DODOMA: Mwenyekiti mtaa wa Mtakuja adaiwa kugawa viwanja kwa wanawake wenye 'wowowo' kubwa

DODOMA: Mwenyekiti mtaa wa Mtakuja adaiwa kugawa viwanja kwa wanawake wenye 'wowowo' kubwa

Mwenyekiti wa mtaa wa Mtakuja, kata ya Chang'ombe mjini Dodoma, Issa Yusuph adaiwa kugawa viwanja kwa warembo na wenye makalio makubwa.

Chini ya utaratibu huo, mwenyekiti huyo amekuwa akiwanyima viwanja wanawake wasiokuwa na sura nzuri na makalio makubwa kwa kuwa hawana msaada kwake.

Shutuma hizo zilitolewa jana na mkazi wa mtaa huo, Neema Juma alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na mkurugenzi wa manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi.

Kunambi aliitisha mkutano huo ili kutatua mgogoro wa viwanja ulioko katika eneo hilo. "Mkurugenzi wala usipate shida, tatizo lipo kwa mwenyekiti wa mtaa, huyo uliyekaa karibu naye"

"Huyo amekuwa akiwapatia viwanja wanawake wazuri na wenye makalio makubwa na sisi tusiokuwa na makalio makubwa na sura nzuri tunaishiwa kutukanwa na kukaripiwa."

"Kwa hiyo ukitaka kutatua huu mgogoro wa ardhi anza kwa kushughulika na huyo mwenyekiti kwa sababu ndiye mwenye tatizo" alisema Neema huku akishangiliwa.


Mtanzania
Hata mimi ningekuwa Mwenyekiti ningefanya hivyo hivyo
 
Back
Top Bottom