Dodoma imepangiliwa vizuri tena wakifanikiwa kujenga mabwawa ya maji huko Membe-Chamwino na Mvumi, Uwanja wa ndege Msalato, Uwanja wa Mpira hapo Nane nane na ring road road kukamilika hata Dar Es Salaam itasubiri sana kuipata. Arusha hali ya hewa yake ni nzuri lakini wakazi wake hawana nidhamu na utunzaji wa mazingira, tabia za kihuni na ubishi wa kijinga.
Serikali inatakiwa itengeneze mazingira mazuri zaidi ili miji kama Songea, Mtwara, Njombe, Kigoma Ujiji, Musoma iwe majiji bila kuisahau Tanga inawirishwe kurejea hadhi yake ya miaka 1970 hadi 1988 kulikuwa kumekucha balaa.
Miji inayokuwa kwa kutegemea nguvu za wananchi wenyewe bila kusaidiwa na serikali ni Mwanza, Morogoro, Singida, Simiyu na Kahama.
DODOMA kuko vizuri
1. UDOM (kijiji cha wasomi kuzunguka milima ya miamba)
2. Mpangilia wa ujenzi wa nyumba za kisasa unaridhisha ( barabara za kwenda Morogoro,, Arusha na Singida ni safi)
3. Magufuli Satellite City ni mfano mzuri wa miji ya kiserikali iliyojengwa kwa ubunifu wa kisasa na wazawa
4. Ikulu bora
5. Utulivu wa wenyeji wa jamii ya Kigogo (sio Warangi)
NB: Wilaya za Dodoma mjini, Mpwapwa na Kondoa ndio kongwe kuliko wilaya zingine ambapo zilianzishwa na wakoloni kabla ya uhuru kati ya 1913-1950
1. Wlaya ya Dodoma mjini ilianzishwa mwaka 1950 na ikatambulika kiserikali mwaka 1955
2. Wilaya ya Mpwapwa ilianzishwa mwaka 1929 lakini ikatambulika kiserikali mwaka 1952
3. Wilaya ya Kondoa ilianzishwa na Wajerumani mwaka 1916 lakini ikatambulika kiserikali mwaka 1926
4. Wilaya ya Kongwa ilianzishwa na Wajerumani mwaka 1947 kwa ajili ya kushughulika na mradi mkubwa za kilimo cha karanga lakini utawala uliowekwa wa mtemi Kalihinya ulishindwa kutimiza malengo ikafutwa na wakoloni mwaka 1949
Kasoro/Mapungufu
1. Ujenzi wa nyumba barabara ya Iringa hauridhishi
2. Barabara ya Dom-Moro kupitia majengo ya bunge haifai kwa sasa maana ni nyembamba inatakiwa iwe njia sita kuanzia bunge hadi Chamwino, Dom-Singida na Dom-Arusha kupitia Msalato barabara zinatakiwa kuwa njia nne
3. Bustani ya Nyerere Square inatakiwa iwekewe mfumo wa maji yanayoruka kama mvua ili kupoza hali ya hewa wakati wananchi wanapumzika hapo
4. Stendi ya daladala hapo Sabasaba ijengwe ya kisasa , pembeni yake zijengwe fremu za kupangisha wajasiriamali na miundo mbinu ya mifereji na mazingira viboreshwe
5. Fly over bridge zijengwe maeneo ya Nzuguni-Stendi ya Ndugai, Round about ya CDA, Mataa ya Chako ni Chako, eneo la bunge njia panda ya kwenda Ikulu Chamwino
6. Ukosefu wa bwawa kubwa lililopandwa miti kuzunguka ambalo litatumika kufanikisha mambo mbalimbali mtambuka kama chanzo cha maji, uhifadhi wa uoto, kupumzika na ku-refesh mind wakati mwisho wa wiki au mapumziko ya kitaifa
7. Ukosefu wa makumbusho wa tamaduni za Wagogo, Warangi na harakati za kutafuta uhuru hayatakiwi yawekwe kwenye ofisi za CCM (Chanzo cha kukua mji wa Idodomya ilianza kipindi cha biashara ya utumwa kabla na baada ya mwaka 1910 ambapo ndipo shughuli za ujenzi wa reli ya kati ulipita hapo chini ya Wajerumani
8 Hamasa ya utalii bado ndogo sana ukiwa jijini Dodoma
9. Inatakiwa kujengwa ICD kubwa Dodoma kwa hifadhi ya mizigo ya kutoka badarini ili kurahisisha uchukuaji na usambazaji kwenda mikoa inayopakana nayo kama Singida, Manyara, Arusha, Iringa nk