Dkt. Wilbert Kleruu - Utata wa kifo chake, historia na maisha yake

Dkt. Wilbert Kleruu - Utata wa kifo chake, historia na maisha yake

Anfaal,

Mimi kipindi hicho nilikua na miaka kumi! tumemaliza tu kusherehekea miaka kumi ya uhuru kwa michezo halaiki,
shule zetu, Kisarawe (siku hizi dar sec), Lumumba, Gerezani na Uhuru Girls tulicheza Gobogobo, it was nice!

hii issue ilitikisa nchi sana na kabla haija poa ikaingia ile soo ya Karume ndio ikawa noma kabisaa!

Ushauri wangu japo hautapendeza ni kwamba wewe kwa kuwa kwa kiasi fulani mko karibu na Bwana Mwamwindi kuhusiana na issue hii, mshirikiane muandike kitabu! kama kikiandikwa vizuri kama hiyo simulizi yako, kitauzika mpaka mtashangaa! na mapato yataenda kwa familia ya marehemu. on the other hand its one of the classic stories of our country ikihusisha vijiji vya ujamaa kama one of the strategies of the young Tanzania just ten years after uhuru hivyo inawapa uwanja mpana zaidi wa mambo ya kuandika ila issue ya Mwamwindi iwe the leeding one.

Ni ushauri tu. best wishes.
 
huyu mzee Mwamwindi ni ndio mwanamme pekeyake na shujaa katika tanzania wala hatatokea tena mwaname kama huyu mpaka kiyama kitasimama
 
Nafikir Majid amefanya mahojiano na mtoto wa marehemu(jambo zuri sana)...lakn Aman kama mtoto wa marehemu kuna vitu anaweza kuviweka kooni kama heshma kwa Mzee...nlipata kukutana na Mzee Mwambugi(rafik mkubwa wa Mwamwindi)mkaz wa Nyang'oro...ni mzee sana,alinisimulia meng sana mana yeye ndo mtu wa tatu ktk wale "wanted"..kilichomsaidia yeye alikuwa na urafiki na Siyovelwa(aliyekuja kuwa mkuu wa Usalama wa Taifa?)...ninayo mahojiano yake ktk Audio

Pls yachape na kisha utu PM..
 
Dah, nimemsoma Mjengwa hadi mwili unanisisimka. Mzee Mwamwindi was a cold blooded killer - damn... yaani unaua mtu kisha unavaa kofia yake, nguvu ya hata kuendesha gari lake ukipita nyumba hadi nyumba na maiti ukisalimia watu..
 
Mkandara said:

Mkandara,

..thanks.

..i was thinking the same thing na nilikuwa nashangaa kwanini niko peke yangu ktk fikra hizo. kumbe na wewe umeliona hilo.

..kama siyo cold blooded killer basi huenda Mwamwindi alikuwa na matatizo fulani ya akili. huenda hata hakustahili hukumu ya kunyongwa.

..sielewi kwanini alikuwa akimanga-manga na maiti ndani ya buti la gari ya marehemu, huku amevaa kofia ya marehemu, kwenda "kusalimia" hao ndugu zake.

..kitu kimoja ambacho Mjengwa angetusaidia wasomaji wake ni kama angewahoji hao ndugu ambao Mwamwindi aliwatembelea mara baada ya kumuua Dr.Kleruu huku akiwa na maiti ndani ya buti la gari.

Hii ni sehemu ya tano ya simulizi. Pichani ni kijijini Isimani. Nje ya nyumba ya marehemu Said Mwamwindi. Pamejengwa kumbukumbu ya kifo cha Dr. Kleruu.

UKIMWONA kwenye mitaa ya Iringa bado anatembea kwa hatua za kijeshi. Ni Mzee David Butinini. Alipata kuwa askari polisi na alishuhudia kwa macho yake, siku Mkulima Said Mwamwindi alipofika kituo cha Polisi Iringa akiwa na mwili wa marehemu Dk. Kleruu kwenye gari aliloendesha.

