Bado tuna wabunge ambao kimsingi wamekaa kishabiki zaidi kuliko kujadiri mambo yaliyoko mbele yetu na mbele yao. Nimewasikiriza wabunge wengi lakini wawili wao yaani Mh.Waitara kutoka Tarime na Mh.Nape mbunge wa Mtama. Wabunge hao wamepewa muda mzuri tu wakuweza kuchangia lakini kwa kiasi kikubwa wameacha mjadara muhimu na kuanza mjadara ambao kimsingi sikuona (mimi kama mimi) haja ya kujikita kujadiri kauli na hotuba ya Mh.Mbowe.
Ukweli ni moja ya wabunge ambao nilitegemea waunge mkono hoja kwa kutoa elimu,ushauri na kuwaondelea wananchi hofu iliyopo juu ya huu ushirikiano ila wame ignore nasijui kama wamejitambua kua wamefanya blunder. Ifike maali wabunge wetu watambue wajibu na kiu ya wananchi mambo ya kusema Mh.Rais lazma 2025-2030 sioni kama it is big deal kwakua Katiba ya nchi naya CCM inaruhusu ilo.
Nimpongeze mbunge Aida Kenani viti maalum (CHADEMA) Huyu mbunge amejitahidi sana kuionyesha serikali na bunge kwa ujumla wake.Kaonyesha ni lipi wananchi wengi wamefikiri,wameaminishwa na kukaririshwa ili serikali iweze kutoa majibu na kuwaondolea hofu watanzania ,kwa ili ameonyesha nia njema sana. Nilitamani mbunge wa CCM aweze kusimama na kujibu hoja au kuelimisha jamii kuhusu ilo.
Mwisho wa siku ,wabunge wetu kuna jambo wanabidi wakumbuke kua wapo Bungeni kuwasemea wananchi wao,sehemu rahisi ya wao kuelimisha na kuwawakirisha wananchi ni Bungeni.Wabunge watambue kua kuwepo Bungeni sio kua mtu huyo anazo haki sana,akili sana na bahati sana ...hapana ni kua ndiyo kapata nafasi na wananchi wamemtuma. Ni wakati sasa serikali yetu pendwa ya CCM kuchukua mazuri ili kuboresha mashirikiano haya...maana tuna imani kua malengo ni mazuri kwa Taifa letu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA