

REST IN PEACE
1. Dr. W. KLERUU
2. S. A. MWAMWINDI

#MzeeWaVituAdimu [emoji134]
FB_IMG_1592895353740.jpg
 
#MzeeWaVituAdimu [emoji134]View attachment 1486632
kuna watu ukishawavuruga basi tegemea balaa zito...
 
JF imekuwa ni mahali pa kupashana habari na kuweza pia kuzungumzia mambo ya historia yetu na mwelekeo wa nchi.

Kuna Huyu bwana anajulikana kama marehemu Dr Kleruu, mie nimekuwa nikimsikia katika wimbo wa Mbaraka Mwinshehe kuwa alikuwa mwanamapinduzi.

Je, kuna yeyote anaweza kutupatia taarifa kumhususu huyu Dr Kleruu alikuwa nani hasa na uana mapainduzi wake ulikuwa vipi katika historia na siasa za Tanzania?

Mnara wa kumbukumbu kifo cha Dr. Kleruu kijijini Isimani

Mtoto wa Said Mwamwindi

=== Historia ya Dr. Kleruu kwa ufupi ===

HISTORIA: MKULIMA ALIYEMUUA MKUU WA MKOA SIKU YA KRISMASI-

ILIKUWA siku ya Sikuku ya Noeli almaarufu Christmas mnamo mwaka 1971. Mkuu mpya wa Mkoa wa Iringa aliyehamishiwa hapo akitokea Mtwara, Dkt. Wilbert Kleruu, msomi wa Shahada ya Uzamivu (PhD) wa Uchumi wa kijamaa katika Kilimo aliuawa na Mkulima aitwaye Said Mwamwindi.

Kipindi hicho kulikuwa na kampeni ya kutaifisha mashamba ya wakulima wakubwa na kuyafanya mashamba ya kijiji. Na Dkt. Kleruu alipelekwa Iringa ili akatekeleze kazi hiyo kwani kipindi hicho Iringa ilikuwa na wafanyabiashara wakubwa waliomiliki mashamba makubwa ya Kilimo hasa maeneo ya Isimani.

Katika eneo hilo la Isimani kulikuwa na mkulima mmoja aliyekuwa anamiliki takribani hekari 400 za mashamba na mfanyabiashara aliyekuwa anamiliki majumba Iringa mjini - Said Mwamwindi-
Kwa wakati ule ilishauriwa angalau kila mtu awe na shamba lisilo zidi hekari 4. Jambo ambalo lilileta mvutano mkubwa kati ya wakulima wakubwa na Serikali.

Sasa siku hiyo ya Christmas, Dkt. Kleruu alikwenda Isimani akiwa katika utekelezaji wa sera ya kutaifisha mashamba. Moja kwa moja alikwenda hadi shambani kwa Mwamwindi, na kumkuta analima.

Mkuu huyo wa Mkoa akamuuliza mbona unalima shamba lako mwenyewe na si la kijiji? Mwamwindi akajibu, sioni tatizo hakuna mtu shambani, leo ni Jumapli tena ni sikukuu.

Maneno yale yalimuudhi Dkt. Kleruu, ambaye alikuwa akisifika kwa ukali, kutekeleza sera za serikali na maneno makali au kutukana watu hadharani pale wanapo fanya makosa.

Dkt. Kleruu baada ya kuudhika alimtukana Mwamwindi tusi lililomlenga mama yake ambaye tayari alikuwa marehemu. Mwamwindi alihoji inakuwaje anamtukania mama yake, huku akimuonyesha kaburi alimozikwa?

Mkuu wa Mkoa, aliendelea kuja juu, huku akisema kaburi ndio nini? Huku akilipiga mateke kaburi la Mama yake Mwamwindi. Kwa kabila la wahehe makaburi yana heshima yake, kwani ndipo nyakati nyingine hutumika katika sala, matambiko na mila kadha.

Kitendo kile kilimghadhabisha Mwamwind, na kuanza kukimbia kuelekea nyumbani. Mkuu wa Mkoa akadhani Mwamwindi anamkimbia, akaamua kumfuata.

