Dodoma: Mbunge aomba uanzishwe mtaala wa Utajiri mashuleni

Dodoma: Mbunge aomba uanzishwe mtaala wa Utajiri mashuleni

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Mbunge wa Ngara ameiomba serikali kuanzisha mtaala mpya wa Utajiri mashuleni ili kuwezesha Wahitimu kuwa na ari ya uwekezaji wanapomaliza masomo yao , amesema jambo hilo ni muhimu likafanyika ili kuleta akili mpya vichwani mwa watu na kuondoa ile dhana kwamba kila Tajiri ni fisadi .

Ameshangaa sana kuona nchi hii hakuna Waziri hata mmoja anayemiliki ndege binafsi , kwa madai kwamba wote wanaogopa kuitwa Mafisadi .

Toa maoni yako .
 
Mbunge wa Ngara ameiomba serikali kuanzisha mtaala mpya wa Utajiri mashuleni ili kuwezesha Wahitimu kuwa na ari ya uwekezaji wanapomaliza masomo yao , amesema jambo hilo ni muhimu likafanyika ili kuleta akili mpya vichwani mwa watu na kuondoa ile dhana kwamba kila Tajiri ni fisadi .

Ameshangaa sana kuona nchi hii hakuna Waziri hata mkoja anayemiliki ndege binafsi , kwa madai kwamba wote wanaogopa kuitwa Mafisadi .

Toa maoni yako .
Naunga mkono hoja
 
Jamaa anaakili sana

USSR
 
Upuuzi mtupu.

Hilo somo litafundishwa na nani? Litafundishwa na hawa walimu maskini walioshindwa kuondoa umaskini wao, viongozi na watendaji wa Serikali waliopata utajiri kwa kuiba pesa ya umma au wataombwa watu wenye utajiri halali kama akina Bakhresa?
 
Utajiri unapatikana wapi ?

Bungeni, Kwenye Siasa au Kitaa..., Kama ni huku kitaa, aachane na huo Ubunge aje kitaa aanzishe shamba Darasa (Bodaboda, Baba /Mama Lishe, au Apatiwe Bidhaa atembeze kitaa) bila kusahau Tozo na unpredictability ya Soko la Bidhaa zake....

By the way kama Utajiri ndio destination na unafundishwa kama ABC, Basi waalimu wote wangekuwa Ndio Matajiri....

Bure kabisa wameshindwa kuweka opportunities za watu kupata basic needs kwa uhakika let alone utajiri alafu wanaleta hadithi za kufikirika hapa.....
 
Naunga mkono hoja though UTAJIRI ni neno pana,angesema tufundishwe elimu ya kujiari,usimamizi na udhibiti wa fedha,hati fungani na hisa..

Nadhani tunalo la kujifunza toka kwa wenzetu wenye asili ya INDIA
Kwa mtazamo wako mkuu ilipaswa kuwa hivyo maana neno Utajiri ni pana sana. Elimu itolewe juu ya Biashara na uwekezaji kuanzia ngazi ndogo ya Ujasiriamali hadi kufikia uwekezaji mkubwa.
 
Kwa mtazamo wako mkuu ilipaswa kuwa hivyo maana neno Utajiri ni pana sana. Elimu itolewe juu ya Biashara na uwekezaji kuanzia ngazi ndogo ya Ujasiriamali hadi kufikia uwekezaji mkubwa.
Duuuh
 
Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe. Ndaisaba George Ruhoro ameitaka Serikali kuanzisha mtaala unaohamasisha utajiri kwa Wanafunzi ili wanapomaliza elimu yao wawe wameshazijua fursa za uwekezaji na waondokane na dhana ya kuamini kila tajiri ni fisadi au kuhisi ni Freemanson.

Mhe. Ruhoro amesema hayo wakati akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi katika Ofisi ya Rais Ikulu na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2023/23 iliyoomba Bunge kupitisha kiasi cha shilingi Trilioni 1.

“Imefika mahali kwenye Taifa letu Watanzania wanaishi kwa uoga nilitarajia kwenye Taifa letu tuwe na Mawaziri wanamiliki ndege ila hatuna, ni waoga sasa matokeo yake tunajinyima fursa, mtu akiwa tajiri anaonekana ni Fisadi au Freemanson.”

WhatsApp Image 2023-04-20 at 18.06.36(2).jpeg

Mwambie huo ujinga anaongea Muda huu ajue kuwa 2025 asije kuanza kulalamika hatuwezi mtuma mtu bungeni then anaanza kuongea pumba wakati anaona Nchi yetu imekwama inahitaji maboresho makubwa .yeye anabwatuka Kama mlevi .
 
Bakhressa anayewalipa watu elfu 3?
Upuuzi mtupu.

Hilo somo litafundishwa na nani? Litafundishwa na hawa walimu maskini walioshindwa kuondoa umaskini wao, viongozi na watendaji wa Serikali waliopata utajiri kwa kuiba pesa ya umma au wataombwa watu wenye utajiri halali kama akina Bakhresa?
 
Huo ndiyo ukweli wenyewe wenye dhamana kama wanaandaa mitaala ya kukidhi soko la ajira inatarajia nini. Nchi INA kila kitu lakini watu wake waoga kama nini kuchukua hatua kutwa kuzunguka na vbahasha vya kaki kutafuta hisani ya kazi. Hayo ni matokeo ya wenye dhamana kuelimishwa hivyo kutegemea hao kuleta mabadiliko ya mitaala Bora haitatokea asilani. Jambo hili napendekeza uwepo mjadara huru ni njia ipi itumike kuelimishwa watoto wetu suala hili ni nyeti kuliko watu wanavyo lichukilia kuzungumza elimu.na ajira ni mzaha na kukosa jibu la msingi. Hakuna nchi duniani iliyo endelea Kwa kuelimishwa watu wake umanamba. Wazo la mbunge naliunga mkono shikilia hapo muwakilishi wetu
 
Jambo jema. Watu wafundishwe biashara halisi za kitaa zinavyoenda, kutunza pesa, kupanga bajeti, mikopo, malipo, leseni, kuuuza na kuagiza, kujitangaza, logistics, kukwepa kodi, kulipa kodi, biashara za kuexport, kuimpor nk nk. Waachane na "commerce is the study which deals with...."
 
Ebu atutajie matajiri halali walioko Tanzania?
Maana wale wapuuzi wa hivi majuzi mtakimbilia kusema ni AZAM.....

Wakati kiuhalisia AZAM iliinunua National Milling Corporations kwa hila,tena hata tunayo kumbukumbu ya ule mchele bandia wa AZAM Zanzibar ulivyotuondolea mwandishi wetu Nguli Stan Katabalo wa gazeti la Mfanyakazi!

Huyo mbunge tajwa ni mmojawapo wa waliowahi kuhojiwa na TAKUKURU huko nyuma.

Anachotafuta ni kuhalalishwa kwa fedha za kifisadi wanazoiba huko serikalini.anashangaa waziri kutokuwa na ndege nchini.

Hivi hawa mawaziri wa Tanzania wenhi wao si ndio hawa hawa mafisadi wanaotajwa na CAG kila uchao?

2025 utawasikia bila aibu oooh tuko bega kwa bega na wananchi!

F**kny kabisaa!
 
Wataalam wengi wanaishia kuongea misamiati ambayo hawajawahi kuexperience.
Ni usanii tu umejaa.
 
Back
Top Bottom