Dodoma hapakaliki, Watu wa Jiji wanafunga biashara za Watu kisa Service Levy

Dodoma hapakaliki, Watu wa Jiji wanafunga biashara za Watu kisa Service Levy

Sijakataa kulipa Kodi lakini, kwani ni lazima waje wakufungie? Si wangeweka mfumo kwamba maybe hupati leseni Hadi ulipie service levy? Hii kufungiana makufuli ni uswahili. Huku ni kuendesha nchi kiswahili. Na siyo kisomi.

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
haya mambo ya fungia biashara si yalishakatazwa au mimi ndio nimesahau?
 
Shida ni hatujawakazia kushusha matumizi ya serikali. Hizi kodi wanazokusanya ndizo zinakwenda kuweka yale mafuta wanayochezea kwa kuzunguka zunguka hovyo na magari bila utaratibu, kulipa watu posho zisizo na kichwa wala miguu.

Kwa ufupi hawa jamaa tunatakiwa kuwanyoosha.
 
Kuna sheria ya kodi; kulipa kodi ni wajibu wa raia, siyo shukurani kwa serikali.

Anzisha biashara yako mwenyewe, tafuta mbinu zao za kuuuza na kupata faida, lakini lazima uilipe serikali kodi yake.
kwa hiyo usiilaumu serikali kwa kukudai kodi yao.

Lalamikia tu utaratibu wa jinsi wanavyodai kodi lakini siyo kwa kukudai kodi hiyo.
Kodi kulipa ni lazima ila haidaiwi kwa nguvu na lazima. Mtu kama hajalipa kodi unatakiwa kumpeleka mahakamani huko sasa ndipo majadiliano yakafanyike sio unamfungia biashara huko ni kuhujumu uchumi kwa kutumia mamlaka halali ya serikali.
 
Kodi kulipa ni lazima ila haidaiwi kwa nguvu na lazima. Mtu kama hajalipa kodi unatakiwa kumpeleka mahakamani huko sasa ndipo majadiliano yakafanyike sio unamfungia biashara huko ni kuhujumu uchumi kwa kutumia mamlaka halali ya serikali.
Sidhani kama post hii kweli inajibu hiyo uliyokwoti. Hata hivyo Elewa pia kuwa kupelekwa mahakamani ni process ya nguvu na lazima, siyo ya kubembelezwa. Serikali haimbembelezi raia kulipa kodi.
 
Nchi ya ovyo utaijua tu. Serikali haijakusaidia kufungua biashara, haijakupa mkopo, haijakupa ujuzi namna ya kufungua biashara. Haijakufundisha namna ya kutengeneza product iendane na soko la kimataifa. Haijawasaidieni muweze hata kupeleka bidhaa zenu soko la kimataifa. Ila wanakuja na makufuli wanakufungia biashara Yako.

Ndo maana watu wanawarecord wanamtumia Mange Kimambi kuonesha upuuzi mnaoufanya .

Hivi hamna organization iliyoko huko duniani ili tuwatumie video jinsi Tanzania tunavyonyanyasika?

Serikali zinakusanya zisipotapanya. Mnavuna mapato ambayo hata hamjayahangaikia . Nchi ya ovyo hii. Loh .
Pole sana kwahiyo ulitaka ufanye biashara bila kulipa kodi,au hoja yako ni nini hasa mana unalialia tu utadhani ndio umefka leo tz.
 
utafanyaje sasa.. huwezi kushindana na wenye mamlaka .. Lipa kodi maisha yaendelee hakuna cha huruma!
 
Kwanza wapigaje hesabu mpaka kujua kua mm natakiwa kulipa kiasi flan Cha pesa kwa ajili ya hiyo service Levy
 
dodoma hovyo, airport pana camera lakini askari wa jkt getini hupokea rushwa za vijana wa bodaboda wanaowapeleka abiria pale, elfu moja moja wanatia mfukoni. Yaani vijana na abiria wao wengine abiria wa kigeni kabisa wanaona ujinga huu, huko madukani nako balaa nasikia
 
Back
Top Bottom