DODOMA: Rais Magufuli azindua ofisi ya Rais (Ikulu) Chamwino na mji wa Serikali eneo la Mtumba

DODOMA: Rais Magufuli azindua ofisi ya Rais (Ikulu) Chamwino na mji wa Serikali eneo la Mtumba

“Nina furaha ya ajabu kuona ndoto ya baba wa Taifa inakamilika kwani ni heshima kubwa na furaha kubwa kwa nchi kuona makao makuu ya serikali yanahamia hapa,” – Rais Magufuli

“Wale wote walioshiriki ujenzi wa mji huu wa Serikali, walioshiriki kujenga nyumba 41, nyumba za Magereza, waliojenga ukuta wa Ikulu, na kiwanda cha Mahindi, hao wote nimewaajiri” -Mh. Rais Magufuli

“Ninataka siku moja tuwe na kikosi cha Ujenzi na kiongozwe na huyu aliyesimamia ujenzi huu ambaye ni Kanali Nguge” -Mh. Rais Magufuli

“Nawapongeza watumishi wote wa Serikali ambao mmeshahamia Dodoma mkiongozwa na mawaziri na Makatibu Wakuu wenu” -Mh. Magufuli, Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Nimemteua huyu ili tuwe na vikosi vya ujenzi, mtu anayefanya vizuri jamani hatutakiwi kuwaonea wivu. Alipokuwa kwenye ujenzi wa ukuta Mirerani alipigwa vita, na baadaye kupelekwa kusimamia michezo." - Rais Magufuli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akifurahia kutimiza ndoto ya kuwa mji mkuu wa serikali huku akiua demokrasia..
Magufuli baba wa taifa angekuwepo hapo sijui kama angehudhuria

Umetufanya kuishi kwa uwoga wakati ni kwetu wenyewe huku tukiminywa Uhuru wa kutoa maoni na kukosoa pale pananpokosewa kwa taifa letu wenyewe..tunapotea tu kama kuku and you don't care...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani si alisema atahamia kabla mwaka 2018 haujaisha?

Tuna Rais chenga mpaka anatushawishi tule mabange hehehe[emoji21]
Nukuu

NA MIMI NAKUJA DODOMA, NILICHELEWA KIDOGO KWA SABABU NAUGULIWA NA MAMA YANGU AMBAYE HADI SASA HAWEZI KUONGEA HAWEZI KUFANYA CHOCHOTE, LAKINI KWA SASA NAHAMIA DODOMA, SIPO MBALI NI KAMA NIMESHAHAMIA TU. FIDIA ZILIPWE..- Magufuli.

Mama yake anaishi naye Magogoni? Au gharama za kuhamia Dom zilihamia kwa matibabu ya Mama yake?

NB: Sijakuuliza wewe niliyekuquote, ila nimehoji hii sababu yake, wajuzi watudadavulie
 
Nakuelewa kiongozi, Magu anajichanganya sana, anadhani mabange kila mtu anaweza kuvuta.

Mama magu kiukweli maisha yake yako ukingoni ameshamaliza kazi iliyomleta duniani abarikiwe, amkanye mwanae aache kiburi na mabavu kabla hajaondoka.
 
Magu kubadilika tabia yake ni vigumu sana. Kashakuwa chronic

Uzuri kashatuambia sisi watanzania sio wajinga..
 
Makamu wa rais Samia Suluhu Hassan ameshangazwa na baadhi ya watu wanaoacha kujadili maendeleo yanayoletwa na rais kwa nchi yetu na kujadili ulinzi wa rais Magufuli!.

Mshangao huo wa Samia umekuja baada Freeman Mbowe kuonekana akihoji kwa nini ulinzi wa rais Magufuli umekuwa mkubwa sana!, mama Samia amewataka Chadema na watanzania wengine wenye roho za korosho kwa maendeleo ya nchi yetu kubadilika na kuanza kutangaza maendeleo ya nchi badala ya kutangaza upuuzi wa kuhoji ulinzi wa rais!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uyu sindio alisema watatoa milioni 50 kila kijiji ziko wapi? naye kafirisika au?

Watu lazima wahoji maana ulinzi ni kodi zao wana haki ya kuhoji Magufuli yupo na uadui na nani mpaka alindwe kama wakina George W Bush wa marekani kipindi kile? Au Putin.

Kwa lipi yuko na uadui na nani?.
 
Makamu wa rais Samia Suluhu Hassan ameshangazwa na baadhi ya watu wanaoacha kujadili maendeleo yanayoletwa na rais kwa nchi yetu na kujadili ulinzi wa rais Magufuli!.

