Aaron Arsenal
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 24,501
- 28,711
England wana utamaduni wa aina yake ambao upo tofauti sana na nchi zingine, kuhusu utambulisho wa watu wao.
Kila watu wana utambulisho wao kutokana na maeneo wanayotoka. Kwa mfano, mtu wa kutoka Manchester huitwa Mancunian. Mtu wa kutoka Newcastle huitwa Geordie, na yule wa kutoka London huitwa Londoner.
Katika watu wote hao, hakuna anayejiona wazalendo kwa eneo lake kama mtu wa kutoka Liverpool, ambaye huitwa Scouser.
Huyu mtu humwambii kitu kuhusu Liverpool yake. Iwe Liverpool kama mji au Liverpool kama klabu.
Unamkumbuka yule dogo aliyerusha mpira haraka haraka kwa Trent Alexander-Arnold katika kona iliyozaa bao la nne la Liverpool dhidi ya Barcelona kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa? Basi ule ndo u-scoucer.
Yule dogo jina lake ni Oakley Cannonier, Scouser wa miaka 14 akiwa anapata mafunzo ya soka kutoka akademi ya Liverpool. Naye ni mzaliwa wa Liverpool,
Pichani ni bwana mdogo Trent Alexander-Arnold, mlinzi wa kulia wa Liverpool ambaye ni mzaliwa wa Liverpool yaani Scouser. Huyu ndiye aliyerushiwa mpira siku ile ili apige kona haraka haraka.
Mwaka 2014, dogo huyu akiwa na 14, naye alikuwa mmoja wa madogo waokota mipira dimbani Anfield, kama anavyoonekana kwenye picha ya chini kushoto kwenye duara jekundu.
Hii ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Chelsea, naye alifanya kama alivyofanya dogo Oakley dhidi ya Barcelona...aliokota mpira na kuurusha haraka haraka kwa Glen Johnson, lakini haikuwa riziki. Wakafungwa 2-0 huku Gerrard akiteleza mbele ya Demba Ba.
Na @Aaron