Dodoma City vs Arusha City (The Battle of Tanzania Capital City vs EAC Capital City)

Na hapo wamejumlisha kata za tarafa za vijijini...tarafa ya hombolo,zuzu na kikombo...kata za tarafa ya dodoma hazifikishi watu laki 5.[emoji16]
 
Na hapo wamejumlisha kata za tarafa za vijijini...tarafa ya hombolo,zuzu na kikombo...kata za tarafa ya dodoma hazifikishi watu laki 5.[emoji16]
Hombolo,Zuzu na Kikombo zipo chini ya mamlaka ipi....kwani hizo ni ngeni au zimeongezwa baada ya Dodoma kuwa Jiji...!!?
Kabla ya Dodoma kupandishwa kuwa Jiji ilikua na hadhi ya Manispaa na hizo zote zilikua under jurisdiction ya Dodoma Municipality naona unaokoteza okoteza tu utoporooo wa kubishana
 
Arusha mnajikuuuuta, eti Arusha na Dar zilikosa mpinzani nchini.
Ndio Arusha ni jiji ila bado ni pori
Aliyeandika ni mtu wa dodoma Bwana nasri kingine arusha na Daresalaam ni majiji mawili yanayoongoza sekta tofauti kabisa mkuu dar ni jiji la biashara arusha ni jiji la utalii na diplomasia...huo upori pori ndio utalii wenyewe hasa watu wakitoka kutafuta dar wanaenda kupumzika arusha na zanzibar sasa kwahio kila mtu ni kiongozi eneo lake.
Nb. Asilimia 80 ya kodi yote tanzania inakusanywa dar...vilevile Asilimia 80 ya watalii wote nchini wanapitia arusha
Kwahio hakuna haja ya mashindano hapa yote ni miji muhimu ya nchi yetu mwanza ni jiji letu la pili kwa ukubwa na dodoma ni makao makuu yetu jitihada lazima zifanyike kuboresha miundominu yetu bado tuna safari ndefu
 
Hakuna aliyepinga hilo mkuu hapo unajitekenya na kucheka mwenyewe😀
Mamlaka ya ustawishaji makao makuu wakati ule CDA waliona kwa manufaa ya ukuaji wa makao makuu wa baadae ni vyema waweke mipaka mikubwa kwa kutambua kuwa ni makao makuu for future development ili baadae wasije wakapata ugumu wa kuplan kwahio unachokiona hapo jiji la Dodoma lina eneo mara mbili zaidi ya mkoa wa Daresalaam na bado population yake ni laki 7 tu😀 angekua mwanafunzi tungemchapa na viboko kabisa licha ya support yote inayopewa na serikali miaka yote bunge liko huko jitihada zilizofanya na awamu ya 5 kuhamishia watu Dodoma bado mko laki 7😃😃 kwenye eneo ambalo ni mara 10 ya mbeya mara 10 ya arusha mara 6 ya mwanza na mara mbili ya mkoa wote wa dar kwanza mnatutiaga aibu tukibattle na wakenya kwenye thread zao mnatupa kazi kuwatetea😀😀 badala yake mnajitia kiburi mkijiona wakubwa kwani hatujui hata hizo barabara mnazojengewa kwa kodi zetu zingekua na maana zaidi arusha mbeya na mwanza ambalo ni jiji la pili kwa ukubwa sisi tuko kimya tumetulia ....nyie mngepaswa mtulie manake kila kitu mnapewa kwa hisani kwa vile ni makao makuu hampo kwenye mikoa inayoongoza gdp wala makusanyo ya tra trust me hata morogoro ingekua inapewa priority kama nyie kwa sqkm hizo wangekua na watu zaidi ya 1m nyie mko na laki 7 bado mnapiga kelele😀😀😀 ukiitembea Dodoma ndio utajua bado mnasafari ndefu kuwa vibrant city atleast kama mbeya mji wenu unakua mpana with nothing if it was me nisingeutanua mji that way miji sikuhizi inakwenda juu kwa majengo ya kuvutia dubai, joberg yote ina sqkm 600 tu ukiweka mji uwe mpana sana na population ya 700k tu unapotezq maana nzima mji take a look ukiwa nane nane bus terminal hadi mtu akushtue hapa ni makao makuu ndio uelewe pako kama porini flani ivi😀 si kwa ubaya but tujifunze hata kwa majirani zetu hapo kigali sasa badala yake nyie tena makao makuu mnabattle na miji ya ndani wakati nyie ndio mnapeperusha benders yetu tanzania 🇹🇿 mnachekesha sana😀😀 population yenyewe hamna mji hauko vibrant miti hampandi na nadhani tunaweza tukawa na mji mkuu wa hovyo sana kwenye ukanda wetu sina uhakika kama mtaweza hata kubattle na bujumbura 😥
 
