Dodoma: NEMC yazifungia Rainbow na Chako ni Chako kwa kupiga kelele

Dodoma: NEMC yazifungia Rainbow na Chako ni Chako kwa kupiga kelele

Walevi mnawaonea sana wivu

Kama ni makelele mgeanzia huko stendi za Mabasi na daladala

Nendeni huko Mpanda watu wanafyeka misitu kama kupambana na shetani

Mipango miji mibovu miundo mbinu ya maji taka nk

Nendeni field mje na mipango yenye AFYA walevi achaneni nao wanajuwa KUJIONGOZA
 
Itakuwa walikuwa wanajadili mambo ya Dungange , huyu kijana asithubutu kumuacha Mganga wake , wallah tena
 
Pombe ndio source of income baada ya mikopo.

Sasa unataka watu wasilipwe mishahara ??
 
Hata Misikiti. Ni kero asubuhi tunaamshwa kuwa kuna Swala. Haya mambo waangalie yanatunyima sisi wengine utulivu Makanisa, Misikiti nayo saa mbili na kumi na moja asubuhi ni kelele tu.
Walau umesema asubuhi,kelele za misikiti ni predictable zinajadilika,na hazizidi dk 5 na sometimes hutusaidia kuwah mihangaiko!!sasa kanisa linakesha kuanzia saa moja usiku mpaka asubuhi tena mtu anaweka cd halafu anaondoka anawaachia msala[emoji1787]
 
Nadhan target ni rainbow. Wanamziki mzuri sana.
 
Tunaomba na NEMC wa Dar waamke manake wamelala. Loh
Luiza Mbutu hukumsikia siku ile ya TMA anamlilia mama, walipigwa PIN watalisha wapi family zao, kifanyike utaratibu wa soundproof km inavyokua kwenye nightclub ukiwa nje nightclub husikii mziki wowote Ila ukiingia ndani unasikizia mziki au mtu alifungua mlango ndio unasikia mziki unapiga ndani Ila nje ni kimya kabisa, sijui wamejengaje yale majengo
 
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limezifungia bar za wazi za Rainbow na Chako ni Chako Pub za Jiini Dodoma baada kukuta kelele zilizo kinyume cha sheria ya usimamizi wa mazingira namba 20 va mwaka 2004 na kanuni ya viwango vya udhibiti wa kelele na mtetemo ya mwaka 2015.

Akiongea leo Dodoma katika oparesheni hiyo Saida Madusi Afisa Mkaguzi wa Mazingira wa NEMC Kanda ya Kati, amesema walifanya ukaguzi huo maïra ya saa tisa usiku na kukuta ukiukwaii wa sheria hivo "Sheria hivo inasema maeneo ambayo yanazunguka maeneo ya Watu na kuna biashara kelele zinatakiwa kuwa 60 DBA wakati wa mchana na 40 usiku, tumefanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali va biashara valiyo jirani na makazi ya Watu"

"Tumefika hapa tumekuta kelele zimefika mpaka 68 DBA na zilikuwa zinasikika hadi nie na tumetembela Mairani walikuwa wanalalamika hizo kelele, sasa tumewaagiza Jumatatu wafike Ofisi za NEMC Kanda ya Kati"
Wakuje na huku uswahilini hatulali kwa mikesha wakadai ni ibada kila siku toka jumatatu hadi jumatatu
 
Siwezi kufunga biashara kijinga hivyo - hahati mbaya wkt wanapima hizo dba hawashirikishi wahusika - so mahakani ni rahisi sana kuwashinda
 
Walau umesema asubuhi,kelele za misikiti ni predictable zinajadilika,na hazizidi dk 5 na sometimes hutusaidia kuwah mihangaiko!!sasa kanisa linakesha kuanzia saa moja usiku mpaka asubuhi tena mtu anaweka cd halafu anaondoka anawaachia msala[emoji1787]
Kelele hata kwa dk 1 ni kelele. Ukishaamshwa usingizini au mtoto akiamshwa ni ngumu kulala anasumbua. Yaani ni kero sana ukijenga nyumba au ukipanga maeneo ya namna hiyo.
 
Mamlaka ya Mazingira NEMC imeifunga Bar maarufu Jijini Dodoma iitwayo Chako ni Chako Pub kwa sababu za uharibifu wa Mazingira ikiwemo makelele

Hapa ndio Wabunge Wengi hupendelea kukutana na rafiki zao

Hata Mwamba alivyoanguka na kuvunjika mguu mh Kibajaj alidai alikuwa ametoka Chako ni Chako

Kufungiwa kwa Chako ni Chako Pub kumeripotiwa na Ayo tv

Dominica Njema!
 
Back
Top Bottom