Elections 2010 Do you know why not Dr Slaa 2010-2015?

Wakifanya kama Kenya kumuapisha haraka......na matokeo yatakuwa kama Kenya......Koffi Annan, Obasanjo n.k wajiandae!
Kama wana mawazo hayo naiona ICT The Hague kwa mbaliii. Ulimwengu huu umebadilika sana. Kama Shimbo na vijana wake(ambao nao wanajisahau kuwa nao ni watanzania ambao kesho na kesho kutwa watastahafu kazi zao na kurudi uraiani kwenye umasikini imara) wataamua kuwaua WaTZ wanaodai kuibiwa kura zao basi wajue ziko mahakama za kimataifa ambazo hazihongeki na watapelekwa tuu.
Wako wapi wakina Taylor? wakina El Bashir anaishi kama swala leo na Kenya kuna wanaosubiri yawafike nk.
Wawaache Watanzania wachague wenyewe nuru au giza. Wakiamua giza kwa utashi wao basi hilo ni lao wenyewe lakini sio kwa kuwaingiza gizani kwa nguvu. Romania na South Africa walikuwa na nguvu kubwa kijeshi lakini tawala hizo ziliangushwa na nguvu ya wananchi sisi hatuna sababu ya kufika huko kwa sababu wananchi wa kawaida ni ndugu kabisa ila itikadi tofauti. Baba Chadema,mama CCM, Mtoto CUF, shangazi NCCR, hapo kwa nini kuuana wenyewe kwa wenyewe kwa ajili ya maslahi ya watu wengine wachache?
WATANZANIA TULIKATAE HILI, tujiulize kwa nini tunafanya uchaguzi wakati yatokanayo na uchaguzi huo wakubwa(kama wanavyojiona wenyewe) hawataki kuyakubali na wanataka kupindisha maamuzi yetu kwa gharama yeyote?
 
Suala la kuiba kura halipo kwa sababu kila mmoja mawazo yake yako huko kwa hiyo kila mshika dau kwenye uchaguzi atataka kuhakikisha haki inatendeka.

Tatizo liliobaki ni vyama vya upinzani kuishinikiza NEC isizuie wapigakura kuwa mita 200 kutoka eneo la kupiga kura.

Wakifanikiwa hila JK na CCM yake wanaturudishia nchi yetu bila zengwe.
 
Jina la director wa uchaguzi Tanzania ni Mheshimwa Kiravu na aliyekuwa director wa uchaguzi Kenya wakati huo ni Mheshimiwa Kivuitu.
Haya majina yanaweza kuwa yanaashiria mambo mabaya kuhusu matokeo ya uchaguzi

Kama mwalimu kichuguu anaweka mbele myth kuliko facts on ground; basi myth kuwa upinzani utasababisha vita itaishi milele.
 
Mambo ya kichochezi siyo mazuri hata kidogo, sisi waAfrica tunalilia watu wenye sera endelevu na siyo vitisho kwamba tukishindwa tutapigana yaani kanakwamba watu wanajisikia kwamba amani ni boring. Kuhusu Chadema kushinda ni ndoto za alinacha kwasababu waTanzania siyo wajinga kumpa nchi mtu ambaye mda wote anaongelea jinsi atakavyo fundisha watu adabu tena kwa gadhabu kubwa, watu kama Jaji Mkuu, Polisi wanaomlinda kwenye mikutano yake ya hadhara, hadi wanajeshi wanaokwenda kwenye mikutano yake au wanajipitia tu alikuwa na anawatisha na kuwatukana kwamba atapeleka adabu huko makambini kwao. Pale jangwani siku ya ufunguzi wa kampeni za Chadema viongozi waandamizi wa Chadema walikuwa wanatukana kwa kufoka eti, dola yote imeoza kwasababu inalinda waliopo madarakani na mengine chungumzima bila kuwa na concrete evidence. Wanadai wakichukua nchi watafanya fagia fagia kwenye serikali yote..watasweka watu jela hawatakuwa na msamaria mtume kwa mtu yeyote yule na kutoa ahadi za kijingajinga. Eti kilakitu kitakuwa bure kuanzia wazee kupanda daladala, elimu, afya, na mambo chungumzima vyote bure...anadhani benki ya dunia, IMF, ADB vyote vitakuwa vinamwangalia tu, au akaulize waZimbabwe.
 

