Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Ameburuzwa kwenye Mahakama ya Mkoa wa Mwanza akikabiliwa na kosa moja la Ulawiti
Amepandishwa leo July 9 baada ya makelele mengi ya wadau kutaka haki itendeke
Bado haijajulikana kama ataswekwa Rumande au atapata dhamana.
====
Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Yahaya Nawanda, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza na kusomewa shitaka moja la kumwingilia kinyume na maumbile Tumsiime Ngemela (21) katika eneo la Rock City Mall jijini Mwanza.
Mshtakiwa huyo amefikishwa katika mahakama hiyo mapema leo Julai 9, 2024 na kusomewa shitaka hilo ambalo anadaiwa kulitenda Juni 2, 2024 katika eneo hilo kinyume na kifungu cha sheria cha 154 kifungu kidogo (a) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022
Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza, Erick Maley, Waendesha mashtaka wa kesi hiyo ambao ni Wakili wa serikali Magreth Mwaseba na Martha Mtiti waliitaja kesi hiyo kuwa ni kesi namba 1883 ya mwaka 2024.
Hatahivyo mshtakiwa alikana shtaka hilo na yuko nje ya dhamana baada ya kukamilisha masharti aliyokuwa amewekewa ambayo ni kuwa mtumishi wa serikali pamoja na bondi ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh 5 milioni.
Baada ya kukamilisha masharti hayo, Mshtakiwa yupo nje ya dhamana hadi Julai 16, 2024 ambapo kesi hiyo itaanza kusikilizwa kwa hoja za awali huku upande wa mlalamikaji ukitakiwa kwenda na mashahidi.
Pia soma

- Binti anayedaiwa kulawitiwa na aliyekuwa RC wa Simiyu: Kesi iende Mahakamani, RC alikuwa mpenzi wangu, walimpa mama Tsh. Milioni 3 ili wazime kesi
- MCL: Mkuu wa Mkoa adaiwa kumlawiti mwanafunzi wa SAUT
- Mkuu wa Mkoa Simiyu atenguliwa, Kenan Kihongosi achukua nafasi hiyo
- RC Said Mtanda wa Mwanza hastahili kuwa kiongozi wa umma kwa kutaka kuzima kesi ya Binti Tumsiime anayedai kulawitiwa na Dkt. Nawanda