Dodoma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe avamiwa, apigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana

Dodoma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe avamiwa, apigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana

Mwanaume hana limitation ya kurudi nyumbani kwake. Muda atakao rudi ndio sahihi kwake.
Kama ni hivyo basi akubaliane na madhara yanayowapata watu watu wenye tabia ya kutembea usiku wa manane!! Ukiamua kuwa na Tania hatarishi, usishangae ukiangukia kwenye hatari na usilaumu mtu!!
 
Hata kama! SAA saba za usiku mume wa mtu unakuwa bado kwenye matembezi? Tuwe wakweli unakuwa unatembea na nani saa saba za usiku? Bila shaka utakuwa unatembea na ambao saa kama hizo wao ndo kazi zao zinakuwa zimechanganya! Unawajua sina haja ya kuwataja!! Ukitilia mhusika ni mshabiki wa bilicanas!! Mzee alikuwa anakumbukia vitu vya bilicanas!
Hivi una ubongo kweli?? Kwa hila zenu si mlimvunjia billicanas yke?? Ucku alikua anatembea na wewe, kwan kuna katazo la mwisho kutembea saa ngap??
 
Haya mambo tulishazoeaga Nchi zenye shidashida kama Burundi, Uganda, Rwanda huko naona taratibu yanabisha hodi Tanzania. Hii si nzuri kwa nchi ya Amani kama Tanzania
Mkuu you are not exceptional mkiongozwa na wanao endorse upuuzi mtafanyiwa upuuzi wazi wazi.
 
View attachment 1472626
View attachment 1472650

Salaam,

Taarifa nilizozipata hivi punde toka chanzo changu kinanihabarisha kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman A. Mbowe amevamiwa na kikundi cha watu wasiojulikana akielekea nyumbani kwake usiku huu na kupigwa na wamemuumiza.

Tukio hili limetokea majira ya saa 6-7 usiku.

Mhe. Mbowe amekimbizwa Hospitali ya Ntyuka iliyopo jijini Dodoma.

Kamanda Muroto amesema wamepata taarifa kuwa kavunjwa mguu wa kulia na amelazwa Wodi namba 4 hospitalini hapo. Amesema taarifa zaidi zitafuata

MAONI YANGU:
Mhe. Mbowe kuvamiwa na kupigwa eneo la Area D, jijini Dodoma, Mtaa wa Sengia; linalotajwa kuwa na ulinzi wa kutosha, kama ilivyotokea kwa Lissu kunaacha maswali mengi, je, hili linaweza kuwa limechochewa na Lissu kutangaza nia ya kugombea Urais wa JMT October 2020? Ni hasira au kitu gani? No one knows.

Bado najiuliza; hivi kama Taifa kwa tabia hizi za kihuni tunaelekea wapi? Hawa wanaojichukulia sheria mikononi kila siku wanafanya hivyo kwa kutumwa na nani? Matendo haya yataendelea kwa viongozi wa upinzani mpaka lini?

We need to wake up, better late than never.

Dah kwa kweli Lissu si wa mchezo....jamaa anajuwa kulipiza kisasi kwa kweli.
 
Hali ya namna hii inaweza kumfanya Antipasi asirudi nchini,na hivyo kutoa mwanya kwa mwenye amafaranga mengi kuchukua nafasi yake.?
Hivi siasa ni biashara,inayokupasa uwe ni risk taker kweli?
 
Kama ni hivyo basi akubaliane na madhara yanayowapata watu watu wenye tabia ya kutembea usiku wa manane!! Ukiamua kuwa na Tania hatarishi, usishangae ukiangukia kwenye hatari na usilaumu mtu!!
Hovyoooooo
 
Nianze Kwanza kwa Kutoa Pole zangu za dhati kabisa kwa Mheshimiwa Freeman Mbowe, Familia yake, Wapiga Kura wake, Wanachama wake wa CHADEMA, Wanasiasa mbalimbali, Wabunge na Sisi Watanzania wa kawaida tusioegemea upande wowote ule (Mzukulu) nikiwemo kwa kilichotokea. Naamini Mwenyezi Mungu ataupigania Uhai wake ila kwa waliohusika Maulana / Mola atawajibu kwa Adhabu Kali kabisa.

Jana nilipoziona tu zile Nondo Kali na zenye Mashiko za Mheshimiwa Tundu Lissu nilihisi kabisa kuwa ili kuwapoteza Watu na Kuyahamisha Mawazo yao katika Kukijadili au Kuyajadili yale aliyoyaandika ambayo yote ni mazuri basi ni lazima tu Spinning ya Hatari ingefanyika. Kilichofanyika ni kutaka Kufunika alichokifanya Lissu jana kuanzia leo Watanzania wote tujikite zaidi katika Kuzungumzia hili lililomkuta Mheshimiwa Freeman Mbowe.