Dk. Kleruu alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa aliyeuawa na Mwamwindi kwa kupigwa risasi. Mzee David Butinini alikuwa pia mmoja wa mashahidi kwenye kesi ya mauaji iliyomkabili marehemu Mwamwindi.

Mzee David Butinini ni rafiki yangu wa muda mrefu. Jioni ya Jumapili moja tunakutana Soko Kuu Iringa. Namuuliza juu ya kumbukumbu zake ya kilichotokea miaka 40 iliyopita.
Tunazungumza huku kwa pamoja tukikiangalia kituo cha polisi kilicho mbele yetu na ambapo Mzee David Butinini alifanya kazi kama Polisi miaka 40 iliyopita.

“Unasikia Maggid, nilishuhudia kwa macho yangu. Nilikuwa bado kijana enzi hizo. Nilikuwa mwanamichezo pia. Nilikuwa kwenye kikosi cha polisi cha mpira wa miguu. Nakumbuka ilikuwa jioni ya Jumapili ya Krismasi . Ni kwenye saa kumi na moja hivi.
Tulikuwa kama askari watatu hivi tumevalia kiraia na tulisimama pale nje ya kituo,” Mzee David ananieleza huku akionionyesha kwa mkono mahali hapo.

Kelele za makuli wabeba mizigo sokoni zinatufanya mimi na Mzee Butinini tusisikilazane vema. Wote, kutokana na utamu wa simulizi hii tunajikuta tunasogea mbele kidogo na kusimama kando ya kibanda cha rafiki yangu Mwarami. Kijana anayeuza matunda Soko Kuu la Iringa.
“Unajua Maggid,.... Soma zaidi; Raia Mwema | Kwa nini mkulima Mwamwindi alimpiga risasi RC Dk. Kleruu? V
 
Mjengwa, story ni ndeefu sana, can you tellen in a single sentes why mwamwindi my hero killed kleruu? Then Haya mengine weka kitabu, story inaboa
 
Mjengwa, story ni ndeefu sana, can you tellen in a single sentes why mwamwindi my hero killed kleruu? Then Haya mengine weka kitabu, story inaboa

Busar,
Asante sana kwa maoni yako. Lakini mbona unaumia hivyo. Una uchaguzi. Si kila kitu kinachoingizwa humu unalazimishwa kukisoma. Kama stori ya Mwamwindi inakuboa ndivyo unavyojisikia wewe. Una haki na feelings zako. Kuna wengine wanajisikia hamu ya kusoma mwendelezo wa simulizi hii. Nao wana haki ya kuwa na feelings hizo. Tusiwe wabinafsi sana, hata kwenye feelings.
Maggid,
Iringa
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
 
majid hii stori nzuri lakini unaipunguza radha kwa kuifanya a never ending story,mara ukikatishe mara ghafla unaianzisha wengine hata hatujui ilianza tena lini,mimi kwa mfano mara ya mwisho kuisoma kule kwako iliishia pale ukifanaya mahojiano na mwammwindi mdogo yule ealikua meya wa iringa,ukaikata imepita muda juzi nasema ngoja nisome gazeti la raia mwema mtandaoni naiona,lakini sio pale ulipoishia ukiwa na mtoto wa mwamwindi,this time nakuona uko na mzee Butinini amabae nahisi ni babake mwanandinga wa Reli zamani Duncun Butinini na dada zake wacheza netiball wale kina Jane Butinini..sasa ukawa umeshanipoteza kabisa kimtitiririko wa hadithi,ndio tukakushauri basi bora uandike kitabu tuisome kwa pamoja yaishe
 
Romantic,
Asante kwa mchango wako. Nakuelewa kuwa huu mfululizo wa simulizi hii unakuchanganya. Kwenye Raia Mwema unakwenda vizuri. Lakini hapa JF nadhani kuna utaratibu mwingine. Hii post unayoisoma sasa huenda ikahamishiwa kwenye thread nyingine ya Mwamwindi. Na hapo huenda ndio huwa mwanzo wa kukosa track yake. Hilo liko nje ya uwezo wangu.
Maggid
 
Tupe links ya kuanzia part 1 hadi mwisho wa hiki kisa, kwa sababu kama alivyosema Romantic hakieleweki, kina kwenda mbele na kurudi nyuma

Wewe tuwekee links za kisa kizima kwenye post moja kisha sisi tutaenda kuisoma huko
 
waambie moderator wa i sticky hii thread yako na waziunganishe zote..tupo wengi tunafuatilia hii stori ni tamu sana ..
 
