johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Askari Polisi wawili wameuawa huko Mpwapwa baada ya kutokea majibizano ya Risasi Kati ya Polisi na Mtuhumiwa
Mtuhumiwa huyo Athanasia Malenda naye ameuawa.
---
Askari Polisi wawili wamefariki dunia wakati wakifanya majibizano ya risasi na Mtuhumiwa Atanasio Malenda (30) ambaye walienda kumkamata usiku wa kuamkia leo December 18,2024 katika Kijiji cha Msagali Wilaya ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma ambapo Mtuhumiwa huyo pia amefariki baada ya majibizano hayo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, George Katabazi amesema “December 18,2024 majira ya saa saba usiku huko katika Kijiji cha Msagali Wilaya ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma Askari Polisi D/Cpl. Jairo Boniface Kalanda na Pc. Alfred John walifariki dunia katika mapambano ya risasi wakati wakimkamata Atanasio Malenda (30), Mkulima, Mkazi wa kijiji cha Msagali aliyekuwa anatuhumiwa kwa tuhuma za unyang’anyi wa kutumia silaha ambapo alilkuwa amemjeruhi Yohana Lameck na kumpora kiasi cha Tsh. milioni “
“Askari Polisi hao wakiwa na wenzao walipata taarifa kuwa Mtuhumiwa huyo aliyekuwa anatafutwa yuko nyumbani kwake katika Kijiji Cha Msagali na walifika Kijijini hapo na kutafuta Uongozi wa Kijiji na kuelekea nao nyumbani kwa Mtuhumiwa huyo ambapo Mtuhumiwa huyo alitoka ndani na kuanza kuwashambulia Askari na katika majibizano hayo ndipo vikatokea vifo hivyo”
“Mtuhumiwa Atanasio Maleda nae amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya Wilata ya Mpwapwa kutokana na majeraha aliyoyapata wakati wa mapambano hayo, aidha katika majibizano hayo Askari D/cpl. Msuka na Raia mmoja anayefahamika kwa jina la Masima Nyau wamejeruhiwa na wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa”
Source: Ayo TV
Inasikitisha sana 🐼