Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Madalali wa DP world washakunja chao mapema.

Msukuma kapata V8 LC 300 safi.
Mkuu keshokutwa narejea DIZIM...nitumie "contacts" zako "bobo" ili tuwasiliane...

Nikifika nitakutumia "chupa 2 kubwa za Ciroc" kwa UBER....si unajua tena NEEMA JUU YA NEEMA kakaa[emoji1787]

Nawe komredi umlambe "mnyama" Ciroc ulisuuze koo lako lililozoea "smart Gin" na shengena.....[emoji1787]

#MamaAnaupigaMwingi[emoji120]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mkataba huu utafanya watu waogope kugombea urais Tz kwa kuwa hakuna rais ataruhusiwa kuuvunja au kuurekebisha. Mama kaua kiu ya wawania urais.

Lakini zaidi DP World itakuwa na nguvu kuliko Katiba ya JMT kwa sababu hata marekebisho yoyote ya Katiba au Katiba mpya yoyote haitaruhusiwa kugusa mkataba wa DP World. Ni mkatabamsahafu usiogusika na wenye nchi yao JMT.

Katiba ya JMT itakuwa subordinate kwa DP World na hivyo nchi kutweza sovereignty yake.

Aidha, Katiba ya Znz itakuwa Superior kwa Katiba ya JMT kwa kuwa DP World hawaruhusiwi na Katiba ya SMZ kugusa bandari ya Znz.

Yote haya yanachagiza mabadiliko ya Katiba ya JMT lkn kwa tahadhari kubwa ya kutogusa maslahi ya DP World.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Hivi Bunge letu lina jipya na cha maana kweli ukiondoa compliance ya Katiba? Nina maanisha does it meet objectives of its establishment or it merely the matter of Katiba compliance?
Mkataba huu utafanya watu waogope kugombea urais Tz kwa kuwa hakuna rais ataruhusiwa kuuvunja au kuurekebisha. Mama kaua kiu ya wawania urais.

Lakini zaidi DP World itakuwa na nguvu kuliko Katiba ya JMT kwa sababu hata marekebisho yoyote ya Katiba au Katiba mpya yoyote haitaruhusiwa kugusa mkataba wa DP World. Ni mkatabamsahafu usiogusika na wenye nchi yao JMT.

Katiba ya JMT itakuwa subordinate kwa DP World na hivyo nchi kutweza sovereignty yake.

Aidha, Katiba ya Znz itakuwa Superior kwa Katiba ya JMT kwa kuwa DP World hawaruhusiwi na Katiba ya SMZ kugusa bandari ya Znz.

Yote haya yanachagiza mabadiliko ya Katiba ya JMT lkn kwa tahadhari kubwa ya kutogusa maslahi ya DP World.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu keshokutwa narejea DIZIM...nitumie "contacts" zako "bobo" ili tuwasiliane...

Nikifika nitakutumia "chupa 2 kubwa za Ciroc" kwa UBER....si unajua tena NEEMA JUU YA NEEMA kakaa[emoji1787]

Nawe komredi umlambe "mnyama" Ciroc ulisuuze koo lako lililozoea "smart Gin" na shengena.....[emoji1787]

#MamaAnaupigaMwingi[emoji120]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
^Profesa, mkataba huu ni wa miaka mingapi?^

Prof. Mbarawa: ^Mkataba utakuwa hai mpaka pale ambapo shughuli za miradi zitasitishwa, au kuisha kwa muda wa mikataba ya nchi mwenyeji na mikataba ya miradi. Msingi wa mkataba huu kuendana na mikataba ya miradi ni kutokana na kwamba unaweka msingi unaowezesha kuingia na kutekelezwa kwa mikataba hiyo nchini.^

Aliyeelewa please
 
Mkataba huu utafanya watu waogope kugombea urais Tz kwa kuwa hakuna rais ataruhusiwa kuuvunja au kuurekebisha. Mama kaua kiu ya wawania urais.

Lakini zaidi DP World itakuwa na nguvu kuliko Katiba ya JMT kwa sababu hata marekebisho yoyote ya Katiba au Katiba mpya yoyote haitaruhusiwa kugusa mkataba wa DP World. Ni mkatabamsahafu usiogusika na wenye nchi yao JMT.

Katiba ya JMT itakuwa subordinate kwa DP World na hivyo nchi kutweza sovereignty yake.

Aidha, Katiba ya Znz itakuwa Superior kwa Katiba ya JMT kwa kuwa DP World hawaruhusiwi na Katiba ya SMZ kugusa bandari ya Znz.

