VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Kufuatia kinachoendelea hapa Bungeni Dodoma,Wajumbe mbalimbali wameingiwa na hofu kuu juu ya mambo fulanifulani. Wajumbe hao-hasa wenye mafungamano na CCM wameonesha hofu juu ya usalama wao na uanachama wao ndani ya chama hicho kwakuwa viongozi wa chama husika wameanza kutumia 'ubabe' kuwadhibiti Wajumbe hao. Wajumbe hao wanadai kuwa kwasasa hawako huru ingawa wana mtazamo tofauti juu ya kilicholikwamisha Bunge kwasasa: kura ya SIRI au DHAHIRI?
"Wewe acha tu.Wengine tunatamani tujiuzulu na kurudi majimboni mwetu. Hapa tunalazimishana kama wanafunzi wa Shule za Msingi. Hatutuko huru kabisa ingawa baadhi yetu hatuoni tatizo la kura ya siri. Ndiyo tuliyoizoea katika kupata uamuzi mkubwa hapa nchini. Lakini,nani atajitokeza kusema hivyo hadharani?" alisema Mjumbe mmoja machachari kutoka Nyanda za Juu
"Wengine walijaribu kuonesha tofauti ya kimtazamo kwenye Party Caucus na wakaishia kutishwa na meza kuu. Hali hapa ni tete. Sisi tunang'ang'ania DHAHIRI;wengine wote SIRI. Kimahesabu,bado hakuna mshindi. Mvutano huu waweza kuendelea kwa muda mrefu bila ya upande mmoja kujirekebisha.Na kimsingi,msimamo wetu kama CCM ni butu na batili.Watanzania wataendelea kutuvumilia kwa muda gani?" aliongeza Mjumbe huyo aliyewahi kupokea vitisho vya kichama kwa misimamo yake
Mzee Tupatupa wa Lumumba (sasa Dodoma)