Dodoma hapakaliki, Watu wa Jiji wanafunga biashara za Watu kisa Service Levy

haya mambo ya fungia biashara si yalishakatazwa au mimi ndio nimesahau?
 
Shida ni hatujawakazia kushusha matumizi ya serikali. Hizi kodi wanazokusanya ndizo zinakwenda kuweka yale mafuta wanayochezea kwa kuzunguka zunguka hovyo na magari bila utaratibu, kulipa watu posho zisizo na kichwa wala miguu.

Kwa ufupi hawa jamaa tunatakiwa kuwanyoosha.
 
Kodi kulipa ni lazima ila haidaiwi kwa nguvu na lazima. Mtu kama hajalipa kodi unatakiwa kumpeleka mahakamani huko sasa ndipo majadiliano yakafanyike sio unamfungia biashara huko ni kuhujumu uchumi kwa kutumia mamlaka halali ya serikali.
 
Kodi kulipa ni lazima ila haidaiwi kwa nguvu na lazima. Mtu kama hajalipa kodi unatakiwa kumpeleka mahakamani huko sasa ndipo majadiliano yakafanyike sio unamfungia biashara huko ni kuhujumu uchumi kwa kutumia mamlaka halali ya serikali.
Sidhani kama post hii kweli inajibu hiyo uliyokwoti. Hata hivyo Elewa pia kuwa kupelekwa mahakamani ni process ya nguvu na lazima, siyo ya kubembelezwa. Serikali haimbembelezi raia kulipa kodi.
 
Pole sana kwahiyo ulitaka ufanye biashara bila kulipa kodi,au hoja yako ni nini hasa mana unalialia tu utadhani ndio umefka leo tz.
 
utafanyaje sasa.. huwezi kushindana na wenye mamlaka .. Lipa kodi maisha yaendelee hakuna cha huruma!
 
Kwanza wapigaje hesabu mpaka kujua kua mm natakiwa kulipa kiasi flan Cha pesa kwa ajili ya hiyo service Levy
 
dodoma hovyo, airport pana camera lakini askari wa jkt getini hupokea rushwa za vijana wa bodaboda wanaowapeleka abiria pale, elfu moja moja wanatia mfukoni. Yaani vijana na abiria wao wengine abiria wa kigeni kabisa wanaona ujinga huu, huko madukani nako balaa nasikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…