Yote haya yanachagiza mabadiliko ya Katiba ya JMT lkn kwa tahadhari kubwa ya kutogusa maslahi ya DP World.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Porojo hizo, kujaza watu ujinga uliokujaa.

Soma article 20.
 
Azimio la Bunge kuhusu Pendekezo la Kuridhiwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii katika Uendelezaji wa Maeneo ya Bandari Nchini leo Juni 10, 2023.

======

Leo Juni 10, 2023, Bunge la Tanzania linatarajia kujadili mkataba kati ya Serikali na Kampuni ya DPWorld unaodaiwa kutotaja ukomo kuhusu Ushirikiano katika Uendeshaji, Uendelezaji na Uboreshaji wa Bandari zote za Baharini na Maziwa zilizopo Tanzania Bara

Mkataba umeibua maswali ambayo hayajapatiwa ufafanuzi wa kina ikiwemo thamani na muda wa uendeshaji pamoja na sababu za Tanzania kuingia mkataba na kampuni inayotajwa katika kesi za ukwepaji kodi na migogoro katika utekelezaji mikataba huku baadhi ya Nchi zikiikataa kampuni hiyo.

Je, unaufahamu kiasi gani Ushirikiano wa DP-World na Bandari?

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anawasilisha Pendekezo la Kuridhiwa kwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anawasilisha Pendekezo la Kuridhiwa kwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii katika Uendelezaji wa Maeneo ya Bandari Nchini, leo Juni 10, 2023

UTOAJI HUDUMA HAUJAFIKIA VIWANGO VINAVYOTAKIWA KIMATAIFA
Prof. Mbarawa amesema: "Pamoja na kuchukua hatua mbalimbali za maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam, bado ufanisi katika utoaji Huduma za haujafikia viwango vinavyotakiwa kimataifa.”

“Hali ya sasa ya utendaji imeendelea kuwa ya kiwango cha chini ikilinganishwa na Bandari shindani kikanda. Kwa mfano, wastani wa meli kusubiri nangani kwa Bandari ya Dar es salaam ni Siku 5 ikilinganishwa na Siku 1.25 kwa Bandari ya Mombasa na siku 1.6 kwa Bandari ya Durban.”

"Ufanisi mdogo wa Bandari ya Dar umetokana na changamoto ikiwemo kukosekana kwa Mifumo ya kisasa ya TEHAMA, maeneo ya kutosha ndani na nje ya Bandari kwa ajili ya kuhifadhia shehena, Maegesho ya Meli, mitambo ya kutosha na ya kisasa ya kuhudumia shehena ambayo ina gharama kubwa ya Uwekezaji.”

“Meli kutumia muda mrefu kupakia na kupakua shehena gatini kwa wastani wa Siku 5 ikilinganishwa na Siku 1 inayokubalika Kimataifa, pamoja na Meli kubwa kutokuja katika Bandari ya Dar kutokana na kuchukua muda mrefu kuhudumiwa

MSINGI WA MKATABA HUU KUENDANA NA MIKATABA
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema Mkataba wa DP World kuendesha Bandari utakuwa hai mpaka pale ambapo shughuli za Miradi zitasitishwa au kuisha kwa muda wa Mikataba ya Nchi mwenyeji na Mikataba ya miradi

Amesema "Msingi wa Mkataba huu kuendana na Mikataba ya miradi ni kutokana na kwamba unaweka msingi unaowezesha kuingia na kutekelezwa kwa Mikataba 10 Nchini."

KAMPUNI YA DP WORLD INA UZOEFU WA KUENDESHA BANDARI BARANI AFRIKA
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi amesema Kampuni ya DP World ina uzoefu katika uendeshaji wa shughuli za Bandari Barani Afrika, Asia, Ulaya na Amerika ya Kaskazini na Kusini

Amesema "Baadhi ya Kampuni zilizowasilisha nia ya kuwekeza Bandarini hazina wakati Kampuni ya DP World inaendesha takriban Bandari 6 Afrika na Bandari zaidi ya 30 Duniani kote kwa ufanisi mkubwa.”

DP WORLD INATAKIWA KUENDELEZA AJIRA ZA WATUMISHI WALIOPO
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema “Uwepo wa ajira za Watanzania hususani Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam ni kipaumbele kikubwa cha Serikali sio tu katika Azimio hili bali katika kila aina ya uwekezaji ambao Nchi itaufanya.”

Amesema “Ibara ya 13 ya Mkataba huu inaitaka DP World kuendeleza ajira za Watumishi wote waliopo, kuwaajiri Watanzania pamoja kuwaendeleza kitaaluma.”

