Dna ya scouser

Dna ya scouser

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
England wana utamaduni wa aina yake ambao upo tofauti sana na nchi zingine, kuhusu utambulisho wa watu wao.

Kila watu wana utambulisho wao kutokana na maeneo wanayotoka. Kwa mfano, mtu wa kutoka Manchester huitwa Mancunian. Mtu wa kutoka Newcastle huitwa Geordie, na yule wa kutoka London huitwa Londoner.

Katika watu wote hao, hakuna anayejiona wazalendo kwa eneo lake kama mtu wa kutoka Liverpool, ambaye huitwa Scouser.

Huyu mtu humwambii kitu kuhusu Liverpool yake. Iwe Liverpool kama mji au Liverpool kama klabu.

Unamkumbuka yule dogo aliyerusha mpira haraka haraka kwa Trent Alexander-Arnold katika kona iliyozaa bao la nne la Liverpool dhidi ya Barcelona kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa? Basi ule ndo u-scoucer.

Yule dogo jina lake ni Oakley Cannonier, Scouser wa miaka 14 akiwa anapata mafunzo ya soka kutoka akademi ya Liverpool. Naye ni mzaliwa wa Liverpool,
Pichani ni bwana mdogo Trent Alexander-Arnold, mlinzi wa kulia wa Liverpool ambaye ni mzaliwa wa Liverpool yaani Scouser. Huyu ndiye aliyerushiwa mpira siku ile ili apige kona haraka haraka.

Mwaka 2014, dogo huyu akiwa na 14, naye alikuwa mmoja wa madogo waokota mipira dimbani Anfield, kama anavyoonekana kwenye picha ya chini kushoto kwenye duara jekundu.

Hii ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Chelsea, naye alifanya kama alivyofanya dogo Oakley dhidi ya Barcelona...aliokota mpira na kuurusha haraka haraka kwa Glen Johnson, lakini haikuwa riziki. Wakafungwa 2-0 huku Gerrard akiteleza mbele ya Demba Ba.

Na @Aaron
tapatalk_1569422496680.jpeg
 
Mimi nilibatizwa miaka 28 iliyopita na Mzungu Muingereza, aliyekuja kufanya huduma ya uchungaji kanisani kwetu kwa miaka 6.

Mimi nilipewa jina lake Mara tu baada ya kubatizwa naye.

Huyu Mzungu alitokea Liverpool na alikuwa anacheza mpira sana kwenye kiwanja cha kanisa letu.

Alikuja na mke wake nyumbani amekuwa Mzee mtu mzima, siku ya Alhamisi 2012, kisha familia nzima tukaenda ViaVia Arusha kuongea na kula pamoja.

Yeye anasema kwa uingereza neno LIVERPOOL ni kama DINI ipo rohoni kwa Watu. Wanapenda sana Football Club yao pamoja na jiji lao.

Yeye ndio alinifanya tangu utotoni nikawafahamu wanamuziki wa kundi la UB 40 wa Birmingham, na kila nikisikia Red red wine namkumbuka sana.

Alimuachiaga Mzee picha zake alizopiga na wanamuziki wa UB 40.…

Anamwongelea sana Daglish

UB 40, ni kundi linalokubalika na kuheshimika sana Liverpool.
 
Asante sana mkuu kwa kushare uzoefu na kumbukumbu nzuri ya kutukuka
 
Asante sana mkuu kwa kushare uzoefu na kumbukumbu nzuri ya kutukuka
Sawa Chief, ila nilitaka kukurekebisha kidogo.

Wakazi wa Liverpool ndio wenye jina hilo, ila Washabiki wazalendo haswaa...wale unaoona wanashangilia kuanzia dakika ya 1-90 na zaidi ni Kopites,

Wale washabiki walikuwa na umoja mpaka nao wameanzisha timu yao ya palepale Anfield.
 
Back
Top Bottom