Mshangao huo wa Samia umekuja baada Freeman Mbowe kuonekana akihoji kwa nini ulinzi wa rais Magufuli umekuwa mkubwa sana!, mama Samia amewataka Chadema na watanzania wengine wenye roho za korosho kwa maendeleo ya nchi yetu kubadilika na kuanza kutangaza maendeleo ya nchi badala ya kutangaza upuuzi wa kuhoji ulinzi wa rais!

Sent using Jamii Forums mobile app
Duh Mama Samia nae kaingia kwenye siasa za namna hii aisee..Sad indeed

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makamu wa rais Samia Suluhu Hassan ameshangazwa na baadhi ya watu wanaoacha kujadili maendeleo yanayoletwa na rais kwa nchi yetu na kujadili ulinzi wa rais Magufuli!.

Mshangao huo wa Samia umekuja baada Freeman Mbowe kuonekana akihoji kwa nini ulinzi wa rais Magufuli umekuwa mkubwa sana!, mama Samia amewataka Chadema na watanzania wengine wenye roho za korosho kwa maendeleo ya nchi yetu kubadilika na kuanza kutangaza maendeleo ya nchi badala ya kutangaza upuuzi wa kuhoji ulinzi wa rais!

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante mama kwa Maelezo mazuri sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja nirudi kwenye Uzi wa Simba nikashangilie timu yangu!
 
Rais wa Nchi Dr. JOHN MAGUFULI leo hii tarehe 13 Aprili anazindua rasmi ofisi za Rais Ikulu Makao Makuu Chamwino Dodoma.

Pia Rais Magufuli anazindua mji mpya wa Serikali eneo la Mtumba.

Hii ni kuashiria kuwa ni rasmi sasa Rais anahamia Dodoma, makao makuu ya nchi.

Matukio haya yanashuhudiwa na viongozi wote wakuu wa nchi akiwemo Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri na Mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania.

Fuatilia uzi huu kwa updates.

updates......
Rais na msafara wake ameshawasili hapa na sasa ni dua maalum kutoka kwa viongozi wa dini.
updates......waziri mkuu anaongea hivi sasa, anampongeza rais kwa hatua yake ya kuamua kuhamishia makao makuu ya nchi dodoma ambayo ni ndoto ya mwasisi wa taifa hili Julius kambarage Nyerere. anasema ujenzi wa majengo ya ofisi ya rais yanakamilika mwezi mei wakati ofisi ya waziri mkuu yanakamilika mwezi huu wa nne.

updates............
sasa makam wa rais anahutubia. anampongeza rais kwa hatua hii muhimu ya kukamilisha azma ya kuhamia Dodoma. anasema tutahakikisha tunaitumia vizuri fursa hii ya kuhamia dodoma kuijenga Tanzania

Rais anasema ndoto ya kuhamia Dodoma iliazimiwa miaka kumi baada ya mwaka 1978.

Anasema kuhamia dodoma sio kazi rahisi...Lakini leo nimefrahi mnooo kuona ndoto ya baba wa taifa imetimia. Hata watz wamefurahi mno kuona malengo yao yametimia.

Na mimi nakuja Dodoma, nilichelewa kidogo kwa sababu nauguliwa na mama yangu ambaye hadi sasa hawezi kuongea hawezi kufanya chochote, lakini kwa sasa nahamia Dodoma, sipo mbali ni kama nimeshahamia tu.

Kuhusu vijana wa JKT walioshiriki kikamilifu kazi ya kujenga makao makuu haya nawaajiri rasmi lakini CDF usichomekee idadi, wale wa Mirerani walishaajiriwa na wamemaliza mafunzo juzi. Walijenga nyumba za Ikulu, wanaojenga ukuta wa Ikulu mle ndani, waliojenga nyumba za magereza hao ndio nimewaajiri.

Naongeza na wale wanaofanya kazi kwenye kiwanda cha mlale. Hao wote ndio tutapanga mikakati nao, kaa na wakuu wenzio wa vyombo.. Kaa na TAKUKURU, Magereza,TISS,Polisi nk tuwatumie hawa vijana.

Aliyesimamia hapa kuanzia leo anakuwa Brigedia, muongezee vinavyotakiwa kukaa kwenye mabega.Kuanzia leo tuwe na kikosi cha ujenzi na mkuu wake ni huyu niliyempandisha cheo hapa.

CDF unafanya vizuri sana, nakutuma mengi unafanya hivyo hivyo wanaotamani ustaafu leo haustaafu labda uharibu.Umetoa hadi gawio la milioni 700 haijawahi kutokea, nasubiri gawio la Polisi, Magereza nk
Mbona hata kapicha hujatupia mkuu?
 
Back
Top Bottom