Hivi uandhani kuwa wapiga kura wakiruhusiwa kubaki katika eneo la kuhesabu kura ndio itasaida na kazi ya kuhesabu itafanyika kwa amani. Hivi hudhani kuwa kama mtu anaamua kuharibu uchaguzi hiyo ndiyo nafasi nzuri kumaliza mpango wake? Labda mwenzetu unaishi katika maeneo ya walala heri lakini huku kwetu usahilini ukiachia "wapiga kura" hata mita mia karibu na kituo unakaribisha vurugu. Na ziaid wahuni wa CCM huo ndio wakati muafaka wa kufanya mambo yao kiusanifu zaidi.
 
Ni kweli wanaweza kuiba kura, lakini mi nadhani tukipiga kura kwa wingi kwa Dr. Slaa itampa nafasi kubwa Dr. Slaa kushinda hata kama wataiba

Miwakala mingine ni rahisi kurubuniwa, kama huko kwenye vijiji vya akina King Unge ukimpiga jamaa na enyimba anatoka baru na kuachia wajipimie kiasi wanachotaka.
 

Nina wasiwasi, ni kweli kuwa unataka kujua strategies? Ili iweje? hujatumwa kweli wewe?
Mi nadhani ukapige kura tu, CHADEMA imejipanga and itatetea ushindi itakavyoweze, sisi wapiga kura tusiache kupiga kura, yasije yakawa ndio yale yale, (Tulijua, ndo maana hatukupiga kura........................)
 
wataweza kuiba pale tu kura za ccm na za chadema zitakapokuwa zimepishana kidogo....sasa watawezaje kuiba ikiwa chadema wana 75% na ccm 20% ya kura!???
 
Actually hata Kenya Kibaki alijaribu saana kuchakachua kura za Odinga at Majimbo level lakini akashindwa.... Kwahiyo wakaona, the only chance remaining ni kufanya lolote liwezekanalo wakati wa kujumlisha kura za majimbo yote...mbinu hiyo nayo ika-bounce. Ndipo wakaamua haraka haraka wakimbilie ikulu(Kibaki na Mwanasheria mkuu wa Kenya) ili matokeo yatangazwe upside down...mshindwa akawa mshindi hatimaye. Kilichotokea baada ya hapo ni historia na fundisho kwa nchi zingine duniani

Pendekezo langu kwa Dr. Slaa(kama kweli atashinda) lazima sasa yeye na Chadema waandae mtandao utakao-cover hizo risk areas tatu hapo juu. Kumbuka Odinga alifanikiwa kuzuia uchakachuaji katika hatua mbili za mwanzo(hatua ya majimbo na ile ya majumuisho ya kura za majimbo, lakini akaishia kuangukia pua kwa kushindwa kung'amua uchakachuaji wa level ya mwisho,yaani hatua ya kutangaza mshindi ndani ya ikulu kwa speed kubwa hata kama si mshindi halali). Endapo Dr. Slaa ataweka control za kutosha katika maeneo hayo huenda akashinda.

Ushauri mwingine kwa Dr. Slaa na CHADEMA unaendana na ule wa Mdau Mkuu Mwanakijiji. Yaani aanzishe utaratibu wa kukutana na kujadiliana na wadau mbalimbali(both in government and non government institutions) juu ya hatma ya nchi endapo atafanikiwa kuingia ikulu. Hii ni pamoja na kuwahakikishia kuwa maslahi yao (ikiwemo vyeo na nafasi zao kazini) yatalindwa(so long as yapo ndani ya sheria na taratibu za nchi). Hii itawapa imani kuwa hawatakuwa victims wa utawala wa Dr. Slaa na kwa njia hiyo wataanza kumuunga mkono(hata kimya kimya). Ikumbukwe kuwa moja ya vitu vilivyomgharimu sana Odinga ni viongozi wengi waandamizi serikalini walikuwa hawamuungi mkono ingawa jamii ya wakenya walio wengi inampenda mno(hata leo polls zinaonyesha Odinga ndio kipenzi cha wakenya)

