Mkuu huyo uliyeenda kwake sio daktari, ni janga. Hakuna magroup ya damu yanayokinzana kupata mimba. Rhesus +ve na Rhesus -ve zinakinzana, lakini kwa utaalamu wa sasa (kama alivyoeleza mchangiaji hapo juu), matibabu spesheli hufanywa na mtoto huzaliwa.
Kuna mawili: Labda mke wako ni R -ve na wewe ni R+ve, may be hukumuelewa Dr. Kapime tena na kama ndivyo muende hpstali kubwa mtasaidiwa.
Vinginevyo Itakuwa mkeo au wewe kuna tatizo la kiafya. Nakushauri utumie dawa za mimea zaidi (kuna member humu alileta thread juu ya clinic fulani ipo shekilango, itafute)...