Mchaga Tajiri
Member
- Mar 14, 2023
- 10
- 16
Dodoma kuna shida ya upatikanaji wa hati miliki za ardhi. Mtu anakuwa amemaliza kulipia kiwanja na kufuata hatua zote zinahitajika lakini linapofika suala la kupewa hati ni mtihani.
Wapo wananchi ambao wamemaliza kulipia viwanja vyao kwa takribani miaka minne sasa, lakini hadi sasa hawajapatiwa hati za viwanja.
Mwananchi mmoja ambaye alikuwa akifuatilia hati yake kwa miaka kadhaa, baada ya kumaliza kulipa aliambiwa ndani ya siku 14 hati yake itakuwa tayari lakini baada ya kurudi kwa siku 14 alizoambiwa hakuipata hati hiyo.
Alikaa kwa muda akarudi tena kufuatilia, alipofika akaambiwa kwamba kuna malipo hajamaliza, uzuri alikuwa na stakabadhi zake zote alipoonyesha ndipo file lake likaletwa ili kufuatilia hati hiyo.
Pamoja na kuambiwa arudi tena kufuatilia hati yake mpaka sasa hajapata hati hiyo, lakini wapo wananchi wanaopata hati hizo kwa haraka tofauti na watu wengine.
Siku zote Serikali inasisitiza umuhimu wa wananchi kupata hati za ardhi mapema, lakini inapokuja suala la utendaji baadhi ya watendaji wake hawatekelezi kwa ukamilifu majukumu yao.