Dodoma: Kofia mbili kuchomoza mabadiliko CCM

VITUKO CCM:
Kata anayoishi Mwenyekiti wa ccm Mkoa wa Kilimanjaro haina Ofisi ya ccm ya Tawi Hata moja wala haina Ofisi ya ccm kata.

Pili kata anayotokea mbunge wa ccm jimbo la Moshi mjini kule Kilimanjaro Hakuna Ofisi ya ccm Kata.

Ni Lini uliwahi kusikia kuna sherehe ya uzinduzi wa Ofisi ya ccm kata?
 
Kilimanjaro watu hawataki kuiona CCM hata kwa macho tu achilia mbali ofisi
 
CCM chama tawala hakina uwezo wa kuandaa kabrasha lenye maelekezo muhimu ya kufanyiwa kazi na makatibu wake wa mikoa na kuwafikishia walitumie kupitia njia mbalimbali za mawasiliano? Wanataka waje ndani ya vikao ili wasikie kwa masikio yao.Daah!
 
CCM chama tawala hakina uwezo wa kuandaa kabrasha lenye maelekezo muhimu ya kufanyiwa kazi na makatibu wake wa mikoa na kuwafikishia walitumie kupitia njia mbalimbali za mawasiliano? Wanataka waje ndani ya vikao ili hasikie kwa masikio yao.Daah!
Hawawezi kusikia kwenye tv au kuona?
 
Wanataka kurudisha ajira 170 wamesahau mishahara kipindi hicho walikuwa wanachangisha kutoka kwa wahindi na waburushi. Wenye akili kubwa ambao waliiwezesha CCM kuwa na fedha za kujiendesha wenyewe waliona hizo ajira ni za kujidurufu. Umaarufu wa kutaka kujipendekeza kwa watu huwa tabia yake ni kukulipa kwa kitambo kidogo sana.
 
Kofia mbili tuseme kuanzia Mwenyekiti wa CCM Taifa asiwe pia Rais wa nchi siyo !! ama ?

Kama hivi ndivyo basi haya yatakuwa mabadiliko makubwa mno ndani ya chama chetu, sijui yamesukumwa na nini? yaani why now ?
Mkuu Fuso, wana maana kuwa mgombea Rais wa CCM itakapo tokea amechaguliwa kuwa RAIS wa Nchi basi ile siku anaapishwa tu apewe na cheo/nadaraka yake ya kuwa Mwenyekiti wa Chama cha CCM, maana kwa utaratibu wa sasa, Rais anayemaliza muda wake huwa amebakiza miaka 2 ya uwenyekiti wake na hivyo kulazimika kujiuzuru mwaka mmoja kabla na kumkabidhi kofia hiyo Rais Mteule awe na kofia mbili akisubili kukabidhiwa rasmi na Mkutano Mkuu wa Chama.

Kwa maoni yangu, muda umefika sasa wakutenganisha kofia mbili. Ukizingatia kuwa Kazi za Rais ni nyingi sana na hasa ukizingatia kuwa leo shughuli za SERIKALI ZA MITAA (LOCAL GOVERMENT) kwa asilimia kubwa inashughulikiwa na CENTRAL GOVERMENT jambo ambalo zamani hai
kuwa hivyo. CCM isiogope kutenganisha kofia mbili. Tuna iomba sana ITENGANISHE KOFIA MBILI KWA MAENDELEO YA NCHI NA WATU WAKE.
 
Mkuu kwa hiyo leo Ramphosa ana kofia mbili?
 
Ili ccm ibakie salama kofia mbili zitenganishwe. Mwenyekiti asiwe na nguvu kuliko wanachama
 
Reactions: Ame
Kama Katiba ya nchi yetu ilivyo ni ngumu kubadilishwa na Rais aliyeko madarakani vivyo hivyo kwa mwenyekiti wa CCM taifa ilivyo ngumu kukubali hoja ya kutenganisha uwenyekiti wake na Urais.

Mwalimu alituachia mzigo mkubwa mno, nafikiri kabla hajaamua kung'atuka angetupatia katiba mpya kwanza..hii kitu itatusesa sana..wengi watakufa, watakuwa vilema, watqfirisika hadi katiba mpya inaoatikana.

Vita bado ni mbichi.
 
Mkuu ni kweli Mwalimu ametuacha njia panda, maana alisema kwa sasa Rais ana kofia mbili lakini kuna hatari kama inaweza kupata Rais katili na akawa na kofia mbili, nchi itapata shida, hivyo ni vyema tukafikiria namna ya kuondoa kofia mbili
 
Mkuu ni kweli Mwalimu ametuacha njia panda, maana alisema kwa sasa Rais ana kofia mbili lakini kuna hatari kama inaweza kupata Rais katili na akawa na kofia mbili, nchi itapata shida, hivyo ni vyema tukafikiria namna ya kuondoa kofia mbili
 
Reactions: Ame
Mtu anaweza kuwaza, wanawarudisha hao kwakua ni wateuliwa kwahiyo wanauwezo wa kupewa maelekezo na wakayatekeleza kwakua wakikataa wanatenguliwa teuzi zao...Mungu saidia nchi yangu...:"CCM dhaifu itazaa serikali dhaifu" wosia wa baba!
 
Kwahili nakubaliana na wewe...Mwl alikuwa na dhamira njema ili nchi isijeikaingia mikononi mwa maadui na viongozi wakashindwa kudhibiti raia wengi ambao ni masikini na ambao hawana uelewa wakutosha, tatizo ni akina sisi maslahi binafsi kupitia kichaka cha maslahi ya taifa. Kuna watu historia itawahukumu kwakujali mambo yao binafsi kuliko ya wananchi
 
Kofia mbili tatizo lake ni kuwa inaondoa wengi kwenye maamuzi na kufanya wachache kudhibiti wenzao huku wao wakiweza kusukuma agenda zao binafsi. Sijui kwanini watanzania tunakuwa wabinafsi hivi!
 
Ni vizuri kusoma na kuelewa ndipo tuandike au tujibu. Hakuna kokote paliposemwa kuondolewa kofia mbili. Kofia mbili zinarudi, lakini kutegemea nafasi. Sasa hivi mwenyekiti wa chama (taifa) hatapigiwa kura tena. Atakuwa mwenyekiti kwa sababu ya nafasi yake. Ina maana raisi akimaliza muda wake, akifariki, au kuacha uraisi kwa sababu yoyote, yule anayechukuwa nafasi yake anakuwa automatically mwenyekiti wa chama (taifa) bila kuita kikao cha kumchagua/kumuidhinisha.
 
Hilo ndio dhumuni kubwa ili fomu ya kugombea 2025 ichapishwe moja tu!! Yule bibi anaweweseka ndani na nje ya chama chake.
Kofia mbili tuseme kuanzia Mwenyekiti wa CCM Taifa asiwe pia Rais wa nchi siyo !! ama ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…