Dkt. Wilbrod Slaa: Utekaji wote unaondelea nchini ni sheria ya idara ya Usalama wa Taifa ya mwaka 2024

Dkt. Wilbrod Slaa: Utekaji wote unaondelea nchini ni sheria ya idara ya Usalama wa Taifa ya mwaka 2024

Na hapa ndiyo inadhihirika kuwa huyu bibi ni shetani kabisa. Kuwa naye ni hasara kubwa kwa nchi na kwa kila mwanadamu.
 
Na hapa ndiyo inadhihirika kuwa huyu bibi ni shetani kabisa. Kuwa naye ni hasara kubwa kwa nchi na kwa kila mwanadamu.

Duh, mkuu unauwezo wa kujua nani ni shetani na nani sio shetani?

Safarini Khartoum Sudani.
 
Dkt Slaa amemshukia Samia kusaini sheria inayowapa Usalama wa Taifa Kinga bila kuzingatia madhara yake kwa umma katika utekelezaji wa sheria hiyo.

Ameyasema hayo kupitia jukwaa la Sauti ya Watanzania alipokuwa anazungumzia hali ya nchi kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Sikiliza video kwenye link upate undani wa alichokizungumza


View: https://youtu.be/LthDMIBnZEQ?si=rL6ng2HpU5-tmDCA

Kwani Father Dk. Slaa ameijua leo hiyo Sheria? Mbona ipo kitambo Sasa?
 
Na hapa ndiyo inadhihirika kuwa huyu bibi ni shetani kabisa. Kuwa naye ni hasara kubwa kwa nchi na kwa kila mwanadamu.
Ndiyo maana Makamu wa Rais na waziri mkuu wameamua kukaa pembeni mapema hawataki shida baadae
 
Dkt Slaa amemshukia Samia kusaini sheria inayowapa Usalama wa Taifa Kinga bila kuzingatia madhara yake kwa umma katika utekelezaji wa sheria hiyo.

Ameyasema hayo kupitia jukwaa la Sauti ya Watanzania alipokuwa anazungumzia hali ya nchi kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Sikiliza video kwenye link upate undani wa alichokizungumza


View: https://youtu.be/LthDMIBnZEQ?si=rL6ng2HpU5-tmDCA

Fvck CCM
 
Anaandika: Dr. Wilbrod Slaa

Msingi wa vitendo vyote vya utekaji unaoendelea nchini ni Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa (TIS) ya mwaka 2024. Bila kurekebisha sheria hii, Watanzania wataendelea kutekwa, kupotezwa na kudhulumiwa hadi tutoweke kabisa kama taifa huru.

Sheria hiyo imeipa TIS mamlaka makubwa ya kukamata watu, lakini bila kuweka utaratibu bayana wa:

(a) Wanapomkamata mtu, wampeleke wapi? Tofauti na Jeshi la Polisi lenye vituo maalumu vya kushikilia watuhumiwa, TIS haina vituo vinavyotambuliwa kisheria vya kuwapokea waliokamatwa.

(b) Hakuna mwongozo wa kisheria unaoeleza nini kifanyike baada ya mtu kukamatwa na TIS. Kwa mfano, Polisi wanapaswa kuhakikisha kuwa ndani ya saa 4 baada ya kumkamata mtu, maelezo (statement) ya mtuhumiwa yanakuwa yamechukuliwa, huku haki za mtuhumiwa zikiwa zimeainishwa wazi katika Sheria na katika taratibu za Police General Orders (PGO). Kwa upande wa TIS, sheria yao haina mwongozo wowote kuhusu haki za waliokamatwa wala hatua zinazofuata baada ya kukamatwa.

(c) Sheria ya TIS imeiruhusu Idara kutumia silaha nzito, pingu na vifaa vingine vya kiusalama, lakini tofauti na Polisi, hakuna mahali sheria inapotamka wazi kuhusu vifaa hivyo vinahifadhiwa wapi, vinatumiwa kwa utaratibu gani, na ni nani anawajibika kuvihifadhi.

Hayo ni baadhi tu ya mapungufu makubwa ya sheria hiyo. Kwa ujumla, sheria hii imeifanya TIS kuwa taasisi isiyoguswa, isiyodhibitiwa na isiyoajibika kwa namna yoyote kwa umma au kwa vyombo vingine vya dola.

Kwa hiyo, kama raia — hususan wasomi — tumeshiriki kimya kimya kuzalisha mazingira haya ya kinyume na utawala wa sheria kwa kukubali kupitishwa kwa sheria hii mbovu bila kupiga kelele. Sasa tunavuna tulichopanda.


My take: TLS Mwabukusi hamuwezi kuipinga hii sheria mahakamani kama Olengurumwa alivyopinga sheria ya kutoshitaki akina Rais na wenzake?

Hii Sheria Ilipokuwa inapitishwa watu walikuwa Busy na Mambo Mengine.TISS sasa hivi wanaweza kufanya Chochote,Popote na hakuna Yeyote anayeweza kuwafanya Lolote.Hata Rais Samia haweza kuwafanya Lolote.Kiufupi TISS ni kundi la Kigaidi dhidi ya Watanzania

Mabadiliko ya Sheria ya TISS yaliyofanyika Mwaka 2023 yameigeuza TISS kuwa Kundi la Kigaidi badala ya kuwa taasisi ya Usalama wa Taifa katika Nchi huru.
Mimi binafsi niliandika thread humu kwenye mtandao huu wa JF kutoa angalizo juu ya suala hili. Maoni yangu yamepuuzwa na hatimaye sasa hivi Nchi imekuwa Jehanamu.

Sasa ni mwendo wa kila Mtu atafute namna ya kuweza kuokoa nafsi yake, na hii ni hatari kubwa sana kupita kiasi kwa Usalama wa nchi.
 
Back
Top Bottom