Wakuu naomba kuwasilisha.
 
ni nadhani kuiba kura hapatasaidia sana kwani kila lenye mwanzo lina mwisho,udhulumati wa ccm umefika mwisho hata wafanye nini slaa atashinda tu
 
wakifanya kama kenya kumuapisha haraka......na matokeo yatakuwa kama kenya......koffi annan, obasanjo n.k wajiandae!

kenya yaliyotokea yanajulikana kwamba baada ya matokeo kutangazwa wakikuyu walifukuzwa na wengine kuuliwa ktk maeneo ya wajaluo na wakalenjin na vivyohivyo ndivyo walivyofanyiwa wao ktk maeneo ya wakikuyu!!!

sasa huku kwetu unamaana itakuwa ni wachaga dhidi ya nani? Maana wachaga wamehamia kila mkoa huko wana mabaa na maduka na kama ikitokea kama yale ya kenya mungu apishie mbali basi watakao athirika watakuwa wachagga ambao wengi wao ni chadema!!! Tunaomba tusifike hapo na uchaguzi wetu ufanyike kwa amani na atakaeshinda aapishwe na atakaeshindwa akubali kushindwa hii ndio demokrasia!!!

kama wapinzani walikubali kuingia ktk uchaguzi kwa kuikubali nec, hawana budi kukubali natija ya kura kwani kama walikuwa na shaka na tume kwanini wameingia ktk uchaguzi? Kama wanaamini ktk peoples power kwanini hawakulazimisha tume huru yenye wajumbe toka vyama mbalimbali?

uchochezi na vurugu haziwezi kusaidia bali zitatuletea shida zaidi ya hizi tulizonazo!!! Tuacheni tuishi kwa amani na wala hatutaki tanzania izae wakimbizi!!! Nchi zote zinazotuzunguka zina vita na migogoro!!! Sasa huku kwetu kukitokea machafuko tukimbilie wapi? Au chadema munatuahidi mahali salama pa kutupeleka pindi pakitokea machafuko? Mbona chadema kila siku munaongelea vita na uasi? Sera zenu ni kumwaga damu za wa tanzania? Hivi hamuoni raha mpaka muzungumzie kumwaga damu zetu? Kila siku matishio! Munatoa siku saba kwa maafisa wa jeshi, yaani yale ya lyatonga mrema miaka ya 90 ndio sasa zimekuwa sera zenu za vitisho!!!

nahakika mwalimu nyerere angefufuka leo na kuona vurugu na sera hizi za chadema lazima angesema (siwezi kuwaachia mambwa watawale nchi yangu)!!!

asiesikia la mkuu huvunjika guu!!!
 
Wandugu, ccm inajua sana kucheza na mawakala wa kuhesabu kura, sijui tutapata wakala gani labda malaika toka kwa sir God, lakini kama ni sisi ngulu mbili,mmmmmm!!, kabulungutu haka hapa udenda unakutoka. Na kibaya zaidi % kubwa ya wakala ni kashushushu wakutupwa na wako kwa ajili hiyo.
 
Watu wanaposema tuige wakenya wanamaanisha nini
 

Tarime walishindwa kufanya chochote kwa vile wapiga kura walikataa kuondoka vituoni
 
kenya yaliyotokea yanajulikana kwamba baada ya matokeo kutangazwa wakikuyu walifukuzwa na wengine kuuliwa ktk maeneo ya wajaluo na wakalenjin na vivyohivyo ndivyo walivyofanyiwa wao ktk maeneo ya wakikuyu!!!
[/size]

Crap
 

Bwa ha haha,
Omar bana, eti anamlinganisha Mbowe na Rostam
Unafiki na uzandiki wa kiwango cha juu kabisa toka kwa consultant wetu.
 
Aongee na nani kabla hajachaguliwa?Aongee na Mwanakijiji na wenzake kwa ushauri labda!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…