Dodoma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe avamiwa, apigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana

Wewe ni lofa hizo 7000/- unazolipwa zisikufanye uwe lofa
Lijualikali amesema mbowe alitoka kwenye ulevi ameanguka kwenye ngazi akaamua atafutie kiki kuwa kapigwa
 
Yeah! Serikali ya KIDHALIMU ambayo imeshindwa kuchunguza kifo cha Mawazo, kupotea kwa Ben Saanane, Azory Gwanda na wengine chungu nzima pia shambulizi la lissu. Serikali ambayo ilihusika katika kuzuia malipo ya matibabu kwa lissu na pia kuhusika kumpora Ubunge wake.

Nonsense, yaani aumizwe Kwa madhambi yake mseme Serikali.
 
Alikuwepo wakati wa tukio au kaamua KUROPOKA bila ya kuwa na ushahidi!?

Lijualikali amesema mbowe alitoka kwenye ulevi ameanguka kwenye ngazi akaamua atafutie kiki kuwa kapigwa
 
Kuna umuhimu wa watu kuonesha ubora wao kama wanavyoaminisha umma. Ukishajiona ni mtu muhimu kiasi cha kuhutubia taifa kwa nafasi yako, ukaomba hata urais wa nchi, unastahili kuonesha ubora wa matendo yako hata iwe kwa kuigiza.

Awamu iliyopita tulilaani rais kusafiri bila faida kwa taifa. Rais kunengua kila asikiapo muziki, nk. Leo hii KUB wetu anatembea usiku wa manane bila walinzi bila kueleweka anatoka wapi. Atawezaje kutuaminisha sababu ya kushambuliwa ktk mazingira hayo? Ni mazoea ya mitaani na ndiyo maana nasema haitakuja kuwa rahisi makuzi ya disco yakugeuze kuwa kiongozi wa taifa bora,.
 
Duh kwani ni huo mguu tu au wamemdhuru na humo ndani
 
Ila vitu vingine jamani, inamaana Mbowe hana bodigadi,yaani anatembea bila walinzi?? Diamond ana bodgad sembuse Kub?? Tuache maigizo basi
Huyo alikuwa na ujinga wake mitaani. Unawezaje kutembea saa 6 usiku kwa nafasi yako bila hata rafiki. Hata kibaka na rungu lake atakujeruhi tu! Ndo tunapoanzia kupima busara za wale wanaotaka kuwa viongozi wa nchi na wana wafuasi kibao!
 
Baada ya kupata taharifa ya Mbowe kuvamiwa, nilistahajabu kidogo kuona watu wengi wakishangaa mitandaoni, baada ya kuisikia kauli ya Kamanda Muroto nimeshawishika kushare machache yangu.

Kamanda Muroto amesema kwamba tukio la kuvamiwa kwa Mh Freeman Mbowe ni la kawaida, na mm ninamuunga mkono.

Yamekwishatokea mengi sana kuliko la huyo Mwenyekiti wa Chadema, wengineo wamepoteza maisha, na wengineo haifahamiki kama wapo hai au walitangulizwa mbele za haki.

Kauli ya Kamanda huyo shujaa inatakiwa wanasiasa na wananchi waielewe vizuri, inawezekana hayakuzoeleka sana katika vipindi vilivyopita lkn kwa sasa inatakiwa Wananchi/aliyevamiwa/aliyevamia wasistaajabu.......
 
Hata baba yako akivamiwa tulia hivo hivo kama unanyolewa
 
Maana yake tutarajie matukio makubwa na ya kutisha hivyo hili ni cha mtoto tu.
 
Pole Mbowe tujifunze kuwahi kurudi nyumbani
Sishangai kauli zako. Hata Magufuli aliwakebehi wana Bukoba wakati wa maafa ya tetemeko. Siyo mila na Desturi za kiafrika. Wakati wa janga kama huu, kawaida ni kutoa pole tu.

Upinzani na CCM ni watani. Wakati wa shida hupeana pole tu, kama Simba na Yanga vile. Ila awamu hii ni uadui tu, hasa serikali dhidi ya upinzani. Na nyie wapambe ndio mnakopi na kupesti utadhani hizo bongo mlizopewa na Mungu mnazitumia kupengea kamasi vile

Kama huna lifaalo kuongea muda huu, ni busara kukaa kimya
 
Katukio ka kawaida saaaanaaaaaaa. Sera ya Siasa za Matukio na Kiki hapo zimebumba kabisa. Wanasema mwisho wa Ubaya ni AIBU.
 
Mkuu mbona nimetoa pole
 
Pole kwa mlevi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…