DOCTOR: Kwa Damu yako hii na Mke wako, Kamwe Hamuwezi kupata mtoto/watoto!

DOCTOR: Kwa Damu yako hii na Mke wako, Kamwe Hamuwezi kupata mtoto/watoto!

Mkuu pole sana. Mosi, usikate tamaa kwani yawezekana ni swala la muda tu. Pili nakushauri ukaonane na daktari bingwa ili vifanyike vipimo kwa undani zaidi kujua chanzo. Nina wasiwasi na mawasiliano yaliyopo kati yako na daktari wako kwani yawezekana hamuongei lugha moja.
 
You are details are true mkuu, thats waht I do understand too. Ila hiyo fact ya doctor i dont know for real. Kimsinginahisi kuna masuala mengine ila ishu ya blood groups kuwa sawa mhhhhh.....lets make more indepth research and see............
🙂
 
. Huyo daktari wako Mangungu achana nae tafuta gyno wa kueleweka
 
Mkuu huyo uliyeenda kwake sio daktari, ni janga. Hakuna magroup ya damu yanayokinzana kupata mimba. Rhesus +ve na Rhesus -ve zinakinzana, lakini kwa utaalamu wa sasa (kama alivyoeleza mchangiaji hapo juu), matibabu spesheli hufanywa na mtoto huzaliwa.
Kuna mawili: Labda mke wako ni R -ve na wewe ni R+ve, may be hukumuelewa Dr. Kapime tena na kama ndivyo muende hpstali kubwa mtasaidiwa.
Vinginevyo Itakuwa mkeo au wewe kuna tatizo la kiafya. Nakushauri utumie dawa za mimea zaidi (kuna member humu alileta thread juu ya clinic fulani ipo shekilango, itafute)...

Nilikuwa sijui hili kweli mungu ni mwema kwa sie Waafrica tunapata watoto by chance maana mpaka mtoto anazaliwa wazazi wengi hata group za damu zao hawajui na tukipima wakati tunataka kuoana ni kuangalia ngwengwe tu
 
Pia nenda Muhimbili mtafute Dr Angela Thomas ni dr mzuri sana aweza kua msaada ,miaka kama 3 iliyopita alikua anapatikana TUMAINI HOSPT sasa sijui kama bado yupo hapo.
 
Lazima huyo ni Dr. wa mitaani! Ana taaluma kabisa ya udaktari?
Kama mwalimu wa biology ninajua kwamba kinachodetermine usalama wa mtoto ni rhesus factors. Na hii huwa ina effect iwapo tu mama anayo negative na baba akawa nayo positive. Ikitokea kwamba mama akapata mimba ya mtoto ambaye ni rhesus factor positive huwa kunaweza kutokea reaction ambayo inaweza kumuaffect mtoto. Lakini kwa case yenu hampo huko. Hata hivyo, mama mwenye rhesus factor negative huwa anachomwa sindano miezi miwili ya mwanzo ya mimba na anakuwa salama. Sasa huyu ni daktari gani anayetoa majibu ya jumla kiasi hicho? Majibu yake si ya kisayansi kabisa.

Problems with the Rh factor occur when the mother's Rh factor is negative and the baby's is positive. Sometimes, an incompatibility may occur when the mother is blood type O and the baby is either A or B.
 
Lazima huyo ni Dr. wa mitaani! Ana taaluma kabisa ya udaktari?
Kama mwalimu wa biology ninajua kwamba kinachodetermine usalama wa mtoto ni rhesus factors. Na hii huwa ina effect iwapo tu mama anayo negative na baba akawa nayo positive. Ikitokea kwamba mama akapata mimba ya mtoto ambaye ni rhesus factor positive huwa kunaweza kutokea reaction ambayo inaweza kumuaffect mtoto. Lakini kwa case yenu hampo huko. Hata hivyo, mama mwenye rhesus factor negative huwa anachomwa sindano miezi miwili ya mwanzo ya mimba na anakuwa salama. Sasa huyu ni daktari gani anayetoa majibu ya jumla kiasi hicho? Majibu yake si ya kisayansi kabisa.

