Dodoma: Peter Mwakiposile amuua mkewe kisa Kikoba

Sijui kama uandishi huu unatoa picha sahihi japo kufa ni kufa tu.Nijuavyo ni kuwa marehemu alipigwa ndio baada ya kuchelewa kurudi usiku ila hakufa papo kwa papo. Alipelekwa hospitali kutibiwa akalazwa siku kadhaa kisha akapata nafuu na kurudi nyumbani ila akiwa nyumbani akazidiwa na baadae kufariki.
 
Sitetei mauaji lakini naomba kufahamu kutoka kwako, kwani VIKOBA ni ajira?
Nenda kwanza ukasome maana ya vicoba na how it works then utapata majibu ya kila kitu.
Kwa kifupi ili uwe mwana kikoba lazima uwe na savings hata kama ni buku 2 kulingana na makubaliano waliyowekeana kuhusiana na bei ya hisa zao.
Sasa kama wewe mkeo hana chanzo cha mapato na ameingia huko basi shida sio kikoba ila shida atakuwa nayo mkeo
 
Ila kuna mambo yanaudhi sana, unaweza kuta mwamba anamuachia ukwasi wa kutosha , lakini bibie ndio kwanzaaa anazidi kujiunga na vicoba vingine, gharama ya kuvihudumia bwanaake ndio anatoa, mwisho wa siku mwanaume ukishindwa kutoa marejesho ndio yanaanza mapicha picha humo ndani, chakula hapiki, akipika anapika makande..na vyakula vingine ambavyo hutegemei kuvikuta nyumbani kwako, yaaani ni balaa tupu. Vicoba kama mwanamke hana kazi usimruhusu ajiunge .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…