Dkt. Wilbroad Slaa: Viongozi wakubwa serikalini na CCM wapatao 38 wamenipigia kuniunga mkono katika kupinga uuzwaji wa bandari za Tanganyika

Ndio imetoka hiyo kaka. Sisi tunataka kazi na Samia aliahidi kutoa ajira, hatukukubaliana atazitafuta vipi. Ila kwa mtazamo wangu, yeye apige, galagaza lakini sisi tunachoangalia ni ajira. Mtaani kunachosha.
Dr Slaa ni mnafiki, sikumuona kulalamikia mkataba wa Nyerere na waingereza kuhusu uuzwaji wa Almasi. Hivi amewahi kuuona mkataba huo, au ni kwa sababu saint mwenzake? Au huu ndio mkataba wa kwanza.
 
Safi sana mtanganyika Dr. Slaa...ila msipange mipango yenu kupitia simu hawachelewi kuwadukua
Huyu Slaa anaumwa Demens wala hakumbuki anachofsema. Wenye tabu na kuja kuumbuka ni hao wajinga wanaompigia simu wakidhani Slaa atafanya siri.
Huyu Padre anazeeka vibaya!
 
Hahahahahaha


Hivi unaijuwa nguvu ya Rais wa Tanzania au unaisikia tu?

Kama huijuwi ngoja nikufahamishe, kuna mtu aliwahi kunifahamisha, kwanza sikumuelewa lakini baada ya kufikiri nikamuelewa:

"Rais wa Tanzania ana nguvu ndani ya Tanzania kuliko Rais wa Marekani ndani ya Marekani".
 
Wanaopinga huko kwenye corridor zao unafikiri hawajulikani?
Pascal naye anakuwa kama mgeni wa mambo haya, walio piga simu wanajua kabisa simu za Dr Slaa zinafuatiliwa na hata Slaa anajua simu zake zinafuatiliwa. Hawawezi kuwa wazembe kama baadhi ya watu wanavyo dhani
 
Hatariiii !!
 
"Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM"- Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

"Mtaji wa Maskini ni Nguvu zake mwenyewe"-hayati Benjamin William Mkapa.
 
Tumuulize na wale wa NEC wamo?
 
hapana, siyo wanafiki , watapoteza kazi zao na ndizo zinawapa ugali wa watoto. Ni wachache kama akina Lisu and team waliokataa kuhongwa vyeo na magufuli ili wa defect chadema wakakataa
Kweli kabisa Lissu na wenzake waliweza kusurvive kwa magufuli hawatashindwa sasa.
 
Ninafurahi sana ninapolisikia neno "Watanganyika"
 
SLaa anajua kucheza na akili za Ccm itakuwa hakuna ukweli kuhusu hilo, ama ame exagerate tu kuendelea kuongeza sintofahamu... huyu mzee anajua kufanya hii kazi ya siasa vilivo..
 
Kama kweli wanakuunga mkono tuwaone hiyo cku ya hayo maandamano yako usidudanganye .
 
Shida ya huyu mzee nae ni kutokuwa na siri, mambo anayoambiwa chumbani anapeleka hadharani, atakosa kupewa siri ... anabwabwaja sana ...low IQ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…