Busar,
Asante sana kwa maoni yako. Lakini mbona unaumia hivyo. Una uchaguzi. Si kila kitu kinachoingizwa humu unalazimishwa kukisoma. Kama stori ya Mwamwindi inakuboa ndivyo unavyojisikia wewe. Una haki na feelings zako. Kuna wengine wanajisikia hamu ya kusoma mwendelezo wa simulizi hii. Nao wana haki ya kuwa na feelings hizo. Tusiwe wabinafsi sana, hata kwenye feelings.
Maggid,
Iringa
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo

Mjengwa, Asante kwa hoja yako Lakini c kamilifu, nimekushauri narration iweke katika kitabu hapa weka snopsys. Ili mfuatiliaji wa thread ajue kisa, hii ni ushauri. Pia Kama utaweka katika kitabu nadhani utaifanya kazi upya ili kuitia radha tofauti na hii manuscript. Mi nimeifuatilia katika raia mwema pia. Chakula kizuri kisifiwe na walaji pia, ukisifu mpishi tuuu..a nadhani SIP sawa. Tazama naa maoni mengine
 
Ukweli nikwamba Kleruu alikua anatembea na mke wa Mwamwindi...na alimfwata shambani kumwoneshea dhalau. Na ktk maneno yaliyoamsha jazba hadi kupigwa risasi, kleruu aligusia uhusiano wake na mke wa Mwamwindi mbele ake. Na moja ya kosa kubwa ambalo Nyerere alifanya ni kusaini hati ya kifo ya mahakama!
 
naungana na wengine hapo juu. tunahamu sana na hii story ila the way inavyotufikia ndo hatuna hamu nayo. ningefurahi kama ma mods wangeiweka kama kile kisa cha Mohamedi Said ya wapigania uhuru wa Tanganyika wa ukweli walioachwa kwa makusudi. hiyo ingetusaidia sana mkuu Maggid.
 
Je kwenye blog yako unapatikana mfululizo wote wa habari nlisoma kidogo kwenye gazeti.
 
Katika mazungumzo yangu na wazee wa kihehe wakanambia kuwa kumbe yule maalufu Mzee Mwamwindi.Mzee huyu aliyeacha historia kwa kumfanyia ukatili mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Kireluu alinyongwa baada ya kukutwa na hatia ya mauaji hayo. Mzee huyu ambaye anaonekana kama alikuwa mpinzani wa siasa ya ujamaa na kujitegemea pia anaonekana kama mtu mwenye msimamo mkali kupinga unyanyasaji wa watu wenye mamlaka. Mgongano huu wa mawazo unatokana na hadithi za kutatanisha kuhusu mauaji hayo hasa mazingira ya tukio, siku tukio lilipotokea na kauli zilizotolewa na mashahidi wa pande zote mbili. Je huyu mzee katika mila ahesabike kama shujaa au kama mhaini na mpinga maendeleo? I stand to be collected
 
mnaokumbuka vijiji vya ujamaa vilipoanzishwa kuna utelekelezwaji wake ulikuwa na mapungufu pale walipotaka kumuamisha mkuluma mkubwa sana mwamwindi na kumtaka ahamie eneo lingine wakati alikuwa analisha iringa .kilichotokea ni kwa mwamwindi kumchapa risasi mkuu wa mkoa dr kreluu sasa kwa mabavu ya serikali dhaifu ya kumteka na kumuumiza dr ulimboka serikali yote itegemee lolote kuanzia sasa yaliyotokea iringa itakuwa fundisho kwa uongozi wetu maana hakuna aliyepata mkasa so far
 
Back
Top Bottom