Hebu tuanze na idadi ya magorofa kisha majengo yaliyoko kwenye ujenzi, idadi ya watumiaji wa magari au lita za mafuta kisha njoo kwenye viwanda malizia na huduma za kijamii kama shule na hospitali bila kusahau hoteli tujue dodoma imezidi kwenye vingapi😀😀
Naona tunabishana na mtu ambaye hajawahi kufika Dom 👇👇
-unazungumzia maghorofa Dodoma ...unajua idadi ya maghorofa yanayojengwa pale Magufuli City ,au City Centre au Tambukareli nyuma ya Jakaya Kikwete Convention Center
-Huduma za kijamii kama vyuo na hospitali,UDOM(Chuo kikubwa cha pili kwa ukubwa Afrika),St John's,CBE,IRDP,Chuo cha Madini
-Hospitali ...Benjamin Mkapa(Hospitali ya Rufaa ya Kanda),Mirembe(Hospitali ya taifa ya magonjwa ya akili),St Gemma,Aga Khan,DCMC-Ntyuka,DECCA,General
-Hotels....Bestern Western City Hotel(nyota tano),St Gaspar,Morena,Midlands,Royal Village,African Dreams,Dodoma Hotel,Nasheera,Karibu Rafiki n.k
-Viwanda...Kiwanda cha Mbolea,Kiwanda cha Magodoro,Viwanda vya Wine,Kiwanda cha nyama(vipo viwili kimoja cha Wachina na kingine kipo Kizota),Kiwanda cha vinywaji baridi DIPC n.k
Kama hujui kitu ni vizuri kuuliza kuliko kubishana kwenye kitu usichokijua