MIMI BABA YENU
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 305
- 728
Unaweza kuta 7bu ni mambo haya haya ya siasa
hii zee liongo sana, nitakuwa wa mwisho kumuamini!.RPC Dodoma Gilles Muroto amesema tukio la kuuawa kwa M/Kiti wa BAWACHA Kata ya Palanga Asia Said, aliyechomwa na mshale halihusiani na siasa, bali ni kuwa mume wa marehemu alikuwa na ugomvi na mtuhumiwa aliyefanya mauaji hayo baada ya kuingiza mifugo kwenye shamba lake.
Asia Said Ali (50) Mrangi ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA Kata ya Palanga, Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma, amefariki dunia baada ya kupigwa mshale na Mtu aliyefahamika kwa jina la Haruna Ali Kimata miaka 35.
Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto ameiambia JamiiForums kwamba, Mtuhumiwa wamemkamata na Mshale uliotumika wameupata ambao ni kidhibiti na akaongezea kwamba, tukio hili halihusiani na Siasa.
Yeah. Kila mtu atalipia kwa anachokifanya. So ni vizuri kutenda wema.mmmnhhhhh
*CHADEMA WAUANA KISA VITIMAALUM*Asia Said Ali (50) Mrangi ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA Kata ya Palanga, Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma, amefariki dunia baada ya kupigwa mshale na Mtu aliyefahamika kwa jina la Haruna Ali Kimata miaka 35.
Marehemu akiwa amekaa na mume wake muda wa saa mbili na nusu Usiku, Waliviziwa na Bwana Haruna Ali Kimeta kwa nia ya Kumpiga Mshale Mume wa Marehemu anayefahamika kwa jina la Iddi Masale miaka 55, lakini Mshale Ukamkosa na kumpata Mke wake Mgongoni ambaye alipoteza maisha Muda mchache baada ya kufikishwa Hospitali ya Kondoa.
Chanzo cha ugomvi, ni kwamba Iddi Masale aliingiza Mifugo kwenye Shamba la Alizeti la Haruna. Siku ya tukio, Mchana Walishinda Wanarumbana na kurushiana maneno Makali.
Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto ameiambia JamiiForums kwamba, Mtuhumiwa wamemkamata na Mshale uliotumika wameupata ambao ni kidhibiti na akaongezea kwamba, tukio hili halihusiani na Siasa.
Pole kwa wafiwa.
Jamaa kamponza mkewe na mtuhumiwa kwa kuingiza mifugo kwenye shamba la mwenzake.
So sad, [emoji29][emoji29][emoji29][emoji29][emoji29][emoji29]....
Watu hawana huruma japo chembe dah
Apumzike kwa amani
Jamani ungesoma habari yote hayo maswali yako ungejijibu mwenyewe bila kugusa key nyingi kivile.Vipi Polisi wanasemaje? Nani amehusika? Je, waliofanya kitendo hicho wameshikwa? Wapi hiyo habari kamili inapatikana?