With Rh hakuna tatizo kwa mtoto wa kwanza.
 
Ila kwa kweli kwa jinsi mie nilivyo na maswali kwa madaktari.....huyo daktari ingembidi kuleta ubao anieleweshe....yaan unadanganywa kirahisi namna hiyo....!!!No wonder biology ikawa compulsory!!!
umeona eeeh!maswali kwa huyu dokta muhimu aisee!
 
Wana JF poleni na shughuri za Kila cku! Nimejitokeza Mbele yenu kuomba Masada kufuatia majibu tuliyopata kutoka kwa Dk mmoja. Ni hivi Mimi na Mke wangu tangu tumefunga ndoa sasa ni zaidi ya Mwaka mmoja na nusu Mke wangu alihangaika sana kupata ujauzito lakini baada Kama ya miezi 6 alifanikiwa mimba ikanasa.

Tulipata furaha sana baada ya kuomba sana na hatimaye Mungu akajibu maombi yetu, kwa bahati mbaya sana furaha ilidumu kwa miezi 2 tu kwani wife alijikuta amepata tatizo la miscarriage. Ilibidi twende hospitali alisafishwa salama, lakini ikabidi tuombe ushauri kwa Dk kwanini hii Hali imetokea ndipo Dk ktk kumuuliza wife Kuwa alitumia kitu gani eg. Chakula au kinywaji kilichopelekea Hali hii? Basi ktk mahojiano ya muda mrf na Dk ilibainika Kuwa wife kuna cku alitumia vitunguu swaumu vilivyopondwapondwa akachanganya na asali akala, hii ni kawaida yake kwani anapopata homa ndogo hutumia vitu hvyo huwa hapendi kutumia dawa za hospital.basi Dk aka conclude Kuwa ndo chanzo cha miscarriage.


Baada ya miezi 2 akapata tena ujauzito uliodumu kwa miezi 3 tu nao ukatoka, tukaenda tena hospital na Dk akatupima magrupu ya Damu zetu wote vipimo vikasema tuna Damu Group A positive na ndipo akasema kwa Damu zenu hizi Hamuwezi kupata mtoto. Ikitokea Mke wangu akapata ujauzito hadi hatua ya kujifungua basi atajifungua Kiumbe ambacho c riziki na hata kikiwa riziki basi mtoto huyo atafariki baada ya muda Fulani sababu Damu zenu hazipatani yaani positive na positive lazima zikwepane.

NB. Damu zetu Kuwa Group A positive simaanishi Kuwa ni HIV Positive la hasha!

Ngugu zangu naombeni msaada wenu kwani ndoa Yangu sasa ipo mashakani hakuna mwenye furaha ni simanzi na majonzi tu Kila cku. Kosa lilifanyika kwa kutopima magrupu ya Damu zetu mapema Kabla ya kufunga Ndoa. Naombeni msaada wenu Jamani.
Pole kwa tatizo ndugu.
Hilo tatizo limewahi kuipata familia ya ndugu yangu. Yeye, mtoto wa kwanza alizaliwa si riziki, wa pili alifariki baada ya siku nne. Kwa sasa wana mtoto aliye hai, ana mwaka na nusu. Kuna mbinu za kitaalamu huwa wanafanya mahospitalini, ambapo mama hudungwa sindano za ku neutralize hizo tofauti zenu. Nitumie namba yako kwenye PM kwa taarifa za faragha zaidi.
 
Pole kwa tatizo ndugu.
Hilo tatizo limewahi kuipata familia ya ndugu yangu. Yeye, mtoto wa kwanza alizaliwa si riziki, wa pili alifariki baada ya siku nne. Kwa sasa wana mtoto aliye hai, ana mwaka na nusu. Kuna mbinu za kitaalamu huwa wanafanya mahospitalini, ambapo mama hudungwa sindano za ku neutralize hizo tofauti zenu. Nitumie namba yako kwenye PM kwa taarifa za faragha zaidi.

