Asha nakubaliana na wewe kwenye mapenzi kuna wivu ila ukizidi ni balaa. Ninachotaka kutofautiana na ntaendelea kusimamia mtazamo wangu ni kuwa binadamu tuko selfish (by nature) mimi nina wivu haswa kwa mume wangu ila si always inategemea na situation kwani kwa kuwa nae muda mrefu nian mjua vizuri na nina more trust kwake than wivu; lakini sipendi yeye anionee wivu japo sitaweza ku mcontrol kwani yeye ni in charge wa feelings zake. Napenda kusema kuwa siwezi kupalilia wivu ila ntapalilia imani yake kwangu nadhani umenipata. Ila nafahamu kuna watu wana force kuonewa wivu thinking kuwa ni kipimo cha penzi. To me I want to be trusted but nina wivu kwake. Na nadhani hata yeye ana penda kuwa trusted ila ana wivu kwangu.
Nimeshashuhudia wadada wanatandikwa vibao na boyfriends (imagine just boyfriend) afu unasikia wanasema jamaa ana wivu kweli. Yani they enjoy being treated that way. That is why I say wivu my foot.
Mimi natafuta trust kwa hiari au hata kwa lazima nikiwa na maana kuwa sometimes na ignore comments na lawama zisizo na msingi na hiyo imenisaidia kuwa na uhuru wa kutosha kupanga mambo ya maendeleo bila kubughuziwa. Na kumjenga jamaa kunipa freedom ninayo deserve.
Ndio maana sielewi mtu anaponambia napenda kuonewa wivu; badala ya kusema napenda kupendwa. Wivu na kupenda vinaambatana mara nyingi lakini wivu si kupenda ni selfishness. Ukiwa less selfish na wivu hautakuwa tatizo kwako. Ndio maana watu wanaojuana vizuri na kuaminiana wanakuwa hawaoneani wivu wa kijinga na wakiwa na doubt jua si bure kuna ka ukweli.