Mkuu huyo uliyeenda kwake sio daktari, ni janga. Hakuna magroup ya damu yanayokinzana kupata mimba. Rhesus +ve na Rhesus -ve zinakinzana, lakini kwa utaalamu wa sasa (kama alivyoeleza mchangiaji hapo juu), matibabu spesheli hufanywa na mtoto huzaliwa.
Kuna mawili: Labda mke wako ni R -ve na wewe ni R+ve, may be hukumuelewa Dr. Kapime tena na kama ndivyo muende hpstali kubwa mtasaidiwa.
Vinginevyo Itakuwa mkeo au wewe kuna tatizo la kiafya. Nakushauri utumie dawa za mimea zaidi (kuna member humu alileta thread juu ya clinic fulani ipo shekilango, itafute)...
Problems with the Rh factor occur when the mother's Rh factor is negative and the baby's is positive. Sometimes, an incompatibility may occur when the mother is blood type O and the baby is either A or B.
Lazima huyo ni Dr. wa mitaani! Ana taaluma kabisa ya udaktari?
Kama mwalimu wa biology ninajua kwamba kinachodetermine usalama wa mtoto ni rhesus factors. Na hii huwa ina effect iwapo tu mama anayo negative na baba akawa nayo positive. Ikitokea kwamba mama akapata mimba ya mtoto ambaye ni rhesus factor positive huwa kunaweza kutokea reaction ambayo inaweza kumuaffect mtoto. Lakini kwa case yenu hampo huko. Hata hivyo, mama mwenye rhesus factor negative huwa anachomwa sindano miezi miwili ya mwanzo ya mimba na anakuwa salama. Sasa huyu ni daktari gani anayetoa majibu ya jumla kiasi hicho? Majibu yake si ya kisayansi kabisa.
That is very true! Nina shuhuda nyingi za couples waliopata mtoto wa kwanza bila shida.With Rh hakuna tatizo kwa mtoto wa kwanza.
umeona eeeh!maswali kwa huyu dokta muhimu aisee!Ila kwa kweli kwa jinsi mie nilivyo na maswali kwa madaktari.....huyo daktari ingembidi kuleta ubao anieleweshe....yaan unadanganywa kirahisi namna hiyo....!!!No wonder biology ikawa compulsory!!!
Pole kwa tatizo ndugu.Wana JF poleni na shughuri za Kila cku! Nimejitokeza Mbele yenu kuomba Masada kufuatia majibu tuliyopata kutoka kwa Dk mmoja. Ni hivi Mimi na Mke wangu tangu tumefunga ndoa sasa ni zaidi ya Mwaka mmoja na nusu Mke wangu alihangaika sana kupata ujauzito lakini baada Kama ya miezi 6 alifanikiwa mimba ikanasa.
Tulipata furaha sana baada ya kuomba sana na hatimaye Mungu akajibu maombi yetu, kwa bahati mbaya sana furaha ilidumu kwa miezi 2 tu kwani wife alijikuta amepata tatizo la miscarriage. Ilibidi twende hospitali alisafishwa salama, lakini ikabidi tuombe ushauri kwa Dk kwanini hii Hali imetokea ndipo Dk ktk kumuuliza wife Kuwa alitumia kitu gani eg. Chakula au kinywaji kilichopelekea Hali hii? Basi ktk mahojiano ya muda mrf na Dk ilibainika Kuwa wife kuna cku alitumia vitunguu swaumu vilivyopondwapondwa akachanganya na asali akala, hii ni kawaida yake kwani anapopata homa ndogo hutumia vitu hvyo huwa hapendi kutumia dawa za hospital.basi Dk aka conclude Kuwa ndo chanzo cha miscarriage.
Baada ya miezi 2 akapata tena ujauzito uliodumu kwa miezi 3 tu nao ukatoka, tukaenda tena hospital na Dk akatupima magrupu ya Damu zetu wote vipimo vikasema tuna Damu Group A positive na ndipo akasema kwa Damu zenu hizi Hamuwezi kupata mtoto. Ikitokea Mke wangu akapata ujauzito hadi hatua ya kujifungua basi atajifungua Kiumbe ambacho c riziki na hata kikiwa riziki basi mtoto huyo atafariki baada ya muda Fulani sababu Damu zenu hazipatani yaani positive na positive lazima zikwepane.
NB. Damu zetu Kuwa Group A positive simaanishi Kuwa ni HIV Positive la hasha!
Ngugu zangu naombeni msaada wenu kwani ndoa Yangu sasa ipo mashakani hakuna mwenye furaha ni simanzi na majonzi tu Kila cku. Kosa lilifanyika kwa kutopima magrupu ya Damu zetu mapema Kabla ya kufunga Ndoa. Naombeni msaada wenu Jamani.
Pole kwa tatizo ndugu.
Hilo tatizo limewahi kuipata familia ya ndugu yangu. Yeye, mtoto wa kwanza alizaliwa si riziki, wa pili alifariki baada ya siku nne. Kwa sasa wana mtoto aliye hai, ana mwaka na nusu. Kuna mbinu za kitaalamu huwa wanafanya mahospitalini, ambapo mama hudungwa sindano za ku neutralize hizo tofauti zenu. Nitumie namba yako kwenye PM kwa taarifa za faragha zaidi.
Sawa, nitakupigia muda si mrefu.Mkuu chukua hyo ya kwangu ili tuwasiliane, nayeyote aliye nania njema naomba msaada zaidi. 0782040509
mkuu nashukuru kwa Hiyo chati ya ufafanuzi hakika imetupa Amani hapa nyumbani , kwani toka tumeambiwa hivyo na daktari, wife amekuwa mtu wa kulia tu Kila cku, nimijuunga JF 21july 2013. Kwasasabu ya kutafuta ushaur naona sasa naweza kufanikiwa zaidi. Aksanteni wakuu.
duh very educative! Mimi ni A+ sasa ngoja nijue mapema blood group ya my Gf..
Na je,hiyo Rhesus factor ni nini?
Nipo Mwanza kaka hapa Saut nafanya M.A Ed.
Mwanza hapo muulizie Dr
Kilonzo sina uhakika anapatikana wapi ila anzia Bugando ni bingwa wa
maswala hayo