Dodoma: Mtoto wa miaka minne akutwa amefariki baada ya kukatwa mkono na sehemu za siri

Dodoma: Mtoto wa miaka minne akutwa amefariki baada ya kukatwa mkono na sehemu za siri

Dah! My God! Kwa hiyo sasa wasiojulika waendelee tuuu?? Ni ruksa?
Kama hao tuliotegemea ndo kazi yao na wanawalipwa kwa kodi zetu majibu yao ndo hayo, basi tumekwisha. Wazazi fungieni watoto ndani au mlale nao chumba kimoja mkiwa na rungu, panga au mkuki.
Tena wamesema wanamtafuta aliyeeneza hizo habari za uongo
 
kwa matukio haya yanayoendelea juu ya mauaji ya namna hii na wahanga kunyofolewa viungo tulitegemea jeshi letu la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama viwe vimewapata hao culprits wenye kufanya matendo haya ya kinyama lakini sioni matumaini yeyote.
 
Dodoma.
Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi wa tukio la mwili mtoto, Telesphore Mwakalinga (4) aliyeokotwa usiku wa kuamkia leo Alhamisi, Julai 18, 2024 eneo la nyumba 300, Kisasa jijini Dodoma akiwa hana mkono na sehemu za siri.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Theopista Mallya amesema tukio hilo lilitokea jana Jumatano usiku kwenye nyumba 300 zilizopo Kisasa jijini Dodoma.
“Jana askari polisi akiwa katika eneo hilo aliona mbwa akiwa na kitu, jambo ambalo lilimfanya kusogelea karibu na kumuona mtoto huyo. Alitoa taarifa polisi ambao walikwenda kwenye tukio na kumpeleka hospitali,” amesema.

Amesema kwa sasa hivi hawawezi kusema mtoto huyo aliuawa ama vinginevyo hadi hapo watakapopata uhalisi wa tukio hilo baada ya uchunguzi kukamilika.

“Siwezi kusema ameuawa hadi tutakapokamilisha uchunguzi wa tukio hilo yakiwemo mazingira ya tukio lenyewe ikiwa aliondokaje nyumbani,” amesema kamanda huyo.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali kutoka katika eneo hilo, mtoto huyo alipotea jana jioni saa 12.00 jioni lakini alipatikana saa 4.00 usiku, akiwa hana mkono mmoja na sehemu za siri katika eneo hilo la nyumba 300 za Kisasa jijini Dodoma.

Kamanda Theopista amesema mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

©Mwananchi
 
Mtoto wa miaka minne jinsi ya kiume amekutwa ametekelezwa nyuma ya nyumba kwenye makazi ya watu Kisasa majumba 300 baada ya kukatwa mkono wa kulia na sehemu za siri na watu wasiojulikana na kutokomea navyo kusikofahamika.

Siku kadhaa hapo nyuma yameshatukia matukio kama haya mawili ambayo nimeyasikia.

Hii taarifa nimeipata kwa moja wa jirani wa wazazi wa mtoto aliyetendewa kitendo hicho cha kikatili na kupelekea umauti wa mtoto huyo.

Swali ni; upo wapi usalama wa raia?

=====

Dodoma.
Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi wa tukio la mwili mtoto, Telesphore Mwakalinga (4) aliyeokotwa usiku wa kuamkia leo Alhamisi, Julai 18, 2024 eneo la nyumba 300, Kisasa jijini Dodoma akiwa hana mkono na sehemu za siri.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Theopista Mallya amesema tukio hilo lilitokea jana Jumatano usiku kwenye nyumba 300 zilizopo Kisasa jijini Dodoma.

“Jana askari polisi akiwa katika eneo hilo aliona mbwa akiwa na kitu, jambo ambalo lilimfanya kusogelea karibu na kumuona mtoto huyo. Alitoa taarifa polisi ambao walikwenda kwenye tukio na kumpeleka hospitali,” amesema.

Amesema kwa sasa hivi hawawezi kusema mtoto huyo aliuawa ama vinginevyo hadi hapo watakapopata uhalisi wa tukio hilo baada ya uchunguzi kukamilika.

“Siwezi kusema ameuawa hadi tutakapokamilisha uchunguzi wa tukio hilo yakiwemo mazingira ya tukio lenyewe ikiwa aliondokaje nyumbani,” amesema kamanda huyo.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali kutoka katika eneo hilo, mtoto huyo alipotea jana jioni saa 12.00 jioni lakini alipatikana saa 4.00 usiku, akiwa hana mkono mmoja na sehemu za siri katika eneo hilo la nyumba 300 za Kisasa jijini Dodoma.

Kamanda Theopista amesema mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

©Mwananchi
Kwa nini hivyo? Mbona matukio ya kikatili yamekuwa yakitokea nchini?
1. Mauaji ya vikongwe Kanda ya Ziwa
2. Mauaji ya albino
3. Wachuna ngozi
4. Mauaji ya watu wenye vipara

Wauaji hawajaridhika tu. Sasa wamehamia kwa watoto.
 
RPC Malya amesema tukio hilo limetokea eneo la Nyumba 300 za kisasa Mjini Dodoma

" Jana usiku askari Polisi akiwa katika eneo hilo aliona Mbwa akiwa na kitu mdomoni jambo lililomfanya kumsogelea karibu na kumuona mtoto huyo, alitoa taarifa police ambao walikwenda kwenye tukio na kumpeleka mtoto hospital " amesema Kamanda

" Hatuwezi kusema mtoto aliuawa ama la hadi tutakapokamilisha uchunguzi na kujua aliondokaje nyumbani " amesisitiza Kamanda Malya

Source: Mwananchi

Mungu wa Mbinguni Utuhurumie sisi

Pia soma:Dodoma: Mtoto wa miaka minne akutwa amefariki baada ya kukatwa mkono na sehemu za siri
 
Huyo mtaalamu wa sasa anahitaji viungo vya malaika wadogo
 
Back
Top Bottom