Wana JF poleni na shughuri za Kila cku! Nimejitokeza Mbele yenu kuomba Masada kufuatia majibu tuliyopata kutoka kwa Dk mmoja. Ni hivi Mimi na Mke wangu tangu tumefunga ndoa sasa ni zaidi ya Mwaka mmoja na nusu Mke wangu alihangaika sana kupata ujauzito lakini baada Kama ya miezi 6 alifanikiwa mimba ikanasa.
Tulipata furaha sana baada ya kuomba sana na hatimaye Mungu akajibu maombi yetu, kwa bahati mbaya sana furaha ilidumu kwa miezi 2 tu kwani wife alijikuta amepata tatizo la miscarriage. Ilibidi twende hospitali alisafishwa salama, lakini ikabidi tuombe ushauri kwa Dk kwanini hii Hali imetokea ndipo Dk ktk kumuuliza wife Kuwa alitumia kitu gani eg. Chakula au kinywaji kilichopelekea Hali hii? Basi ktk mahojiano ya muda mrf na Dk ilibainika Kuwa wife kuna cku alitumia vitunguu swaumu vilivyopondwapondwa akachanganya na asali akala, hii ni kawaida yake kwani anapopata homa ndogo hutumia vitu hvyo huwa hapendi kutumia dawa za hospital.basi Dk aka conclude Kuwa ndo chanzo cha miscarriage.
Baada ya miezi 2 akapata tena ujauzito uliodumu kwa miezi 3 tu nao ukatoka, tukaenda tena hospital na Dk akatupima magrupu ya Damu zetu wote vipimo vikasema tuna Damu Group A positive na ndipo akasema kwa Damu zenu hizi Hamuwezi kupata mtoto. Ikitokea Mke wangu akapata ujauzito hadi hatua ya kujifungua basi atajifungua Kiumbe ambacho c riziki na hata kikiwa riziki basi mtoto huyo atafariki baada ya muda Fulani sababu Damu zenu hazipatani yaani positive na positive lazima zikwepane.
NB. Damu zetu Kuwa Group A positive simaanishi Kuwa ni HIV Positive la hasha!
Ngugu zangu naombeni msaada wenu kwani ndoa Yangu sasa ipo mashakani hakuna mwenye furaha ni simanzi na majonzi tu Kila cku. Kosa lilifanyika kwa kutopima magrupu ya Damu zetu mapema Kabla ya kufunga Ndoa. Naombeni msaada wenu Jamani.