Dodoma: Peter Mwakiposile amuua mkewe kisa Kikoba

Poleni Sana, Vikoba Shida Sana
Ki ukweli haya mambo ya vikoba/michezo ya kukopeshana kwa wanawake kwa sasa ni tatizo kubwa sana!!yaani ikifika siku ya marejesho mtu hatulii kabisa!!siku moja nimekutana na dada mmoja tandika simjui hanijui, akanisimamisha na kuniomba hata 2000 kwani jioni anatakiwa awe ametimiza 25, 000 za mchezo!!sasa hapo kuna nini??
 
Pole sana ndugu yangu, naona kabisa unavyoumia. Mwache apambane na vicoba vyake mwenyewe ila sasa......
Kama hana kipato cha kueleweka atafanya kila means apate pesa ya marejesho. Pole zaidi😆😆😆
 
Pole sana ndugu yangu, naona kabisa unavyoumia. Mwache apambane na vicoba vyake mwenyewe ila sasa......
Kama hana kipato cha kueleweka atafanya kila means apate pesa ya marejesho. Pole zaidi😆😆😆
Kazi anayo kwa hio atajua mwenyewe anafanyaje na Vicoba vyake maana ukipiga mwisho ndio eeenhe hivyo mwisho unajikuta Segerea Keko
 
He's not a man but a coward child
 
Kama huna akili kwann uoe? Ndoa inataka mtu mwenye akili, SAsa anadhani ndugu wa mke nao watamuacha tu kawaulia ndugu yao
 
Last year wife alinishirikisha kwenye hiyo vicoba nikampa go ahead sasa bana kumbe alichukua vitabu kumi badala ya vitabu vitano tulivyokubaliana.
To make story short mke wangu akawa kama chuma ulete kila pesa unayompa haimtoshi iwe matumizi ya nyumbani na watoto au pesa ya matumizi yake binafsi akawa yuko busy sana hatulii nyumbani mtu ukirudi home msosi haueleweki na mbaya zaidi akafikia hatua ya kutumia pesa ya ada ya watoto ya term nzima kimyakimya....
Ningekurupuka kwenye maamuzi bila kuchunguza mzizi wa tatizo ningeishia pabaya aisee
 
Msitafute visingizo kwahiyo unataka kusema wanaocheza vikoba waume zao hawahudumii mnaendekeza tamaa zisizo na msingi
 
Sitetei mauaji lakini naomba kufahamu kutoka kwako, kwani VIKOBA ni ajira?
 
Sio wote japo wapo wengi tu wana tabia ya kujiuza ili kupata hisa au rejesho.

Kama ambavyo kuna faida hasara pia hazikosekani.

Ila wapo ambao vicoba vimewabeba sana sana nikiwemo mimi hapa.

Tena kicoba cha halali kabisaa
Pesa za VIKOBA huwa mnapata wapi?
 
Kikoba hauchezi wewe inacheza biashara, if you don't have proper source of income achana na hivi vitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…