Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais Samia akishiriki Maadhimisho ya Siku ya Sheria Nchini katika viwanja vya Chinangali-Park Dodoma Februari 3, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
"Kwa mwaka 2024 Jumla ya mashauri 172, 301 yalisajiliwa na kumalizika katika mfumo wa mtandao katika ngazi ya mahakama za mwanzo. Aidha mashauri 70,714 yalisikilizwa na kumalizika kwa njia ya mtandao kuanzia ngazi ya mhakama za wilaya hadi mahakama kuu" - Rais Samia Suluhu Hassan
"Sauti za Wananchi wengi zinatamani tanzania ya miaka 25 ijayo iwe ni Taifa jumuishi lenye ustawi haki na kujitegemea. (....) Kwamba miaka 25 ijayo tunataka Tanzania iwe ni Tifa jumuishi lenye ustawi, haki na linalojitegemea" - Rais Samia Suluhu Hassan
"Dira ijayo itaweka lengo la kuongeza pato la Taifa hadi kufikia Dola Bilioni 700 ifikapo mwaka 2050, sasa ili tuweze kufikia hapo tunalazimika kuchukua hatua za kukuza sekta za kiuchumi ikiwemo kuvutia uwekezaji na biashara, kuvutia mitaji nchini na kukuza njia za ukusanyaji wa mapato nchini" - Rais Samia Suluhu Hassan
"Tunakokwenda miaka 25 ijayo tunakwenda kuwa Taifa kama ilivyo dunia litakalopunguza matumizi ya fedha taslimu mkononi au cashless nation. lakini pia tunakwenda kupambana na mifumo ya fedha za mitandaoni au fedha za hewani" - Rais Samia Suluhu Hassan
"Serikali inatambua mazingira magumu ambayo watumishi wa mahakama wamekuwa wakifanyia kazi. Ili haki iweze kutamalaki na kushamiri na maslahi ya Taifa letu yalindwe vyema kama alivyosema rais wa TLS ni wajibu wa serikali kutengeneza mazingira mazuri na vivutio kwa utendji wa mahakama" - Rais Samia Suluhu Hassan
"Nyinyi majaji na mahakimu ni mawakala wa utoaji haki hapa duniani ila mmenyimwa Jaala na Kudra hizo sifa hamna, uwezo huo hamna. Kwahiyo mnafanya kazi yenu kwa kufuata makubaliano yenu kikatiba na sheria za nchi kama tulivyoziweka. Niwasihi sana, niwaombe sana tusiwe miungu watu hatuna sifa ya kudra wala jaala tutoe haki kwa misingi ile ambayo tumekubaliana na kuiweka kisheria".
Sehemu ya hotuba ya Jaji mkuu wa mahakama Tanzania Prof. Ibrahim Juma
Jaji mkuu wa mahakama kuu Tanzania Prof. Ibrahim Juma amewataka wananchi kutumia Call Center ya mahakama ambayo ipo wazi siku zote za wiki kwa saa 24 kwa ajili ya kutoa maoni na mapendkezo na wasisubiri tu hadi wiki ya sheria.
Prof. Ibrahim Juma ameeleza kuwa mahakama ipo tayari kuwasaidia chama cha mawakili Tanganyika kuweza kubuni mikakakti ya kuweza kufikia rasilimali ambazo zitakuwepo katika dira ya 2050.
Prof. Ibrahim amemshukuru Rais Samia Hassan kwakuwezesha mahakama kupata fedha kutoka benki ya dunia mara mbili. Dola Milioni 61 kwa awamu ya kwanza, na dola milioni 91 kwa awamu ya pili.
rais wa TLS
"Tunaposhirikiana na Serikali hatulambi asali, tunapata changamoto watu wanapoona tunashirikiana na serikali wanafikiri tunalamba asali. TLS siyo kikundi cha magaidi It's a structural body kwahiyo sehemu ya kuonya tutaonya kwa haki na pakupongeza tutapongeza kwa haki" -Mwabukusi, rais wa TLS
Wakili Mwabukusi ataka mkazo uwekwe kwenye sheria zinazolinda rasilimali, kwa kuwa kila taifa lina bargaining card na hivyo hivyo bargain Card ya Tanzania ni mali na rasimali hivyo ni vyema kuweka mkazo katika kuzilinda.