Dodoma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe avamiwa, apigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana

Dodoma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe avamiwa, apigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana

Kwani amewaumiza wangapi ndani ya Chama?
Naunga Mkono hoja, ni wakati wake sasa kulipa.
Unalala na wake za watu, kila girlfriend wa mwenzio unamtamani, hutaki mtu akuguse.
huyo muhuni unaye mzungumzia hapa ni nani? naona kama kuna mtu mwenye tabia cahfu
 
Mkuu km mimi ni mmoja niliyekuumiza uniwe radhi sana
Ila Chadema mkiacha matusi mtandaoni na nyie mtatendewa vyema

Ila kama yule jamaa enu wa ubeligiji anaongoza kwa matusi unadhani nyie ntaachwa kutukanwa?

Mimi Mbowe namkubali ni mtu humble japo anamagumashi kwenye pesa na totoz
 
Unadhani wataona vipi vibaya ikiwa huo uhuni unawafaidisha?
Yaani damu iliyomwagika ya Mtanzania mwenzetu tunafurahia? Kweli kabisa? Ni lini Mbowe aliidhihaki Tanzania hata kustahili hayo? kustahili dhihaka na kejeli kutoka kwa wana CCM? Je wao wataishi daima?? Kwanini tukubali siasa itufikishe hapa kuw aleo akiumizwa Mbowe, akiuliwa Mawazo, na Pro Chadema wengine tufurahie??
 
Tumewaambia Chadema watalipwa kutokana na matendo yao

Wao hufurahia mabaya ya Ccm kuna wengine wanaombea hata viongozi wafe
Acha undumilakuwi sio chadema waliokuwa wanafurahia vifo vya watu/viongozi waliokuwa wanakufa kipindi Cha hofu ya Corona? Ikitokea kada wa CCM amekufa hata kwa malaria mnasema Corona na dhihaka juu Sasa mnadhani DJ wenu adhihakiwa
 
Mkuu km mimi ni mmoja niliyekuumiza uniwe radhi sana. Ila Chadema mkiacha matusi mtandaoni na nyie mtatendewa vyema.
Nionyeshe au nitajie popote pale mwana chadema yoyote yule aliyetukana, nipe mfano wowote ule. Ndugu Tanzania ni yetu sote, siasa za kishenzi namna hii hazijengi, tukosoane kwa heshima. Wote tuna maumivu sawa, leo hii Mbowe yuko kitandani, wewe inakusaidia nini? inakuongezea nini? Tukeindelea kushabikia huu ushenzi watoto wetu na ndugu zetu watarithi nini? Chuki? CCM, CCM, CCM MUNGU anawaona.
 
Sio uongo, nimefika mahali nimetamani makundi kama ya mungiki Kule Kenya ambayo kazi yake ilikuwa kulipa visasi na mpaka watu wakaheshimiana.

Viongozi wa CCM ndio wasababishaji wa haya mambo na yakitokea nadhani wanapongezana. Pengine wakiona wenzao wawili watatu wametawanywa ubongo ndio watatoa matamko ya kulaani ujinga huu.

Yaani KUB anapigwa kama kibaka na nchi imetulia? Ingekuwa kwingine sasa hivi tunazima moto vituo vya mafuta vilivyo chomwa, ofisi za serikali au vituo vya polisi. Ila ndio tuendako
 
Acha undumilakuwi sio chadema waliokuwa wanafurahia vifo vya watu/viongozi waliokuwa wanakufa kipindi Cha hofu ya Corona? Ikitokea kada wa CCM amekufa hata kwa malaria mnasema Corona na dhihaka juu Sasa mnadhani DJ wenu adhihakiwa
Wewe shetani nakuweka kiporo, DJ naye ni mtu, wewe mwenye PhD ndio umefanya nini? Kutuua? Kutuumiza? Kisa mnaringia dola? Ok
 
Tumewaambia Chadema watalipwa kutokana na matendo yao

Wao hufurahia mabaya ya Ccm kuna wengine wanaombea hata viongozi wafe
Nionyeshe ni wapi walifurahia? Kwahio kwakuwa walifurahia ndio na nhyie mfurahie? ndio busara inavyowatuma? Ok sawa ngoja tuone
 
Yaani damu iliyomwagika ya Mtanzania mwenzetu tunafurahia? Kweli kabisa? Ni lini Mbowe aliidhihaki Tanzania hata kustahili hayo? kustahili dhihaka na kejeli kutoka kwa wana CCM? Je wao wataishi daima?? Kwanini tukubali siasa itufikishe hapa kuw aleo akiumizwa Mbowe, akiuliwa Mawazo, na Pro Chadema wengine tufurahie??
Inasikitisha sana.
 
