Dodoma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe avamiwa, apigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana

Ccm ya magufuli itakunywa damu nyingi mwaka huu hadi itapike
 
Tanzania tunachokitafuta tutakipata.... wenye dhamana msidhani mpo salama eti kwa sababu mnatembea na ulinzi muda wote...mambo yakisanuka huwezi kuyapoza kwa mlio wa risasi....hapo ni kama unachochea tu.

Tunakwenda kwenye uchaguzi Mkuu, hizi ni dalili mbaya sana...kama kiongozi anashambuliwa je watu wa kawaida si watafyekwa vichwa mchacha mchana..

Tusilipeleke hili taifa kusiko, kutofautiana kiitikadi si dhambi ya kujenga chuki na uadui kama wanyama wa mwitu, hapana sisi ni Binadamu na tumeumbwa kwa mfano wa Mungu...nani anayetuletea unyama huu katika nchi yetu? mbona mambo haya yahakuwepo tangu kitambo kwa nini iwe sasa?
 
Siasa zimekuwa uadui, badala ya hoja watu wanashambuliana kwa maneno makali, matusi na silahà.

Taifa linazidi kuwa la kindezi sana.
 
Mbowe hana walinzi?

Kama hii habari ni ya kweli basi CHADEMA ni sikio la kufa lisilosikia dawa!
Maswali magumu, kama hilo lako, litapewa jibu jepesi kabisa.

Lissu, mnajimu wao, naye alishambuliwa na kwa kauli ya dereva wake alimtaahadharisha na bado hawakuchukua hatua za kiusalama!

Mbowe, KUB, anao walinzi na ikizingatiwa hivi karibuni amekuwa akiaandamwa na tuhuma, kwa mtu yeyote, kikawaida, angeimarisha usalama wake.

Lissu katangaza nia na saa chache M/Kiti wake, ambaye hatima ya Lissu kupitishwa awe mgombea iko mikononi mwake, anashambuliwa! Je, kuna uhusiano - connecting dots?

Namwombea mkono wa uponyaji wake Mola ufanye kazi yake, arejee kukitumikia chama kuelekea uchaguzi mkuu
 
Minyukano imeanza, tumeanza kuvunjana miguu mapema kabisa..
 
Wana CCM wenzangu WAOGA SANA, yaani tumekuwa kama INTALAHAMWE? Kweli?
 
Wameanza ile Mbinu yao ya kujiteka kutafuta huruma ya Wapiga kura. Uzuri tuliokuwa Chadema tunaifahamu hii mbinu ya kutafuta kiki za kisiasa. Mbowe amejiteka. Acheni ujinga wenu wa kuyasumbua masikio yetu.
Na endeleeni kujiombea kujiteka, One day Alshab babu watawafanyia kweli mbwea nyie ambao hamjui madhara ya hiyo mbinu ya kisenge
 
Saa 6_7mbona usiku Sana, au kazi za bunge huwa zinaendelea mpaka mda huo?
Kuna utaratibu wa kupangiana muda wa kutembea usiku. Je kama ametoka kwenye shughuli binafsi, wengine ofisi ndo wanafunga ofisi muda huo
 
ONLY IN AFRICA
 
Kwa uoga walionao watz hata siku moja hayatakuja kutokea machafuko
 
Kwa hili tukio la kushambuliwa kwa mbowe tusiilaumu tuu serikali bali tulitizame kwa mitazamo kama 2 au mitatu hivi.

(1)inawezekana kweli serikali inajua au laa hasha haijui (hapa kama haihusiki au kujua ijitokeze wakanushe ili kututoa tongoto.

(2)inawezekana serikali haijui ila huku huko serikalini kuna kundi linataka au limeamua kumwekea doa mh rais hasa hasa kipindi hichi tunakokaribia uchaguzi ambalo hili kundi liko humo humo ila halimkubali limeamua kama mbwai na iwe mbwai kumkomoa.

(3)inawezekana huu ni mpango umepangwa baada ya upinzani kutangaza nafasi ya urais iko wazi na aliekuwa mbunge wa Singida Tundu Lissu kutangaza nia ya kugombea,wametengeneza tukio hili ili huko aliko kwa kuwa yuko nje ili asije aone bado usalama wake utakuwa mashakani kama akija, hivi vyote vinawezekana kwa mtizamo wangu tusiilaumu tuu serikali tuache vyombo vya ulinzi na usalama vifanye kazi itajulikana tuu kama serikali haihusiki.
 
Dah, kisa madaraka tu inaonekana bora kuua, kutesa wakosoaji wako! Kumbuka: Siku moja isiojulikana utapata hukumu yako ukiwa hai au umekufa, duniani au ahera. Get well soon Mbowe. Siasa zinakua uadui sasa.
 
Naiogopa nchi yangu.
Au nilikufa nimefufukia nchi nyingine ?
Hii siyo tz yangu.
 
Kupambania haki bongo nitabu sana wananchi waoga na hawajui hata kufikiri vyema unaweza jikuta unaumizwa mmno na familia inapitia magumu nawao watalialia umechukua vihela vyao sijui unaenda kulima bull shiii!!!

Ingefaa maandamano ya amani kama USA hawa wasiotakiwa kujulikana ifike mahali wajulikane uovu umekuwa mkubwa sana tatizo hata wakijulikana hawatofanywa kitu kama yule wa dokta ulimboka ambaye hakufanywa lolote na wananchi wakatulia tuli!! Tuwaambie hawa "chama cha mauaji"

#toa goti lako shingoni mwetu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…