utaifakwanza
JF-Expert Member
- Feb 1, 2013
- 14,193
- 2,813
Rais wa Nchi Dr. JOHN MAGUFULI leo hii tarehe 13 Aprili anazindua rasmi ofisi za Rais Ikulu Makao Makuu Chamwino Dodoma.
Pia Rais Magufuli anazindua mji mpya wa Serikali eneo la Mtumba.
Hii ni kuashiria kuwa ni rasmi sasa Rais anahamia Dodoma, makao makuu ya nchi.
Matukio haya yanashuhudiwa na viongozi wote wakuu wa nchi akiwemo Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri na Mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania.
Fuatilia uzi huu kwa updates.
updates......
Rais na msafara wake ameshawasili hapa na sasa ni dua maalum kutoka kwa viongozi wa dini.
updates......waziri mkuu anaongea hivi sasa, anampongeza rais kwa hatua yake ya kuamua kuhamishia makao makuu ya nchi dodoma ambayo ni ndoto ya mwasisi wa taifa hili Julius kambarage Nyerere. anasema ujenzi wa majengo ya ofisi ya rais yanakamilika mwezi mei wakati ofisi ya waziri mkuu yanakamilika mwezi huu wa nne.
updates............
sasa makam wa rais anahutubia. anampongeza rais kwa hatua hii muhimu ya kukamilisha azma ya kuhamia Dodoma. anasema tutahakikisha tunaitumia vizuri fursa hii ya kuhamia dodoma kuijenga Tanzania
Rais anasema ndoto ya kuhamia Dodoma iliazimiwa miaka kumi baada ya mwaka 1978.
Anasema kuhamia dodoma sio kazi rahisi...Lakini leo nimefrahi mnooo kuona ndoto ya baba wa taifa imetimia. Hata watz wamefurahi mno kuona malengo yao yametimia.
Na mimi nakuja Dodoma, nilichelewa kidogo kwa sababu nauguliwa na mama yangu ambaye hadi sasa hawezi kuongea hawezi kufanya chochote, lakini kwa sasa nahamia Dodoma, sipo mbali ni kama nimeshahamia tu.
Kuhusu vijana wa JKT walioshiriki kikamilifu kazi ya kujenga makao makuu haya nawaajiri rasmi lakini CDF usichomekee idadi, wale wa Mirerani walishaajiriwa na wamemaliza mafunzo juzi. Walijenga nyumba za Ikulu, wanaojenga ukuta wa Ikulu mle ndani, waliojenga nyumba za magereza hao ndio nimewaajiri.
Naongeza na wale wanaofanya kazi kwenye kiwanda cha mlale. Hao wote ndio tutapanga mikakati nao, kaa na wakuu wenzio wa vyombo.. Kaa na TAKUKURU, Magereza,TISS,Polisi nk tuwatumie hawa vijana.
Aliyesimamia hapa kuanzia leo anakuwa Brigedia, muongezee vinavyotakiwa kukaa kwenye mabega.Kuanzia leo tuwe na kikosi cha ujenzi na mkuu wake ni huyu niliyempandisha cheo hapa.
CDF unafanya vizuri sana, nakutuma mengi unafanya hivyo hivyo wanaotamani ustaafu leo haustaafu labda uharibu.Umetoa hadi gawio la milioni 700 haijawahi kutokea, nasubiri gawio la Polisi, Magereza nk