Mkuu chukua hyo ya kwangu ili tuwasiliane, nayeyote aliye nania njema naomba msaada zaidi. 0782040509
 
kuna dada mmoja namfahamu yeye mimba zilitoka 11,ya 12 ndio akazaa salama.hakukata tamaa.huyo dada ana uzazi balaa.hospitali aliambiawa kuwa hata akibeba mimba mtoto atafariki tu.huyo wa 12 ni pre mature lakini mzima kabisa.ana ugonjwa ambao nimeusahau jina tatizo kwake ni hilo ndio linalomfanya mimba zake ziharibike
 
mkuu nashukuru kwa Hiyo chati ya ufafanuzi hakika imetupa Amani hapa nyumbani , kwani toka tumeambiwa hivyo na daktari, wife amekuwa mtu wa kulia tu Kila cku, nimijuunga JF 21july 2013. Kwasasabu ya kutafuta ushaur naona sasa naweza kufanikiwa zaidi. Aksanteni wakuu.

Nafikiri mlionana na clinical officer (afisa tabibu) na si Daktari (Medical Doctor). Nawashauri muonane na daktari bingwa (Obs and gyne) atawasaidia. Ni kweli hutokea group za damu (rhesus factors) zikawa haziendani, lakini huwa kuna sindano maalumu (ina gharama - ant - D) huchomwa kwa mjamzito ili kuondoa mgongano wa cells za mama na zile za mtoto. Kimsingi, kutokana na kutokukubaliana kwa rhesus factor, kiumbe kilichopo tumboni huonekana kama foreign body na mwili wa mama hutengeza mazingira ya kukitoa nje mapema iwezekanavyo. Usikate tamaa, utapata mtoto!
 
Mwanza hapo muulizie Dr Kilonzo sina uhakika anapatikana wapi ila anzia Bugando ni bingwa wa maswala hayo
 
duh very educative! Mimi ni A+ sasa ngoja nijue mapema blood group ya my Gf..
Na je,hiyo Rhesus factor ni nini?
 
duh very educative! Mimi ni A+ sasa ngoja nijue mapema blood group ya my Gf..
Na je,hiyo Rhesus factor ni nini?

Rhesus factor ni aina ya blood proteins flan ziligunduliwa kwa Rhesus monkeys,kwa hiyo rhesus factor ilipewa jina hilo kwa sababu iligunduliwa kutoka kwenye rhesus monkeys.However,wale wenye Rh+ inamaanisha wanazo hizo proteins na wale wenye Rh- inamaana hawana hizo proteins.Hizi factors ni inherited,yaan zinakuwa transmitted from kizazi kimoja kwenda kingine.Na zina influence kwenye haya ma'complexities ya kuishi kwa watoto walio tumboni....just google utaielewa zaidi.

http://anthro.palomar.edu/blood/Rh_system.htm
 
Hakuna kitu kama icho, pangekua na shida endapo mama angekua na negative Rh na wewe ukawa na iyo positive kwa kuwa positive Rh ni dominant kwa negative then mtoto lazima angekuwa na positive na hapo ndipo kungekuwa na shida kwan mwili wa mama ungetambua mtoto kama mvamizi na hivyo kutengeneza antibodies kwa ajiri ya kujilinda, kwa mtoto wa kwanza haina shida ila kwa mtoto wa pili mama anaweza poteza maisha wakat wa kujifungua ikitokea mtoto akakua tumbon coz dam zkichanganyikana damu ya mama itacoagulate...
 
Dr Kilonzo alishastaafu siku nyingi bugando, yuko na hospital yake rufiji inaitwa mwanza hospital, mnaweza kwenda hapo pia
Mwanza hapo muulizie Dr
Kilonzo sina uhakika anapatikana wapi ila anzia Bugando ni bingwa wa
maswala hayo
 
Back
Top Bottom