Mbona unaruka ruka tu kubadili topics...nimeshakwambia population inapimwa kwa idadi ya watu sio eneo.Ukiulizwa leo taja majiji yenye watu wengi duniani utaangalia idadi ya watu au eneo la mji😀😀😀.
Alafu fact nyingine ni kwamba population wala sio kigezo cha kupima ubora wa mji...unaweza kuwa na mji una population kubwa lakini mipangomiji,miundombinu na huduma za kijamii ni mbovu na vilevile unaweza kuwa na mji una watu wachache na ukawa bora kuzidi wenye watu wengi.
Nakupa mfano Jiji la Luxembourg au Monaco City yana wakazi chini ya lakitano lakini kimaendeleo yamepita mbali sana majiji mengine yenye wakazi zaidi ya milioni mbili mfano Bucharest.
 
Are you sure?
 
Nyie shindaneni kwanza na bujumbura manake mnatutia aibu 😀😀 nyie ni mji mkuu mmepewa sapoti yote na serikali lakini bado hamuwezi kutuwakilisha kimataifa lazima mkubali Dodoma bado inajengwa haitafika inapotakiwa ndio maana hata viongozi wakubwa wakija watapelekwa dar second option itakua arusha
 
Dom ikue mara ngapi wakati inazidi hayo Majiji yenu yote takribani Kwa Kila kitu?
 
Kama Kuna mtu hajakuelewa bas ni kichaa
 
Dom ikue mara ngapi wakati inazidi hayo Majiji yenu yote takribani Kwa Kila kitu?
Hebu tuanze na idadi ya magorofa kisha majengo yaliyoko kwenye ujenzi, idadi ya watumiaji wa magari au lita za mafuta kisha njoo kwenye viwanda malizia na huduma za kijamii kama shule na hospitali bila kusahau hoteli tujue dodoma imezidi kwenye vingapi😀😀
 
Components ya Ukubwa wa Jiji ni mapato inayotengeneza full stop.

Hata ukileta wingi wa mafuta itaishia kuleta takwimu za Mkoa badala ya takwimu za Jiji.

Kwa hiyo Arusha Jiji Wana matumizi makubwa ya mafuta kushinda Jiji la Dodoma?
 
Naona tunabishana na mtu ambaye hajawahi kufika Dom 👇👇
-unazungumzia maghorofa Dodoma ...unajua idadi ya maghorofa yanayojengwa pale Magufuli City ,au City Centre au Tambukareli nyuma ya Jakaya Kikwete Convention Center
-Huduma za kijamii kama vyuo na hospitali,UDOM(Chuo kikubwa cha pili kwa ukubwa Afrika),St John's,CBE,IRDP,Chuo cha Madini
-Hospitali ...Benjamin Mkapa(Hospitali ya Rufaa ya Kanda),Mirembe(Hospitali ya taifa ya magonjwa ya akili),St Gemma,Aga Khan,DCMC-Ntyuka,DECCA,General
-Hotels....Bestern Western City Hotel(nyota tano),St Gaspar,Morena,Midlands,Royal Village,African Dreams,Dodoma Hotel,Nasheera,Karibu Rafiki n.k
-Viwanda...Kiwanda cha Mbolea,Kiwanda cha Magodoro,Viwanda vya Wine,Kiwanda cha nyama(vipo viwili kimoja cha Wachina na kingine kipo Kizota),Kiwanda cha vinywaji baridi DIPC n.k

Kama hujui kitu ni vizuri kuuliza kuliko kubishana kwenye kitu usichokijua
 
Endelea kujifariji tu.....Mwanza inazidi nini Dodoma zaidi ya population na viwanda vya samaki.Ebu tupe vigezo vya kupima ubora wa Mwanza tuone hiyo safari[emoji3][emoji3]
Nafikiri mada hii ni Dodoma na Arusha ila sijui ni Mwanza ipi hiyo unaongelea lakini kama ni hii ya Tanzania hapana nduguyangu Dodoma bado sana kwa Mwanza jiji.

Sent from my D6503 using JamiiForums mobile app
 
Nafikiri mada hii ni Dodoma na Arusha ila sijui ni Mwanza ipi hiyo unaongelea lakini kama ni hii ya Tanzania hapana nduguyangu Dodoma bado sana kwa Mwanza jiji.

Sent from my D6503 using JamiiForums mobile app
😀😀Bado sana kwa vigezo vipi ebu tutajie kama ni
-ubora wa mipango miji
-miundombinu
-huduma za kijamii
-uwepo wa ofisi na taasisi nyingi za serikali
🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…