William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,400
Jamaa kukuzaba kibao mbele ya watoto wako na mke ni dharau kubwa mno.Usipotetea haki yako wakati huo basi wewe hata ukiishi miaka elfu hapa duniani huna faida yoyote. Kuna mambo mengine hayakubaliki kabisa.
I know one thing, ni kwamba Wahehe walimlilia sana Chief wao Adam Sapi, afanye kila awezalo kumuokoa Mwamwindi, asinyongwe. Sapi alijaribu kila njia kumuokoa Mwamwindi kwa kumbembeleza sana Mwalimu na Kawawa, lakini Mwalimu aliweka mguu chini. Infact yeye Sapi na Mwakawago, waliishia kwua wanasiasa very unpopular huko Iringa kwa sababu ya kushindwa kumuokoa Mwamwindi,
Chief Sapi, aliacha kabisa kwenda Iringa, na Mwakawago alishia hata kutokujenga nyumba kabisa huko Iringa, na hata ule ubunge aliokuwa akiupata ilikuwa ni kwa sababu ya kumuoa dada wa Sapi, ambapo Sapi alipofarikit tu ukawa mwisho wake wa ubunge na uwaziri.
Kwa maneno yake mwenyewe Mwalimu, kitendo cha kusaini kifo cha Mwamwindi, kilikuwa kikimtesa sana Mwalimu, aliyekua akitembea na Biblia kila mahali akimuomba Mungu amsamehe, kwa sababu ndiye aliyekwua the only mwananchi aliyenyongwa kwa saini yake.
Ahsante Wakuu.