Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,455
- 73,145
Kama wana mawazo hayo naiona ICT The Hague kwa mbaliii. Ulimwengu huu umebadilika sana. Kama Shimbo na vijana wake(ambao nao wanajisahau kuwa nao ni watanzania ambao kesho na kesho kutwa watastahafu kazi zao na kurudi uraiani kwenye umasikini imara) wataamua kuwaua WaTZ wanaodai kuibiwa kura zao basi wajue ziko mahakama za kimataifa ambazo hazihongeki na watapelekwa tuu.Wakifanya kama Kenya kumuapisha haraka......na matokeo yatakuwa kama Kenya......Koffi Annan, Obasanjo n.k wajiandae!
Wako wapi wakina Taylor? wakina El Bashir anaishi kama swala leo na Kenya kuna wanaosubiri yawafike nk.
Wawaache Watanzania wachague wenyewe nuru au giza. Wakiamua giza kwa utashi wao basi hilo ni lao wenyewe lakini sio kwa kuwaingiza gizani kwa nguvu. Romania na South Africa walikuwa na nguvu kubwa kijeshi lakini tawala hizo ziliangushwa na nguvu ya wananchi sisi hatuna sababu ya kufika huko kwa sababu wananchi wa kawaida ni ndugu kabisa ila itikadi tofauti. Baba Chadema,mama CCM, Mtoto CUF, shangazi NCCR, hapo kwa nini kuuana wenyewe kwa wenyewe kwa ajili ya maslahi ya watu wengine wachache?
WATANZANIA TULIKATAE HILI, tujiulize kwa nini tunafanya uchaguzi wakati yatokanayo na uchaguzi huo wakubwa(kama wanavyojiona wenyewe) hawataki kuyakubali na wanataka kupindisha maamuzi yetu kwa gharama yeyote?