LGE2024 Dodoma: Rais Samia ashiriki zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la Wapiga Kura kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

LGE2024 Dodoma: Rais Samia ashiriki zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la Wapiga Kura kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Leo Oktoba 11, 2024, Rais Dkt. Samia anaongoza watanzania katika zoezi la kujiandikisha katika daftari hili ili kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.


View: https://www.youtube.com/live/oreFWNwWmTY?si=mpNgbVFGvb8Q81HQ

Snapinsta.app_462112896_18347708302193701_1707065649549765930_n_1080.jpg

Rais Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama kwenye foleni ya wakazi wa Kijiji cha Chamwino mkoani Dodoma katika zoezi la kujiandikisha katika Daftari la Mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu.

Snapinsta.app_462431970_18347708257193701_8857358113086742788_n_1080.jpg

Rais Samia Suluhu tayari akijiandikisha kwenye Daftari la Mpiga Kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, katika Kitongoji cha Sokoine Kijiji cha Chamwino mkoani Dodoma.

NENO LA RAIS SAMIA KWA WANANCHI
Kupiga kura hakuna dini. Hakuna kiongozi asiye na kiongozi. Ili mradi wanakaa mtaa huo, viongozi wetu wa dini hawa hapa, wamekuja kujiandikisha. Leo ni furaha kwangu na nimshukuru Mungu kwamba leo tumeanza zoezi la kujiandikisha. Na mimi nikaona nisipoteze muda nikasema niwahi leo leo kujiandikisha mtaani kwangu kwasababu kesho nitaelekea Mwanza kwenye shughuli… nikitoka huko shughuli zetu hazitabiriki.

Kwahiyo nashukuru nimemaliza na ninawaomba wooote hapa kila mmoja akajiandikishe kwasababu kuna ubabaifu unajitokeza; wengeine wanafikiri wakishajiandikisha kwenye daftari lile la Tume ya Uchaguzi, hana haja ya kujiandikisha huku. Hapana! Tunajiandikisha kule kwa uchaguzi wa mwakani, lakini hapa kwenye eneo lako unamchagua M/kiti wako wa Kitongoji na Kamati yake na viongozi wengine. Ni daftari jengine tofauti.

Kwahiyo, niwaombe wengine wote kuanzia leo nadhani mpaka tarehe 20 mwezi huu ni kipindi chote hiki cha kujiandikisha. Kila mmoja kwa nafasi yake tukajiandikishe.

Suala lingine ni kwamba uchaguzi huu au zoezi hili lina umuhimu wake. Umuhimu wake ni kwamba viongozi hawa tunaowachagua wanatusaidia kuweka usalama na amani kwenye maeneo yetu. Utambuzi wa watu kwenye maeneo yetu ni dhamana yao – nani kaingia, nani katoka, nani ana shughuli gani nan ani hana shughuli, kesi ndogo kwenye naeneo yetu n.k..

Hata nmimi, pamoja na makuta yale (ya Ikulu) nikiwa najaza fomu naulizwa mwenyekiti wangu wa Kijiji na inabidi nimfuate, nipate idhini yake, muhuri wake ndiyo nipate huduma nyingine. Sasa jiulize, usipokwenda kumchagua na ukachaguliwa, ukawekewa ambaye hukudhania ungewekewa, au jengine…

Tunapofanya shughuli zote hizi za maendeleo, hawa ndiyo wa kwanza katika maeneo yao tunawasukuma wawe mbele watoe watu washiriki. Sasa akiwa mzembe utaanza kualamika kuwa kiongozi ni mzembe, lakini hukwenda kumchagua. Ukienda kumchagua, kura yako na mwingine na mwingine, utaweka yule ambaye si mzembe na anayefaa kuwatumikia.

Lakini pia zoezi hili ni uhuru wa demokrasia na tamaduni za nchi yetu. Katiba yetu imeweka mfumo huu wa tawala za mikoa… Sasa usiposhiriki, unakiuka katiba inayokuongoza ndani ya nchi yako. Kwahiyo mfumo huu, ni mfumo wa Kikatiba n ani haki ya kila mtu kushiriki kuchagua au kuchaguliwa.

Sasa nataka nizungmze la kuchaguliwa. Kwenye kuchaguliwa, tunaambiwa kila mwenye miaka kuanzia 21 mkimuona ni mzuri mweney sifa, mwingiliano mzuri na watu, yupo mbele kwenye shughuli za maendeleo– wa jinsia yoyote ile – akijitokeza kuomba kuchaguliwa, basi mchagueni. Na mmmemuona anafaa lakini yupo nyuma, hataki kwenda anaogopa labda atashindwa, lakini mna uhakika ni mzuri atasaidia, msukumeni. Mwambieni hebu nenda tukuone.

Zoezi hili ni la kila mwenye sifa. Wanaomba, tunachujana vizuri bila kupendeleana, na wale wazuri tunawapeleka wakashindane na wakiibuka ndio viongozi wetu. Si ndiyo?

Niwaombe sana zoezi lifanywe kwa usalama, lifanywe kwa amani, ili tusitie sdoa kwenye nchi yetu. Tumalize chaguzi zetu hizi za awali salama.

Niwakumbushe kuwa uchaguzi huu ndiyo unaotoa taswaira ya uchaguzi ule mkubwa tunaokwenda nao. Kwahiyo niwaombe sana wanachi, twendeni tukachague vyema ili tupate taswira halisi ya kule mnele tunakoelekea.
 
Tanzania ya Samia katika historia ya kukumbukwa na vizazi vijavyo. Uchaguzi utafanyika siku ya jumatatu, ni siku ambayo haitakuwa na muingiliano wa kiimani na dini zinazotambulika katika nchi yetu, Tumpongeze Rais Samia kwa jambo
 
Back
Top Bottom