Alipofika nyumbani, tayari Mwamwindi alisha ingia ndani na kuchukua bunduki yake, Dkt. Kleruu baada ya kuona hali ile mara moja alianza kumuomba msamaha, lakini hasira zilimuwaka Mwamwindi kama moto wa nyika; hakuwa na msamaha, alimfyetulia risasi kichwani Dkt. Kleruu na kumuua.

Baada ya kumuua, Mwamwindi aliuchukua mwili ya Mkuu wa Mkoa na kuuweka ndani ya gari (inadaiwa kwenye boneti) alilokuja nalo Mkuu huyo wa Mkoa.

Kisha alichukua kofia ya Dkt. Kleruu na kuivaa, akaingia ndani ya gari na kuanza safari ya kuelekea Iringa mjini tena akipita njia isiyo ruhusiwa kwani barabara ilikuwa 'one way'.

Alipo karibia mjini, askari walishangaa ni nani anaye pita njia isiyo ruhusiwa, ila mara waligundua ilikuwa gari ya RC wa Iringa, hivyo walidhani amepata dharura.

Gari lilipowasili kituoni, Polisi walijiandaa kupiga salute, mara alishuka Mwamwindi akiwa na bunduki yake na kuelekea ndani (counter). Askari walipigwa na butwaa.

Alipofika aliwaambia "Nendeni mkachukue Nguruwe wenu ndani ya gari," na Kisha akakabidhi bunduki yake.

Lilikuwa tukio la kustaajabisha, na kushangaza na lililofanyika kwa haraka sana.

Baada ya taarifa kuenea, msako wa polisi ulianza mara moja. Ila katika msako huo, Polisi waliwakamata baadhi ya watu walio kuwa wakinywa bia kwa furaha, shangwe na nderemo baada ya kusikia Dkt. Kleruu ameuawa. Kwani wanadai alikuwa na dharau.

Kesi ya Mwamwindi alipelekwa haraka sana na ndani ya miezi kadhaa, Juni 1972, Mwamwindi alihukumiwa kunyongwa hadi kufa, ikiwa ni moja ya hukumu chache za kunyongwa zilizo wahi kuidhinishwa.

Inadaiwa Mwalimu. Nyerere alihuzunishwa sana na kifo hicho, na hata kesi ya Said Mwamwindi ilipoisha na kupewa hukumu ya kifo, Inasemekana Nyerere hakusita kusaini, na ni mojawapo ya hukumu tatu tu za kifo zilizotekelezwa wakati wa utawala wa Nyerere

MICHANGO YA WADAU:

-----------------------------

Habari nyingine inayohusiana na habari hii fuatilia - Binti wa Dkt. Wilbert Kleruu atoa ya moyoni
Aise we jamaa, jana nilikua iringa maeneo ya isimani, nimefanikiwa kukutana na babu yangu mdogo ambaye yeye na wazazi wake pamoja na nduguze walikua ni wenyeji wa huko, kwa wakati huo babu alikua mgambo wa kijiji akiwa ni kijana aliyetoka tu, kumaliza mafunzo jeshini, alinipa historia ya dr kleruu na mwamwindi, kama ulivosimulia na nimoja kati ya watu wachache waliomwona dr kleruu anavoenda Isimani na anavorudishi akiwa mauti, kwani babu alikua anatoka iringa mjini kupeleka mayai na kuku kuuza kama ilivokua utaratibu wake kila siku ya jumapili na sikukuu, kwa mujibu wa babu mdogo ambae pia alikua katibu wa kijiji aliyeteuliwa na kleruu alipofanya mkutano wa hadhara, kleruu alikua ni moja ya viongozi wachapakazi sana, hasa kwenye sera ya utaifishaji ila shida yake alikuwa na dharau kubwa kiasi kwamba, alikuwa hatembei hata ulinzi wala backup yeyote akienda kutaifisha mashamba ya watu.kwa asilimia kubwa historia yako kifo cha kleruu ineshabihiana sana na ile aliyoitoa babu yangu
 
Mkuu
Habari Hii Ipo Jamiiforums.com Miaka Mingi Sana
Ukileta Kama Vile Mpya Siyo Sawa
Mods Iunganisheni Kwenye Thread Kongwe Humu
 
Back
Top Bottom