Na Kiutaalam zaidi ili kuonyesha kuwa hawa Wahuni wanaolelewa vibaya na walijipanga ni kwamba itakuwa walijipanga tokea pale Taarifa za Mheshimiwa Tundu Lissu aliposema kuwa atazungumza na Watanzania hivyo hata Wao walishajipanga na walipoona Jana Mheshimiwa Tundu Lissu katoa Nondo ile Kabambe basi na Wao wakaamua Kulitekeleza hilo walilolitekeleza.

Kuna Mmoja namuheshimu sana humu ila sasa nitaanza Kumdharau amesema kuwa Mheshimiwa Mbowe Kavamiwa na Majambazi akiwa na Kimada aliyemnunua. Ameshindwa kujua ya kwamba Siku zote Mbinu za Kijasusi huwa zinaratibiwa vyema na Kimkakati zaidi kwa kuwahusisha Magenge ya Wahuni ili hata likija Kufanikiwa basi hao Majasusi wasijulikane moja kwa moja kama ni Wao.

Kwa hali ilivyo na kwa uelewa wangu mdogo sana wa Masuala ya Usalama ( Ujasusi ) ila wale wanaojua zaidi yangu hapa JF watanisaidia ni kwamba kwa Nyakati tuliopo na kwa Hofu ya Wapinzani na Agenda zao, na kwa Uchungu wa Kulikosa Jimbo la Hai ambalo wanalitaka na kwa kutaka Kuleta Hofu na Vitisho nitakuwa wa mwisho Kuamini kama katika hili Tukio la Mbowe hayo Mapanga hayakuwa na Sumu za Kijasusi.

Namalizia tu kwa kusema kama Tanzania ya sasa imefikia hapa ambapo Wanasiasa wanafanyiwa mambo haya mabaya halafu nchi ina Kiongozi Mkuu na ina Idara yake ya Usalama na mambo (matukio) haya yanatokea kila Kukicha ila wanayanyamazia basi huenda kwa Mwaka huu Tanzania ikawa na Vifo vingi vya Wanasiasa (hasa wa Upinzani) na Wanaharakati kuliko wale ambao labda CORONA ingewauwa au imewauwa.

Nawaombea LAANA mbaya sana na Kali mno kwa Mwenyezi Mungu hawa Wote wanaoyafanya haya na hasa huyo Mkubwa wao anayewatuma.
Analysis yako ipo vizuri na ina-make sense ukiondoa bias.
Siku Tundu Lissu anapigwa risasi, simulteneously RAIS Magufuli alikuwa akipokea taarifa NYETI ya kamati ya uchunguzi wa namna tunavoibiwa madini. (na kumbuka Tundu Lissu alikuwa mpinzani mkubwa wa namna serikali ilivokuwa inarekebisha mikataba mibovu ya madini)
Taarifa ile ilikuwa na a lot of BREAKING NEWS.
Lakini kuna watu walikaa wakaamua kuidestruct kwa kumvamia Lissu tena wakahakikisha wanafanya uhalifu huo mchana kweupe na katika mazingira yatakayoonesha serikali ndiyo inahusika.
Wenye akili wanajua HAKUNA intelligence ya serikali yeyote duniani inayoweza kufanya unyama ule huku ikihakikisha indicators zote zitapoint fingers kwake.
Lakini wale wahalifu walifanikiwa -kwanza kudestruct hoja ya Kamati ya madini, na pili walifanikiwa kuwaaminisha baadhi ya watu kuwa serikali ndiyo iliyomtungua Lissu.
 
Kama ni hivyo basi akubaliane na madhara yanayowapata watu watu wenye tabia ya kutembea usiku wa manane!! Ukiamua kuwa na Tania hatarishi, usishangae ukiangukia kwenye hatari na usilaumu mtu!!
Nasikia maeneo aliyo shambuliwa kuna ulinzi mkali sana sasa hapo ndipo inaleta utata kidogo.
 
we mpuuzi kaa kimy tu, hii ncbi tupo huru hata kutoka saa tisa usiku kwenda mahali popote kufanya chochote halali, hayo mambo ya kuhoji ni uminywaji wa uhuru,,,, yeyote aliefanya huu upuuzi ni yule yule aliemwagia lisu risasi,
Pumbavu kabisa! Yani mko huru mda wote alafu usiku unajifungia na makomeo kila kona?
Mwambieni Mbowe awe serious

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
Sitashangaa kama mke wake atakuwa anatoa machozi ya mamba!! Kina mama wanajua!!
 
Kama CHADEMA hawakujifunza kutokana na yaliyomkuta Mh Lissu basi nina wasiwasi na mikakati yao! Yaani kwa Mh. Mbowe hadi sasa hivi na hakuna Mlinzi wala yeye hana walinzi na hata CCTV Camera hakuna? Hata ulinzi wake binafsi kama bastola, pilipili, manati....

download.jpg
 
Back
Top Bottom