Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Athuman Malesa (22) mkazi wa Kijiji cha Kaloleni wilayani Chemba mkoani Dodoma, ameuawa na watu wenye hasira kali kwa kuchomwa moto, akituhumiwa kwa mauaji na kufanya vitendo vya ukatili ikiwemo ubakaji na kulawiti watoto.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Olboloti wilayani Chemba Shabani Maslahi Maslahi amethibitisha kifo hicho.
Amesema hatua hiyo imetokana na kundi la vijana maarufu 'Maronjoo' ambao huishi na mifugo porini kufanya vitendo vya uhalifu na kuua.
Marehemu akiwa na wenzake walisakwa na wananchi wenye hasira kali kisha kuuawa ofisi ya kijiji cha Olboloti huku wengine wakishikiliwa na Jeshi la Polisi
Wanaoshikiliwa na Polisi ni Sefu Malekela (23), na Alhaji Hamad (21) wote wakazi wa Kijiji cha Kaloleni.