Tukiacha siasa, nadhani sasa ubinadamu lazima uchukuwe nafasi yake.
Mbowe ni baba, mume, kaka na mjomba wa watu.
Kwakweli watu tomekosa utu na siasa zinaonekana kututawala hadi kutothamini tena ubinadamu.
Wewe tulia tu, waache tu, hakuna shida, MBOWE sio mtu, Mbowe ni kama mnyama tu, si ndio wanavyochukulia, tulia tu. MUNGU hadhikiwi
 
wewe shetani nakuweka kiporo, DJ naye ni mtu, wewe mwenye PhD ndio umefanya nini? Kutuua? Kutuumiza? Kisa mnaringia dola? Ok
Shetani ni wewe mwenye ndimi mbili na mwenyekiti wenu udj ni professional yake Nani kasema yeye ni sio mtu, huu mchezo hauitaji hasira [emoji23][emoji1787][emoji2960]
a9868a767d072d04683d769372a2934e.jpg
 
Nianze Kwanza kwa Kutoa Pole zangu za dhati kabisa kwa Mheshimiwa Freeman Mbowe, Familia yake, Wapiga Kura wake, Wanachama wake wa CHADEMA, Wanasiasa mbalimbali, Wabunge na Sisi Watanzania wa kawaida tusioegemea upande wowote ule (Mzukulu) nikiwemo kwa kilichotokea. Naamini Mwenyezi Mungu ataupigania Uhai wake ila kwa waliohusika Maulana / Mola atawajibu kwa Adhabu Kali kabisa.

Jana nilipoziona tu zile Nondo Kali na zenye Mashiko za Mheshimiwa Tundu Lissu nilihisi kabisa kuwa ili kuwapoteza Watu na Kuyahamisha Mawazo yao katika Kukijadili au Kuyajadili yale aliyoyaandika ambayo yote ni mazuri basi ni lazima tu Spinning ya Hatari ingefanyika. Kilichofanyika ni kutaka Kufunika alichokifanya Lissu jana kuanzia leo Watanzania wote tujikite zaidi katika Kuzungumzia hili lililomkuta Mheshimiwa Freeman Mbowe.

Na Kiutaalam zaidi ili kuonyesha kuwa hawa Wahuni wanaolelewa vibaya na walijipanga ni kwamba itakuwa walijipanga tokea pale Taarifa za Mheshimiwa Tundu Lissu aliposema kuwa atazungumza na Watanzania hivyo hata Wao walishajipanga na walipoona Jana Mheshimiwa Tundu Lissu katoa Nondo ile Kabambe basi na Wao wakaamua Kulitekeleza hilo walilolitekeleza.

Kuna Mmoja namuheshimu sana humu ila sasa nitaanza Kumdharau amesema kuwa Mheshimiwa Mbowe Kavamiwa na Majambazi akiwa na Kimada aliyemnunua. Ameshindwa kujua ya kwamba Siku zote Mbinu za Kijasusi huwa zinaratibiwa vyema na Kimkakati zaidi kwa kuwahusisha Magenge ya Wahuni ili hata likija Kufanikiwa basi hao Majasusi wasijulikane moja kwa moja kama ni Wao.

Kwa hali ilivyo na kwa uelewa wangu mdogo sana wa Masuala ya Usalama ( Ujasusi ) ila wale wanaojua zaidi yangu hapa JF watanisaidia ni kwamba kwa Nyakati tuliopo na kwa Hofu ya Wapinzani na Agenda zao, na kwa Uchungu wa Kulikosa Jimbo la Hai ambalo wanalitaka na kwa kutaka Kuleta Hofu na Vitisho nitakuwa wa mwisho Kuamini kama katika hili Tukio la Mbowe hayo Mapanga hayakuwa na Sumu za Kijasusi.

Namalizia tu kwa kusema kama Tanzania ya sasa imefikia hapa ambapo Wanasiasa wanafanyiwa mambo haya mabaya halafu nchi ina Kiongozi Mkuu na ina Idara yake ya Usalama na mambo (matukio) haya yanatokea kila Kukicha ila wanayanyamazia basi huenda kwa Mwaka huu Tanzania ikawa na Vifo vingi vya Wanasiasa (hasa wa Upinzani) na Wanaharakati kuliko wale ambao labda CORONA ingewauwa au imewauwa.

Nawaombea LAANA mbaya sana na Kali mno kwa Mwenyezi Mungu hawa Wote wanaoyafanya haya na hasa huyo Mkubwa wao anayewatuma.
Tanzania kwa matakwa ya kisiasa inaelekea kubaya kwa mendokasi. Ni mtoto mdogo tu ndiye atadiriki kutamka wazi kuwa: "Mfalme yuko uchi".
 
Tanzania tuna upuuzi upuuzi bado. Kwa Tz tunahisi kukashifu na matusi ndiyo siasa yenyewe.

Hivyo pande zote mbili za utawala na upinzani kutukanana na kashfa imekua sehemu ya maisha ya kisiasa. Visiwani wameenda mbali mpaka kuuziana bidhaa imekua tatizo kidogo.

That being said, kwani Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani hana ulinzi binafsi?
 
Nyie hamna kumbukumbu mmejaa ujinga wakifa viongozi wa Ccm mnashangilia mmesahau hilo?

Back
Top Bottom