TANZIA Dodoma: Asia Saidi, Mwenyekiti wa BAWACHA afariki dunia kwa kupigwa na mshale

TANZIA Dodoma: Asia Saidi, Mwenyekiti wa BAWACHA afariki dunia kwa kupigwa na mshale

Matope

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Posts
892
Reaction score
683
Asia Said Ali (50) Mrangi ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA Kata ya Palanga, Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma, amefariki dunia baada ya kupigwa mshale na Mtu aliyefahamika kwa jina la Haruna Ali Kimata miaka 35.

Marehemu akiwa amekaa na mume wake muda wa saa mbili na nusu Usiku, Waliviziwa na Bwana Haruna Ali Kimeta kwa nia ya Kumpiga Mshale Mume wa Marehemu anayefahamika kwa jina la Iddi Masale miaka 55, lakini Mshale Ukamkosa na kumpata Mke wake Mgongoni ambaye alipoteza maisha Muda mchache baada ya kufikishwa Hospitali ya Kondoa.

Chanzo cha ugomvi, ni kwamba Iddi Masale aliingiza Mifugo kwenye Shamba la Alizeti la Haruna. Siku ya tukio, Mchana Walishinda Wanarumbana na kurushiana maneno Makali.

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto ameiambia JamiiForums kwamba, Mtuhumiwa wamemkamata na Mshale uliotumika wameupata ambao ni kidhibiti na akaongezea kwamba, tukio hili halihusiani na Siasa.
 
Back
Top Bottom