TAUHIDA: KIONGOZI ANAYETAMKA KAULI ZA UBAGUZI TUNAMSHANGAA SANA

Mbunge Tauhida Gallos Nyimbo amesema “Nikimuona kiongozi anayewaongoza watu anatamka kauli ya kibaguzi tunamshangaa sana, mimi natokea Songea, mama yangu ni Mzaramu lakini ni Mbunge wa #Zanzibar.”

Ameongeza “Serikali haikatai kukosolewa, ikikosolewa inafanya uboreshaji zaidi.”

MDEE: MKATABA WA DP WORLD UMETAJA VITU KIJUMLAJUMLA
Akizungumzia mkataba wa #Tanzania na Kampuni ya #DPWorld, Mbunge #HalimaMdee amesema “Tuna nafasi ya kubadilisha baadhi ya vitu katika Mkataba huu lakini najua hatutabadilisha

Ameongeza “Kama Mkataba huu unagusa Mtwara, Tanga, Mwanza, Dar es Salaam na Kigoma kwani usizungumzwe kwa mapana yake? Tukiupitisha unaenda kuwa mkataba wa Kimataifa, chochote ambacho kimetajwa kijumlajumla kuhusu Bandari kitahusika.”

BOFYA HAPA KUSOMA: Maoni ya Kamati ya Pamoja Kuhusu Azimio la Bunge Kuridhia Makubaliano Kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali Ya Dubai Kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii Kwa Ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji Wa Utendaji Kazi wa Bandari Tanzania la Mwaka 2023

RASMI: BUNGE LAPITISHA AZIMIO LA KUUNGA MKONO MKATABA WA TANZANIA NA DP WORLD
View attachment 2653047View attachment 2653047View attachment 2653047View attachment 2653047View attachment 2653047
Bunge limepitisha mkataba kuhusu Ushirikiano wa Tanzania na Kampuni ya Dubai ya DPWorld katika Uendeshaji, Uendelezaji na Uboreshaji wa Bandari zote za Baharini na Maziwa zilizopo Tanzania Bara, ikiwemo Bandari ya Dar es Salaam

Sehemu ya Azimio hilo imesomeka, "kwa kuzingatia manufaa ambayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itayapata kutokana na Mkataba huu, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wake wa 11 na kwa mujibu wa Ibara ya 63(3)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, linaazimia kuridhia Makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai Kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii kwa ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi katika Bandari Tanzania"

Mkataba huo uliibua maswali kutoka kwa Wananchi ikiwemo thamani na muda wa utekelezaji
Kuna mahali lipo tatizo kubwa kabisa na hata Rais sijui kama analijua.
Unajiuliza je Hawa walioweka mkono saini je walisoma mstari hadi mwisho.
Kwa kuwa Mh. Rais yeye anapoenda mahali anaandamana na Hao mawaziri husika.

Wanapoingia kusaini hii mikataba Hawa wanapewa Ile kurasa ya mwisho ya kuweka saini bila kusoma yaliyopo ndani kwani ni mrefu na muda pia..
Hatuoni alikoweka saini Rais si ajabu Hawa ndio matokeo ya yote haya kuingiziwa mapungufu kibao.

Sasa basi na Hawa wabunge wetu mambuluma wanapitishaje kitu yenye mapungufu kivile? Hawasomi na hata kama hawasomi je hawasikii mawazo na maoni ya wajuvi huku mtandaoni??

Mh. Rais unahujumiwa na bado hushtuki! Huu hauna tofauti na aliokataa Hayati Yale ya Bagamoyo! Huu nao umezidi kiwango. Rais umeupitia kabla
???
 
Kuna mahali lipo tatizo kubwa kabisa na hata Rais sijui kama analijua.
Unajiuliza je Hawa walioweka mkono saini je walisoma mstari hadi mwisho...
Wasiwasi wako tu.

DP World wanakwenda kutuingizia mapato yanayolingana na nusu bajeti ya nchi ya kila "fiscal year"....

Hakika mama anaupiga mwingi[emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna Bunge hapo.

Labda useme Mh.Rais SSH anakua wa kwanza kuruhusu mjadala wa mikataba katika kikao cha chama chake ambacho yeye ni mwenyekiti, bila yeye kuhudhuria kikao hicho.
[emoji15][emoji15][emoji1787][emoji1787]

Hakuna bunge na wabunge walikuwa kikaoni ?!!!

Mkuu una "delusion"?!!!

Hilo ndilo bunge letu...liko kikatiba[emoji1787]

#Tuko na DP WORLD [emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom