Lamborgini
JF-Expert Member
- Nov 28, 2024
- 954
- 1,617
Kwa Nini Dar es Salaam Inaonekana Kama “Imeshafeli” kuwa jiji la kisasa(world class city) dar inaachwa mbali kiubora,mpangilio na miji kama windhoek(namibia) na gaborone(botswana) sababu ya mipango mibovu na kutokuwa na udhibiti wa ujenzi.
1. Miji Imejaa Kupita Kiasi
Mamilioni ya watu (zaidi ya milioni 6) wanaingia mjini kila siku bila mipango bora.
Ukosefu wa nyumba bora umezalisha makazi holela (kwa mfano: Mbagala, Buguruni, Kinondoni za pembezoni),wazee wa manzese ndo balaa,kinachosikitisha ni kwamba hata maeneo yaliyowazi sasa bado yanaendelea kujengwa hovyo kama kigamboni,mbezi.
2. Barabara Zinazidiwa na Magari
Traffic imekuwa kero ya taifa. Hata DART (BRT) haikutosha.
Kukosekana kwa barabara mbadala (feeder roads), flyovers za kutosha, au metro, yani dar kuna boda wengi hadi kero halafu wanapita kwenye njia za watembea kwa miguu.
3. Usafi na Maji Taka
Majitaka huingia baharini bila kusafishwa.
Mifereji imejaa takataka, maji ya mvua hayana njia ya uhakika, hivyo mafuriko kila mvua, yani mpk karne hii bado wanajenga mirereji ya wazi ndani ya jiji, hii inapelekea utupaji taka mpk inaziba.
4. Miundombinu Haiendani na Ukuaji
Umeme wa umma, maji, mitandao haviwiani na watu wanaoongezeka kila mwaka.
Miji inaongezeka lakini miundombinu haipanuki, nyaya za umeme zimejazana pana kariakoo cjui ikitokea hitilafu wanatengeneza vipi.
Yani bongo mambo yanafanyika kizamani sn kama hatuna wataalamu, kiukweli suala la mipango miji ni janga la taifa tumezidiwa hata na rwanda.
Dodoma – Tumaini Mpya?
Dodoma bado iko kwenye hatua ya kujengwa kimiundombinu, serikali inanafasi kubwa ya kurekebisha makosa yaliyotokea dsm yasijirudie dodoma, haya ndio nnayoona.
1. Fursa ya Kupanga Upya Mji
Dodoma ni greenfield city yaani mji unaopangwa toka chini(from scratch) ni rahisi kupanga mji sababu maeneo mengi yapo wazi
Serikali imeanza kujenga barabara kubwa kama inner na outer ring road, majengo ya kisasa kwenye mji serekali na NNC link kwa ajili ya taasisi za umma, kiwanja cha ndege msalato kikiwa na barabara pana za kuingia pamoja na sehemu ya tram iliyotengwa n.k.
2. Idadi ya Watu Bado Ni Dogo (ikilinganishwa na Dar)
Hii ni nafasi nzuri kujenga kabla ya matatizo ya msongamano kuanza.
3. Serikali Inakaa Huko Umakini Upo
Kwa kuwa viongozi wakuu wapo Dodoma, miundombinu mingi ya kisasa inaelekezwa huko hospitali kubwa, barabara, uwanja mpya wa ndege, nk.
Dodoma itakuja kuwa bora sana kama mipango yote itatekelezwa.