NewChapter
JF-Expert Member
- May 17, 2024
- 306
- 196
Mbunge wa Mvomero, Mhe. Sara Msafiri, amehoji utekelezaji wa maelekezo ya Serikali na Bunge kuhusu miradi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), akibainisha kuwa licha ya kuelekezwa kwa kila mamlaka ya serikali kuandaa angalau mradi 1 wa PPP na kila halmashauri kuandaa angalau miradi 3, bado utekelezaji wake hauonekani.
Mhe. Msafiri amesema hali hiyo inatia wasiwasi kwa kuwa takribani asilimia 70 ya gharama za utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo zinatarajiwa kutoka sekta binafsi, huku PPP ikitajwa kuwa nyenzo muhimu ya kufikia lengo la uchumi wa Dola Trilioni 1.
"Mpango huu hauwezi kutegemea mikopo na bajeti ya ndani ya Serikali pekee. Kama sekta binafsi itachangia asilimia 70 ya utekelezaji, basi maandalizi ya miradi ya PPP yanapaswa kupewa kipaumbele," alisema.
Pia amehoji kwa nini taasisi za Serikali zinapata fedha za kuandaa miradi inayotegemea mikopo na kodi za Serikali, lakini hazionekani kutenga fedha kwa ajili ya kuandaa miradi ya PPP.
Mbunge huyo alimpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo SGR, maboresho ya bandari na miradi mingine ya maendeleo, lakini akasema baadhi ya taasisi za Serikali bado hazijaendana na kasi ya mabadiliko hayo.
Aidha, ameibua changamoto ya nyumba za watumishi akieleza kuwa licha ya Serikali kujenga vituo vya afya, zahanati, shule na ofisi za kisasa, bado halmashauri nyingi zenye maelfu ya watumishi zinakabiliwa na upungufu wa makazi.
Mhe. Msafiri ametaka Serikali kueleza kwa nini miradi ya nyumba za watumishi isitekelezwe kupitia PPP, akisisitiza kuwa kama sekta binafsi inatarajiwa kuchangia asilimia 70 ya utekelezaji wa mpango wa maendeleo, basi miradi hiyo inapaswa kuwa sehemu ya fursa za uwekezaji kupitia mfumo huo.
View: https://www.instagram.com/reel/DfFxJPSgTE7/?psln=eThyMzAzMHhidm9v
#PPP #PPP_CENTRE #Uwekezaji #Maendeleo