Uchaguzi 2020 Dodoma: Anthony Mavunde azomewa na wananchi

Uchaguzi 2020 Dodoma: Anthony Mavunde azomewa na wananchi

Torquemada

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2020
Posts
231
Reaction score
260
Habari wakuu!

Jana, Oct 30 2020 Mbunge aliyeshinda jimbo la Dodoma mjini kwa tiketi ya CCM, ndugu Anthony Mavunde ameshindwa kuongea na wananchi wa Dodoma mjini baada ya kundi kubwa kuanza kumzomea.

Kitu hicho kilimpelekea kuingia kwenye gari na kuondoka kwa aibu kubwa.

Wananchi hao walisikika wakisema " WE NENDA, HATUKUTAKI , HATUJAKUCHAGUA, PANDA GARI UENDE ZAKO"

Hali iliyozua maswali mengi mtandaoni kwamba inakuwaje kuzomewa na kundi kubwa vile tena kipindi alipoenda kutoa shukrani kuchaguliwa?

Hii inaashiria nini tuendako? Na Dodoma si ngome ya CCM?

Je, wananchi wanatuma ujumbe gani kwa hili tukio?

Kusema wenye nchi ni wananchi?

Nisiwachoshe kwa maswali tazama mkasa mzima hapo chini.

 
Hii ndio kutest mitambo, yajayo yanafikirisha sana... Kuna uwezekano mkubwa hii style ( ya wananchi kuanza kuwa shusha wabunge wa CCM toka majukwaani) ikazuka na kutapakaa nchi nzima...CCM jipangeni... madhara ya wizi wa kura...
 
"Wee nenda, hautuhusu, hatujakuchagua, ingia kwenye gari yako uondoke...". Maneno mazito kweli kweli. Eh, hata Dodoma? Watapata sana taabu kwa unyang'anyi wao. Yaani, yaani.... ngoja tuone kati ya umma na jeshi nani ana nguvu. Bila shaka mwisho wao utakuwa mbaya sana kama ulivyo mwisho wa madikteta wote.

CCM kama ni mgeni ambaye amekwishapitisha siku zake za kuwa mgeni lakini hajitambui. Hata mkifanya mema vipi, kama watu wamekwisha wachoka haitasaidia. Mtajenga sana mabarabara, mabwawa, SGR... lakini hayatawaingiza katika mioyo ya watu. You have overstayed. Mtatakiwa kuiba kura tena 2025.
 
Miaka 5 mateso jasho damu....vikwazo
Acha mkuu!

Ndio maana wananchi tumepewa mbadala wa kuandamana kwa HAKI.

Hatuwezi kuporwa HAKI yetu na Serikali kutuchagulia mtu wanayemtaka wao na sio sisi wananchi!

Haingii akilini tukishindwa kutetea HAKI zetu kwa maandamano HALALI.
 
"Wee nenda, hautuhusu, hatujakuchagua, ingia kwenye gari yako uondoke...". Maneno mazito kweli kweli. Eh, hata Dodoma? Watapata sana taabu sana kwa unyang'anyi wao. Yaani, yaani.... ngoja tuone kati ya umma na jeshi nani ana nguvu. Bila shaka mwisho wao utakuwa mbaya sana kama ulivyo mwisho wa madikteta wote.
Nimeshangaa kweli kwa Mavunde kuzomewa wakati kule ndio ngome ya CCM.

Ameondoka kwa aibu, sijui akikaa mwenyewe huwa anajionaje kukataliwa na watu anaotakiwa kuwaongoza!
 
Hio ndio uniform kwa Tanzania nzima ,tusimuonee haya mvivu mzembe mzururaji na mwizi wa maamuzi ya Watanzania ,CCM lazima mwaka huu watarudi nchini kwao,wengi inasemekana wanatokea Rwanda na Burundi , Watanzania tumewashitukia.

Mbunge hata akiingia msikitini au kanisani ama atoke yeye au aachwe peke yake ndani ya sinagogi. Zanzibar imeshaanza msikitini wanaachwa peke yao,akiingia liciciemuwatu wanaondoka wanaenda kuswali kwengine.
 
Back
Top Bottom